Ukinyonga na unafiki wa Sitta na Mwakyembe wadhihirika

Ukinyonga na unafiki wa Sitta na Mwakyembe wadhihirika

John Okello

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2014
Posts
459
Reaction score
207
*Mtandao wao wa kumchafuwa na kumpoteza Lowassa wazidi kuparaganyika

kwa wasiofahamu Samweli Sita ni kiongozi Pekee aliyethibitika kuwahi kumuudhi Mwalimu Nyerere kiasi cha kupoteza Imaan naye...... akiwa mwanafunzi chuo kikuu Udsm kitivo cha Sheria Samweli Sitta aliendesha Mapambano ya wazi kupinga Mfumo wa uendeshaji wa Chuo hicho.... Dhahiri shahiri akidai baadhi ya huduma kutokidhi ubora kwa mahitaji ya wanachuo hao....

J.okello nakumbuka Mwalimu akiwa katika ziara yake chuoni udsm alikutana na maandamano ya vijana wa chuo kikuu udsm maanadamano yalioongozwa na mzee Samwel Sitta akibeba bango lililoongoza kuonyesha hasira za wanafunzi kwa serekali ya mwalimu bango la sita lilikuwa likidai "Aheri Mkoloni Mweupe kuliko mkoloni mweusi" kauli hii ilijengeka katika madai ya sitta na wenzie kudai kupatiwa chai na mkate au uji wenye blue band na maziwa

Hii inaonyesha namna sitta alivyoanza uasi kwa serekali akiwa kijana mdogo kabisa wa makamo.... Na kama unavyofahamu jasiri haachi asili........ Siasa za sita za usaliti na unafiki hazikuishia katika viunga vya udsm aliendelea nayo hata pale alipokuwa kiongozi wa chama na serekali

Mara kwa mara Samweli Sitta amekuwa rafiki ndumi lakuili kwa wapinzani wa ccm sababu ya siasa zake za upinzani dhidi ya serekali ya chama chake, john Okello nakumbuka Mzee Samweli Sita alikuwa moja ya wanamtandao waliompigania JK kuingia madarakani Mwaka 2005 huku akitarajia kupewa nafasi ya Uwaziri mkuu japo hakuwa na sifa hiyo.......Jk alipoingia madarakani alimwacha samweli sitta na kumtaka akagombee uspika wa bunge na haya yalikuwa maazimio ya mtandao.......

Samweli alionyesha kukasirishwa na uwamuzi wa kamati kuu ya mtandao wao,alikubali kugombea uspika kwa shingo upande, kazi kubwa aliyoifanya sitta ni kuihujumu serekali ya ccm chini ya jk.......issue kubwa ikiwa ni uwaziri mkuu

Kuibana na kuruhusu mijadala isiyo na tija bungeni ilikuwa ni ishara ya chuki za wazi na dhahiri kwa jk na timu yake ya mawaziri na ishu kubwa ikiwa ni uwaziri mkuu.......alichokifanya samweli sitta ndani ya chama ni kuungana na walewote walio mpinga na kumkataa jk wengine wakiwa wale walio tamka wazi wazi ya kwamba jk hawezi kuwa raisi wa tanzania na ikitokea hivyo wataama nchi na ndani ya bunge aliungana na wabunge walioongoza kampeni za kumkataa jk na kuweka wazi hawawezi kuongozwa na mtu mgonjwa........urafiki kati ya Samweli sita na Mwakyembe au Samweli Sita na nape Unaondoa Mashaka juu ya Mahusiano yenye dhamira ya kukikwamisha ccm na serekali yake.....

Mwaka 2008 katika sakata la Richmond sita na mwakyembe na jasusi mmoja aliyekuwa naibu waziri wa wakati huo walitumika kuihujumu serekali ya ccm kwa kupanga mbinu na mikakati ya kuibua tuhuma ya richmond kuisimamia na mpaka kupatikana kwa matokeo ya tuhuma hiyo....... Ikumbukwe hapa ndio mwanzo wa uswahiba wa samweli sitta Mwakyembe na Membe ulipozidi kukuwa kwa kasi.....

Kubwa ilikuwa wafanikiwe kuihujumu serekali ya jk na waziri wake mkuu bwana edward lowassa, mtandao huu uliratibiwa kwa ujasiri ujasusi na umakini mkubwa mno katika kufanikisha dhamira yao ya kumhuju jk kupitia kwa waziri mkuu wake......

*Dhambi ya Usaliti yaanza kuwarudia na kuwatesa

Baada ya kufanikisha misheni yao kila mmoja alirudi katika nafasi yake ilikutafuta maslai yake binafsi mwakyembe na sita waliendelea kuwa wamoja mpaka pale mwakyembe alipochaguliwa kuwa waziri katika serekali ya mtu aliyemuita dhaifu na hafai kuwa mkuu wa nchii huku akimuunga mkono mwandosya....

Jasusi mbobezi yeye baada ya kumaliza kazi ya kwanza ya kumfitinisha jk na wanamtandao wenzie kina rostam na Lowassa alihamia ndani ya chama akichochea kuni ya dhana mpya ya vua gamba iliopandikizwa kimafia na wanamtando waliojiunga makusudi kummaliza lowassa ndani ya chama.....

