bado sijaamini pamoja na kumkoboa magamba yote nufu mfu lakini bado anajipendekeza kwa ccm? nafikiri msumari wa mwisho wa yeye na pacha wake sitta ndiyo huu kwamba waliudanganya umma kuhusu Richmond - nasubiri movie ianze.Watu wa JF wanamwabudu mwakyembe kama Mungu na wanamwita JEMBE. Hawawezi kukuelewa kama mwakyembe ni janga kuliko maelezo lakini anajua kucheza na media na akili za watanzania.
NI MIMI NA WEWE TU WENYE UPEO MDOGO WA KUFIKIRI TULIOJAA UPUMBAVU NDO TUNAONA ILIFAA SERIKALI IINUNUE MITAMBO HII TOKA MWANZO LAKINI WENYE AKILI PEVU NA PANA KIMTAZAMO WALISHAONA KUWA MITAMBO HII ILIPASWA KUBINAFSISHWA BURE BILA YA KUTOA HATA SHILINGI ILA KWA KUWA TUNA VIONGOZI WEPESI NA DHAIFU KIUTENDAJI NDO WALIOSABABISHA YOTE HAYA MPAKA TUNATAKIWA KULIPA FIDIA NA GHARAMA ZA KESI ZA DOWANSI. SASA KOSA NI LA NANI HAPO?
1. Mwakyembe na Sita - waliounda na kuwa katika tume ya kubaini ukweli wa jambo husika Richmond
2. Lowasa na Rostam - wamiliki wa Richmond na Dowans
3. Bunge - Taasisi iliyojadili na kutolea uamuzi suala hisika la Richmond na Dowans
4. Serikali - Taasisi iliyotakiwa kutekeleza maazimio ya bunge ikiwemo kubinafsisha mitambo
SASA KAMA UNA AKILI PANA UTAPATA JIBU KUWA NI NO.4 LAKINI KAMA NA WEWE UNA AKILI SAWA NA MIMI KIAKILI JIBU LAKE HAPO NI NO.1
NA WENYE JIBU NO. 1 WOOOTE NDIO HAO WALIYOKO CCM WANAOTULETEA MAJANGA NDANI YA TAIFA LETU.
Hivi hapa kosa la Mwakyembe na Sitta ni lipi? Kamati ya bunge iliyoongozwa na Mwakyembe kazi yake kubwa ilikuwa ni kuchunguza uhalali wa mkataba wa Richmond pamoja na uwezo wa kampuni yenyewe wa kuzalisha umeme na ilidhihirika kwamba mkataba ulikuwa na matatizo na kampuni yenyewe haikuwa na uwezo, kwa hiyo hapo kosa la hao watu ni lipi?
Kama ni kumsafisha huyo Lowasa basi rudi ukamwambie akufungashie na brush kabisa
Kosa lao kubwa ni kumwangusha Lowasa pekee na kuilinda serikali kwa kuficha mambo waliyoyaona. Kama serikali wakati ule ingeanguka, ni kweli tungepata hasara fulani lakini pia watu wangejifunza kuwajibika na huu utapeli usingeenelea kama ilivyo leo.
Ndiyo maana kuna wakati ninafika naona kwa kweli pamoja na mambo mengine rais Kikwete ni mvumilivu. Ebu jaribu kuwaza jinsi watu hawa walivyokuwa wanatangaza kila mahali wanataka kuuliwa na kwamba wanachukiwa sana kwa kuwa ni wapenda haki na wafichua mafisadi. Lakini rais kwa kujua ni njaa zao tu na uchu wa madaraka alipowapa uwaziri wote wametulia kana kwamba hawajawahi kuliletea taifa hili hasara za ajabu. Hivi mitambo hii si ndiyo ile Zitto alisema serikali iinunue wakamjia juu. Sasa kiko wapi? Sitta na Mwakyembe wana kesi ya kujibu kama siyo hapa duniani basi mbinguni. Halafu mbaya zaidi sana wote ni wanasheria.
Acha uchonganishi na kupandikiza chuki, nani kasema kuwa Richmond haikuwa kampuni feki na ya kubumba? kwani Lowasa alijiudhuru kwa sababu ya Dowans au Richmond? acha kujenga chuki kwa jamii bial kuwa na sababu za msingi.Dowans wameshinda kesi ya Kimataifa , fedha wanalipwa, mitambo walioisema chakavu imeuzwa na ndiyo inatumika mpaka leo.
Hawa wameisababishia taifa hasara kubwa sana. Kama serikali ingenunua hii mitambo tungekuwa tumekwepa kununua umeme kwa gharama kubwa sana.
