Unafiki wa wasanini sio mzuri

  • Thread starter Deleted member 421398
  • Start date
D

Deleted member 421398

Guest
Wasanii wa kwetu hapa ni wa ajabu sana yaani waliwekwa ndani wakina TID na wenginao ila hapakuwa na hata mmoja aliekuwa akipost picha zao na kuwapa maneno ya faraja ila sasa kawekwa Vanessa Mdee sasa kila kona kwenye social media wanapost picha zake na kumpa maneno ya faraja.

Hapo ndio unajua kuwa watu wana makundi yao na hakuna umoja ni unafki tu na uzandiki wa hali ya juu.
 
Kwa hiyo ulitaka tuendelee kukausha tu kama hatujui linaloendelea
 
Kaka hali ya kumfariji MTU ktk matatizo ni jinsi gani huyo muhusika anakaa na jamii.

Hao wanaopost hawakukaa kikao ila kila MTU kwake na ana post hizo faraja

Si unafikiri wala uzandiki ila ni mahusiano aliyonayo na mhusika
 
Huwezi kuwa rafiki wa kila mtu. Hata waliopo kazini, sio kila mfanyakazi ni rafiki yako wa karibu. Hivyo, kutokufanya chochote kwa mtu asiyekaribu nawe sioni kwanini uwe unafiki
 
Kwa hiyo ulitaka tuendelee kukausha tu kama hatujui linaloendelea
Kama unaoa hivyo ni sahihi sawa kausha tu si unajua kila mtu anakuwa na utashi wake
 
Mkuu si ndio maana wanaitwa "Wasanii"

Au hujui "Msanii" ni mtu wa aina gani!!!!?
 
Hao wasanii ni kama jirani zako tu hapo mtaani ukiishi nao poa lazima watakua nawe kwenye kila jambo ila kama picha haziendi basi siku nyumba yako ikiwaka moto watakuja na petroli wakisema maji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom