Unafikiri sifa kuwa na kitambi!!

Unafikiri sifa kuwa na kitambi!!

Hiyo kitu inakera zaidi kwa kina dada. Mwanaume si vibaya akiwa na kitambi. Ila sasa kuna midada imeshamiri kwa vitambi vya bia za ofa.
Yaani hamna janamke linalinikera kama lenye kitambi cha bia za ofa.
 
Hamjambo waungwana wangu

Mwenzenu leo sasa nimeingia kwa kupindapinda na kunyooka kiasi
Ishu niliyoingia nayo leo ni khusu hawa ndugu, marafiki, makaka na
mababa zetu kiujumla sitaki kuwaita majina ya ajabu kama vijiweni
wanavyowaita ninawaita kwa heshima na adabu kubwa sana kwani
pasipo hao sisi tusingekuwepo kwani tumetoka katika ubavu wao
au natania wakinadada jamani!! wengi watasema sitanii bali nasema
wazi tena wazi kabisa.


Mwenzenu nimekaa na kutafakari sana ndani ya mooyo wangu na
na nimekuja na hiki kitu ambacho kimenishangaza na pengine kime-
nifanya niduwae sana, na wakati mwingine kimenifanya nione kioja
kwangu. Jambo ambalo limenifanya nilisema hapa ni kuhsu hawa
makaka, mababa, zetu jamani wengi wao siku hizi ukipishana nao
utasema alhamndulilahi Mungu amewaridhia sana na kuwakumbuka
yaani wengi wao siku hizi wana vitambi utafikiri wamebeba kila 50
za mahindi kwenye hilo tumbo, na wengine utaona wanavaa vishati
vya kuwabana ili kitambi kionekane, wengine wanadiriki kusema kuwa
ni fashion imeingia kwao. Jamani fashion hata kwa vitambi mm sijawahi
ona kabisa kuwa hata mwili nao ni fashion.

Wao wanaona sifa kuwa na kitambi, eti kwao nifahari, wewe uliona wapi
kuwa na kakitambi ni fashion jamani, si maradhi hayo jamani, yani
unakaribisha maradhi mwenyewe mwilini mwako wewe nenda kwa
doctor akupime utaona kuwa kama huna kwashiakoo au utapiamlo
bandugu makaka, mababa zetu sio sifa kuwa na kitambi namna hiyo
kwani hata akina dada, mama, wanawake hawapendi mwanaume
mwenye kitambi namna hiyo, atampeleka wapi mtu mwenye kitambi?
Mimi mwenyewe Ladyf sipendi kuwa na mume mwenye kitambi utafikiri
anaumwa utapiamlo, kumbe mwenyewe ni sifa tu na kusema yuko
kwenye fashion,

Wanaume nawasihi jamani punguzeni hizo tumbo zenu, fanyeni mazoezi
ya viungo, na fanyeni shughuli ambazo zitawapunguzia hizo mizigo ya
vitambi kwani kuwa na kitambi ni ugonjwa jamani. Maradhi mengine
tunayatafuta wenyewe kwa kula sana, yaani mwanaume wa siku hizi
bila kumsongea ugali unga 4kg hali anasema ni kidogo jamani mbona
mnatukondesha wake zenu hivyo. utafikiri unawapikia watu 10 hicho
chakula kumbe ni mmoja ndiye anayekula. Waungwana kaka zangu
wa jf acheni sifa ya kuwa na kitambi ni ugonjwa mnakaribisha.


Namshukuru Mungu mm ladyf kwani mume wangu Mentor ana
kitambi na wala hapendi kuwa na kitambi kabisa maisha mwake,
nimefurahi sana tena sana kuona nina mume asiyependa kuwa na kitambi,
kazi hiko kwa wadada, wanawake wenzangu ambao wana wanaume
walio na vitambi, acha niwasaidie jamani akinadada wenzangu. Nikiwasihi
wanaume jamani punguzeni kuwa na vitambi na nyie mlio na vitambi
fanyeni mazoezi ya viungo vitapungua hivyo
SIO SIFA KUWA NA KITAMBI
NA HATA SHEPU UNAIHARIBU BURE NA UKITAKA KUVAA SUTI INATUNA OVYO
UNAKUWA TOO SHEPULESI.


Hebu angalia picha ya wenye vitambi wanavyoshindwa kufanya kazi za muhimu



Hawa ulikutana nao wapi? Mbona kama picha za faragha hizi, ni mrithi wa penzi lako nini?
 