Hawa watu hawastaili kuwa viongozi kabisa. Chuki walizokuwa nazo kwa Lowassa zimekuja kuigharimu nchi.
HAWA WATU NI HATARI KWA TAIFA HILI NI WAKUOGOPWA KULIKO UKIMWI
Sitta na Mwakyembe hawana kosa kama mleta maada anavyotaka kutuaminisha, acha ushabiki wakisiasa mwenye chuki mbaya unaoweza kubomoa umoja wa nchi.Hivi hapa kosa la Mwakyembe na Sitta ni lipi? Kamati ya bunge iliyoongozwa na Mwakyembe kazi yake kubwa ilikuwa ni kuchunguza uhalali wa mkataba wa Richmond pamoja na uwezo wa kampuni yenyewe wa kuzalisha umeme na ilidhihirika kwamba mkataba ulikuwa na matatizo na kampuni yenyewe haikuwa na uwezo, kwa hiyo hapo kosa la hao watu ni lipi?
Kweli mkuu hawa jamaa wanakesi ya kujibu. Siku zote njia za waongo ni fupi.
....Buchoo! jibu basi hoja za huyu great thinker!NI MIMI NA WEWE TU WENYE UPEO MDOGO WA KUFIKIRI TULIOJAA UPUMBAVU NDO TUNAONA ILIFAA SERIKALI IINUNUE MITAMBO HII TOKA MWANZO LAKINI WENYE AKILI PEVU NA PANA KIMTAZAMO WALISHAONA KUWA MITAMBO HII ILIPASWA KUBINAFSISHWA BURE BILA YA KUTOA HATA SHILINGI ILA KWA KUWA TUNA VIONGOZI WEPESI NA DHAIFU KIUTENDAJI NDO WALIOSABABISHA YOTE HAYA MPAKA TUNATAKIWA KULIPA FIDIA NA GHARAMA ZA KESI ZA DOWANSI. SASA KOSA NI LA NANI HAPO?
1. Mwakyembe na Sita - waliounda na kuwa katika tume ya kubaini ukweli wa jambo husika Richmond
2. Lowasa na Rostam - wamiliki wa Richmond na Dowans
3. Bunge - Taasisi iliyojadili na kutolea uamuzi suala hisika la Richmond na Dowans
4. Serikali - Taasisi iliyotakiwa kutekeleza maazimio ya bunge ikiwemo kubinafsisha mitambo
SASA KAMA UNA AKILI PANA UTAPATA JIBU KUWA NI NO.4 LAKINI KAMA NA WEWE UNA AKILI SAWA NA MIMI KIAKILI JIBU LAKE HAPO NI NO.1
NA WENYE JIBU NO. 1 WOOOTE NDIO HAO WALIYOKO CCM WANAOTULETEA MAJANGA NDANI YA TAIFA LETU.
EL arudishiwe uPM wake,
EL ni kichwa kuliko ma'CCM yote wewe.Kama akiwa PM alisema wafanyakazi wakiongezewa Mishahara nchi haitatawalika na mfumuko ndio huo wa bei, akirudishiwa watapona? Shame on you? Sasa wafanyakazi wariongezewa na imekuwa afadhali japo bado tulifanyiziwa saaana.
Hili mapema zitto
aliliona akashauri serikali inunue ile mitambo,lakini kwa sababu nchi ya
wanasiasa kila kitu kinaendeshwa kwa siasa hakuna cha maana,tunakuja
kukumbuka shuka kushakucha,mambo mengine yakitaalamu wangeachiwa
wataalamu wanasiasa wangekaa pembeni,lakini kila kitu tunaamuliwa na
wanasiasa maendeleo yatakuja mwaka 3000
Mkurugenzi mkuu wa TANESCO wakati ule alisema mitambo ile mizuri tununue. Wanasiasa uchwara sasa "oooh mitambo mitumba ile mibovuuu imechokaa hatuwezi kununua mitumba", huyu mwanasiasa anayewaambia hivi hata hana ushahidi wowote au hajatumia reference yeyote ya kitaalam zaidi ya kubwabwaja tu na hata ukimuuliza specifications za mitambo anayoizungumzia yeye hajui. Na hapo ndio nchi yetu ilipofika wakiongea wanasiasa ndio wanasikilizwa maana wao wanayo Platform ya kuzungumzia nani anawasikiliza wataalam waliopo vyuoni? ndio maana na wao wanataka kuwa wanasiasa siku hizi wanatafuta majimbo. Hawa wakina Sitta ni watu hatari sana we were two steps ahead wameturudisha 10 steps back , thank god tunaye rais ambaye ni mvumilivu otherwise wangekuwa CCJ sasa hivi.