Akiwa kwenye mkutano na wananchi Kigoma, leo Novemba 29, 2024 Zitto ameongea mengi:
- Amewaonya CCM kuwa wanachofanya kwa sasa kitawageuka kama inavyotokea nchi nyingine.
- Ametolea mfano yanayoendelea Angola na Msumbiji kuwa Vyama tawala vilitegemea Vyombo vya Dola kubaki madarakani
- Ameonya kuruhusu Taifa kuendeshwa na Vyombo vya Dola badala ya Demokrasia iliyowekwa kikatiba
- Asema Chama cha Siasa ambacho kinashindwa kushawishi wananchi na kuishia kuegemea Dola, siku kinaondoka madarakani hakitajua. Na kudondoka kwake kutakuwa kwa mshindo mkubwa sana
- Ameongeza kuwa Vyombo viwili vya Dola vimeshaingizwa kwenye siasa (Polisi na Idara ya Usalama)
Namnukuu:
Nataka nimwambie mwenyekiti wa CCM Rais Samia, kama kuna kosa ambalo CCM wanafanya ni kusurrender siasa kwa vyombo vya ulinzi na usalama. Vyombo vya Usalama vikishaonja madaraka ya kisiasa kama hivyo unavyofanya watakaofata kushughulikiwa ni CCM wenyewe, hivyo vyombo vitawaondoa CCM Madarakani.
Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Tunayoyaona ayantokea Angola, Mozambiki ni makosa ya FLELIMO na MPLA kusarenda kisiasa kwa vyombo vya dola ndio maana muda wote wangu wote nilivyokuwa mbunge katika jambo nililokuwa nalipigania kwa nguvu zangu zote ni kuiondoa Idara ya Usalama wa Taifa katika makucha ya CCM, nikawapigania mageuzi ya TISS kwasababu ni kosa kubwa sana kuiondoa nchi kwenye democracy na kuipeleka kwenye nchi inayoongozwa na vyombo vya dola.