Nishawahi kumshuhudia mdada mmoja ana kitambi kikubwaaaa kama kapigwa zongo,halafu kavaa kitop kinavutika kuelekea juu, kila akikishusha wala hata hakikai vizuri kinarudi juu kama tiara kwenye tufani ya upepo...
Yaani tumbo limevimbiana kama katoka kufakamia ubwabwa wa hitma na ndizi kisukari halafu kashushia na juisi ya Ribena...
Chini kavaa kitu kama kanyela mumo wenyewe sijui mnaziita skini taiti sijui legingi...
Yaani hiyo shepu yake ukimwangalia, unaweza kujiuliza kitunguu kimetoka shambani kutafuta nini barabarani!!!...
Huku pembeni kwenye mbavu sasa, kuna pingili za nyama uzembe kama mistari ya mahindi kwenye kigunzi...
 
ladyfurahia
kwanza siungi hiyo hoja mkono
sababu ni kwamba siyo akina baba tu wana vitambi
mbona akina mama nasi matumbo ndo yanazidi kuwa makubwa
nitakubaliana na mtoa mada akisema vitambi vimezidi kwa akina mama na akina baba pia.

kwa kwa kwaaaaaa acha nicheke mie jamani vitambi wengine vinawatokka hata kabla hawajaoa sasa sisis akina mama tunawapa hivyo vitambi si wao wenyewe wanajiendekeza ovyo llkwa ulafi wao jamani he he hee heeee Mamndenyi na gfsonwin njoo mnisaidie huku jamani naumia mbavu zangu he hee heeeeee heeeeee
 
Last edited by a moderator:
Mama kitambi kina raha yake lakini kisiwe too much. Ukikonda sana napo suti hazikai inakuwa kama zimechomekwa kwenye jiti.
 
- wanaume wengi wanaota vitambi kwa sababu wanakunywa sana bia na nyama choma, na kinachowavutia huko baa ni wanawake

...............mmmmmmhhhhhhh?????????????
 
Wanawake ndo mnaosababisha wanaume wawe na vitambi, so mjilaumu wenyewe
- wanaume wengi wanaota vitambi baada ya kuoa...
- wanaume wengi wanaota vitambi kwa sababu hawafanyi mazoezi, mda wa mazoezi wanakuwa kwa wanawake
- wanaume wengi wanaota vitambi kwa sababu wanakunywa sana bia na nyama choma, na kinachowavutia huko baa ni wanawake
- wanaume wengi wanaota vitambi maana hawafanyi kazi za mikono kama kufua, kudeki, kupika kwa kuwa hizo kazi zimehodhiwa na wanawake

Kwa hiyo anza kubadilika wewe ladyfuraha...

Mkuu utasababisha tunyimwe kwenda bar sasa, ........................!:frusty:
 
Ha haa haa haa haaaaa jamani kaka bhaana wakati mwingine, nimeipenda signature yako tu imenivutia tena sana
Aisee ni ugonjwa hasa kwa wanawake maana kwanza hawapendezi tena ila kwa wanaume kitambi kinafanya kazi iwe ngumu hadi wakati mwingine kifanyio kudisappear kabisa

Copy kwa The secretary
 
nazungumizia kitambi kilichovuka mipaka na sio kitambi cha kawaida cha chakula, kwani nani amekwambiakuwa ukiwa mwembamba suti hazikupendezi acha kujidanganya wewe zinakaa tena sana inategemea umekwenda dukani ukachagua saizi gani kwako na isiwe oversize kwani ndo inakuwa imechomekwa au wewe umekamatwa nini?
Mama kitambi kina raha yake lakini kisiwe too much. Ukikonda sana napo suti hazikai inakuwa kama zimechomekwa kwenye jiti.
 
ngoja niingie tena dimbani nilete matukio ya wanawake nayo mchangie naona sasa mnataka nanyi pia mtajwe pia hapa, lakini hayo yote ni mambo ya BEIJING jamani
ladyfurahia
kwanza siungi hiyo hoja mkono
sababu ni kwamba siyo akina baba tu wana vitambi
mbona akina mama nasi matumbo ndo yanazidi kuwa makubwa
nitakubaliana na mtoa mada akisema vitambi vimezidi kwa akina mama na akina baba pia.
 
nazungumizia kitambi kilichovuka mipaka na sio kitambi cha kawaida cha chakula, kwani nani amekwambiakuwa ukiwa mwembamba suti hazikupendezi acha kujidanganya wewe zinakaa tena sana inategemea umekwenda dukani ukachagua saizi gani kwako na isiwe oversize kwani ndo inakuwa imechomekwa au wewe umekamatwa nini?
Jaribu kusoma tena hoja yangu vizuri, nimezungumzia wote mama wanene kwa wembamba nikasema lakini isiwe too much.
 
mwambie wewe huyo maana hata mengi pia ana kitambi mengi.jpg
Kwa hiyo Bill Gates ana bonge ya kitambi sio, akenajo?
 
Back
Top Bottom