Unafikiri sifa kuwa na kitambi!!

Unafikiri sifa kuwa na kitambi!!

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Hamjambo waungwana wangu

Mwenzenu leo sasa nimeingia kwa kupindapinda na kunyooka kiasi
Ishu niliyoingia nayo leo ni khusu hawa ndugu, marafiki, makaka na
mababa zetu kiujumla sitaki kuwaita majina ya ajabu kama vijiweni
wanavyowaita ninawaita kwa heshima na adabu kubwa sana kwani
pasipo hao sisi tusingekuwepo kwani tumetoka katika ubavu wao
au natania wakinadada jamani!! wengi watasema sitanii bali nasema
wazi tena wazi kabisa.


Mwenzenu nimekaa na kutafakari sana ndani ya mooyo wangu na
na nimekuja na hiki kitu ambacho kimenishangaza na pengine kime-
nifanya niduwae sana, na wakati mwingine kimenifanya nione kioja
kwangu. Jambo ambalo limenifanya nilisema hapa ni kuhsu hawa
makaka, mababa, zetu jamani wengi wao siku hizi ukipishana nao
utasema alhamndulilahi Mungu amewaridhia sana na kuwakumbuka
yaani wengi wao siku hizi wana vitambi utafikiri wamebeba kila 50
za mahindi kwenye hilo tumbo, na wengine utaona wanavaa vishati
vya kuwabana ili kitambi kionekane, wengine wanadiriki kusema kuwa
ni fashion imeingia kwao. Jamani fashion hata kwa vitambi mm sijawahi
ona kabisa kuwa hata mwili nao ni fashion.

Wao wanaona sifa kuwa na kitambi, eti kwao nifahari, wewe uliona wapi
kuwa na kakitambi ni fashion jamani, si maradhi hayo jamani, yani
unakaribisha maradhi mwenyewe mwilini mwako wewe nenda kwa
doctor akupime utaona kuwa kama huna kwashiakoo au utapiamlo
bandugu makaka, mababa zetu sio sifa kuwa na kitambi namna hiyo
kwani hata akina dada, mama, wanawake hawapendi mwanaume
mwenye kitambi namna hiyo, atampeleka wapi mtu mwenye kitambi?
Mimi mwenyewe Ladyf sipendi kuwa na mume mwenye kitambi utafikiri
anaumwa utapiamlo, kumbe mwenyewe ni sifa tu na kusema yuko
kwenye fashion,

Wanaume nawasihi jamani punguzeni hizo tumbo zenu, fanyeni mazoezi
ya viungo, na fanyeni shughuli ambazo zitawapunguzia hizo mizigo ya
vitambi kwani kuwa na kitambi ni ugonjwa jamani. Maradhi mengine
tunayatafuta wenyewe kwa kula sana, yaani mwanaume wa siku hizi
bila kumsongea ugali unga 4kg hali anasema ni kidogo jamani mbona
mnatukondesha wake zenu hivyo. utafikiri unawapikia watu 10 hicho
chakula kumbe ni mmoja ndiye anayekula. Waungwana kaka zangu
wa jf acheni sifa ya kuwa na kitambi ni ugonjwa mnakaribisha.


Namshukuru Mungu mm ladyf kwani mume wangu Mentor ana
kitambi na wala hapendi kuwa na kitambi kabisa maisha mwake,
nimefurahi sana tena sana kuona nina mume asiyependa kuwa na kitambi,
kazi hiko kwa wadada, wanawake wenzangu ambao wana wanaume
walio na vitambi, acha niwasaidie jamani akinadada wenzangu. Nikiwasihi
wanaume jamani punguzeni kuwa na vitambi na nyie mlio na vitambi
fanyeni mazoezi ya viungo vitapungua hivyo
SIO SIFA KUWA NA KITAMBI
NA HATA SHEPU UNAIHARIBU BURE NA UKITAKA KUVAA SUTI INATUNA OVYO
UNAKUWA TOO SHEPULESI.


Hebu angalia picha ya wenye vitambi wanavyoshindwa kufanya kazi za muhimu
 

Attachments

  • man1.jpg
    man1.jpg
    2.2 KB · Views: 1,228
  • man2.jpg
    man2.jpg
    2 KB · Views: 1,242
Last edited by a moderator:
hasa kwa wake wao ndio sababu maana hawajui vyakula gani kuwapikia waume zao
wee umepika ugali maharage tuu ofcoz lazima nile sana ili nishibe.
 
Wanawake ndo mnaosababisha wanaume wawe na vitambi, so mjilaumu wenyewe
- wanaume wengi wanaota vitambi baada ya kuoa...
- wanaume wengi wanaota vitambi kwa sababu hawafanyi mazoezi, mda wa mazoezi wanakuwa kwa wanawake
- wanaume wengi wanaota vitambi kwa sababu wanakunywa sana bia na nyama choma, na kinachowavutia huko baa ni wanawake
- wanaume wengi wanaota vitambi maana hawafanyi kazi za mikono kama kufua, kudeki, kupika kwa kuwa hizo kazi zimehodhiwa na wanawake

Kwa hiyo anza kubadilika wewe ladyfuraha...
 
lakini inategemea huyo mume anataka nini jamani maana mwingine anapenda sana ugali maharage ukimpikia lost maini anakukaripia kama mbogo vile sasa utafanyaje best si utampikia hicho chalkula akitakacho yeye ili yaishe bana
hasa kwa wake wao ndio sababu maana hawajui vyakula gani kuwapikia waume zao
wee umepika ugali maharage tuu ofcoz lazima nile sana ili nishibe.
 
Hebu angalia picha ya wenye vitambi wanavyoshindwa kufanya kazi za muhimu[/QUOTE]

Hapo kwenye red nadhani you need bo be more specific, when you say kazi za muhimu what do you mean mdada.

Ushauri wako ni wa muhimu lakini na wewe ama ninyi wanawake mna mchango mkubwa kumfanya mwanaume kupatwa na hicho unachoita ugonjwa na wengine upande wa pili wakiita fasion ama dalili ya pesa nk, kumbe basi kila mtu atimize wajibu wake ili kunusuru hiyo hali.
 
kwa kwa kwaaaaaa acha nicheke mie jamani vitambi wengine vinawatokka hata kabla hawajaoa sasa sisis akina mama tunawapa hivyo vitambi si wao wenyewe wanajiendekeza ovyo llkwa ulafi wao jamani he he hee heeee Mamndenyi na gfsonwin njoo mnisaidie huku jamani naumia mbavu zangu he hee heeeeee heeeeee
Wanawake ndo mnaosababisha wanaume wawe na vitambi, so mjilaumu wenyewe
- wanaume wengi wanaota vitambi baada ya kuoa...
- wanaume wengi wanaota vitambi kwa sababu hawafanyi mazoezi, mda wa mazoezi wanakuwa kwa wanawake
- wanaume wengi wanaota vitambi kwa sababu wanakunywa sana bia na nyama choma, na kinachowavutia huko baa ni wanawake
- wanaume wengi wanaota vitambi maana hawafanyi kazi za mikono kama kufua, kudeki, kupika kwa kuwa hizo kazi zimehodhiwa na wanawake

Kwa hiyo anza kubadilika wewe ladyfuraha...
 
Last edited by a moderator:
ni kweli ulichokiongea naunga mkono asilimia 100, labda tumwite spika wa bunge hili Baba V aje atoe jukumu au nimwite mbunge machachari Nicas Mtei ateme yake nini hapa leta hoja bro ukumbi ni wako hapa wasemaje?
Hebu angalia picha ya wenye vitambi wanavyoshindwa kufanya kazi za muhimu

Hapo kwenye red nadhani you need bo be more specific, when you say kazi za muhimu what do you mean mdada.

Ushauri wako ni wa muhimu lakini na wewe ama ninyi wanawake mna mchango mkubwa kumfanya mwanaume kupatwa na hicho unachoita ugonjwa na wengine upande wa pili wakiita fasion ama dalili ya pesa nk, kumbe basi kila mtu atimize wajibu wake ili kunusuru hiyo hali.[/QUOTE]
 
Last edited by a moderator:
mm siwaumbui bana natoa hoja yangu ukitaka kuunga mkono unga, usipotaka achana nao eti spika Baba V unakubaliana nami hapo au nimwite mbunge wa jimbo la kusini kaskazini watu8 aje atoe yake hapa, huyu hapana ataaribu bure hapa namwita Mtambuzi atoe hoja mheshimiwa sipika mwongozo tafadhali hapa
Wewe acha kutuumbua bana kitambi ni dalili ya kuwa na fedha
 
Last edited by a moderator:
hee! jamani kuwa na kitambi ni ugonjwa bana asikudanganye mtu hapo eti Mentor, Filipo, watu8 na kaka yangu Erickb52 kuwa na kitambi ni kuwa na fedha nyingi? pls nijibuni
Aisee ni ugonjwa hasa kwa wanawake maana kwanza hawapendezi tena ila kwa wanaume kitambi kinafanya kazi iwe ngumu hadi wakati mwingine kifanyio kudisappear kabisa

Copy kwa The secretary
 
Last edited by a moderator:
Kwanza ukiwa na kitambi hata kwenye mechi za ugenini unashindwa kushughulika vyema.
 
lakini unajua kuwa kuna tofauti kati ya kuwa na tumbo kubwa na kitambi? kuwa na tumbo kubwa ni maumbile ya mtu hata kama atafanya mazoezi atakuwa mwepesi lakini tumbo laweza lisipungue tofauti na mwenye kitambi.

lakini pia kitu kizuri au kibaya ni macho ya anayekiangalia na fikra zake juu ya anachokiona. hivyo wapo wanawake wanapenda wanaume wenye vitambi na wapo wasiowapenda, hiyo ni sawa na baadhi ya wanaume kuwapenda wanawake wenye makalio makubwa na wengine kutowapenda.

ukiipenda pespsi usimshangae anayependa fanta.
 
Mwanaume wa siku hizi
bila kumsongea ugali unga 4kg hali anasema ni kidogo
jamani mbona
mnatukondesha wake zenu hivyo. utafikiri unawapikia watu 10 hicho
chakula kumbe ni mmoja ndiye anayekula.

Kwahiyo Mentor anakula kilo 4 mwenyewe? Dah!!!! Nilikua sijui!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Huku kwetu moja ya kigezo cha kupewa angalau ka udiwani ni kuwa na KITAMBI...unanekana huna njaaa... Chezeya heshima ya kitambi weye
 
Back
Top Bottom