Huku pia akitumia mbinu za kikachero kuwamaliza baadhi ya wanamtandao hofu yake kubwa ikiwa ni uchaguzi wa mwaka 2015, hapa ndipo dhambi ya usaliti ilipomtesa mwakyembe baada ya kukumbwa na dhahama ya magonjwa ya kutengenezwa na majasusi yeye na mfuasi wake mwandosya ambao wao Walikuwa wakifanya kampeni chafu ya kusema Jk Hafai kuwa rahisi wa nchi hii kwa sababu ni mgonjwa, kazi ya jasusi kutoka rondo iliwamaliza mwakyembe na mwandosya

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 mbobezi alikuwa na kazi ya kuwashughulikia baadhi ya makada wakubwa katika chama wasirudi bungeni, jasusi wa rondo alifanya kwa muzihiri akafanikiwa na akafanya kwa Samweli Sita Japohakufanikiwa ila aliweza kuweka mazingira magumu..., utakumbuka mke wa Samweli sita Alikamatwa na Rushwa akigawa simu kwa wananchi hii ilikuwa ni kazi ya bm.....

Sita alihujumiwa na bm kwa kiasi kikubwa dhamira ya bm alijua ameshammaliza lowassa sasa Awamalize mwakyembe mwandosya na sita ili kufanikiwa 2015... Kutaka kuanzishwa kwa ccj kupitia nape aliyepewa kazi ya kumwingiza mkenge sitta ni dalili ya mpango kazi wa bm kumaliza sitta,kumbuka nape ni kijana mtiifu wa bm kila alichokuwa akikifanya ni mpango ulioratibiwa kibobezi na bm......

*Kinachofanywa na sitta sasa kwa mwakyembe ni kudhirisha yeye ni mnafiki katika siasa za msimamo

Tangu samweli aondolewe katika uspika nguvu yake kubwa ilipotezwa akakosa mahala pa kusimama imara ili kufanya siasa ngazi ya kitaifa jina lake likafifia......hata alipopelekwa wizara ya afrika mashariki alikwenda kusoma magazeti tuu maana hakukuna na kazi ya kumoa uhalali katika jamii

Kugeuka kwa Samweli sitta ni trick anayoitumia kupata umaarufu wa kisiasa kwa kumfanya mwakymbe ngazi au daraja lake kuvuka 2015...... Tangu kuingia wizara ya uchukuzi na usafirishaji wizara aliyokuwepo mwakyembe sitta amekuwa akimshughulikia vilivyo makwembe..... kwanza alianza kwa kufanya reshefle ya kuowaondoa watendaji mbalimbali waliowekwa na mwakyembe pili kuibua ufisadi uliofanyemwa na mwakyembe.....hapa kwa haraka haraka kuna picha inajengeka

Kwangu mimi john okello ni dalili ya uasi na urafiki wa mashaka ya kisaliti kwa hawa wanamtandao waliowahi kufanya kazi pamoja kwa nyakati tofauti ya kumharibia na kumpoteza lowassa

Ni mimi
Raia wa uganda niliyeshiriki mapinduzi ya zanzibar

John okello
 
Imebakia kuwa historia tu
Hata hivyo asante kwa kutukumbusha ya nyuma ambayo ni historia
 
Mwaka huu tutaona mengi ila LOWASA kajipanga sana lazima achukue nchi.nakumbuka sita baada ya kuachwa kando na kwenda kuanzisha ccj alipelekwa ikulu na mtutu wa bunduki akaambiwa atulie atapewa uwaziri kwi kwi kwi kwi kumbe anapelekwa east africa akasome magazeti
 
Ndani ya chama chetu hakuna hizi siasa maana mambo haya nilidhani yangezungumzwa ndani ya vikao vyetu
 
Tangu sitta asimamie hii katiba haramu ya chenge,nimemdharau.
 
  • Thanks
Reactions: rpg
Pata pesa/madaraka ili tuijue tabia yako. Huyo wa sasa ndie Sitta halisi. Aliyoyafanya kwenye mchakato wa katiba mpya kama spika hata siyasemei hapa. Ila kiukweli, mimi binafsi, cna hamu nae tena huyu mzee!!
 
Lakuambiwa... wao wafanye yoote ila kama m/ngu kasema MOTOCHINI wewe ndie wa MAGOGONI lazima iwe hivyo, hayamengine watajua wao
 
Hivi John Okello ndio yule tunayemsoma kwenye historia ya mapinduzi ya Zanzibar?
 
Last edited by a moderator:
MUNGU azidi kuyaweka yaliyofichika peupeeee uhakika Lowasa NI chaguo La Mungu kwa watanzania hivyo bac tunaona jinsi anavyompigania adui zake wanaokuja kwa Njia moja Mungu anawasambaratisha kwa Njia saba tofauti tofauti yani wapinzani wa lowasa kweli Mungu anawashuhulikia hasa.... Lowasa oyeeeeeeee
 
Haaa,,,lowassa ni kaa la moto huwezi kulizima bomu la nyukilia,,,,,watasoma namba tuu,,,lowassa juuu
 
Dr.Harrison Mwakyembe atakumbukwa na taifa kama msomi aliyeshindwa kusimamia alichojifunza pale aliposhindwa kueleza maoni yake BMK kuhusiana na Serikali ya Shirikisho ambayo aliandika kitabu kuhusu na kuweza kutunikiwa udaktari. Watu wamekuwa wanafiki wa nafsi zao wenyewe, nafsi yake inajua na elimu aliyopata na kuamini inamwambia vile lakini amekubali kuenenda kama walivyoagizwa na Lukuvi, Wassira.

Samweli Sitta mnafiki na ndumila kuwili asiye na haya wala kujiuliza msimamo wake wa maisha na kisiasa. Ni kweli katika siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu lakini Sitta amekubuhu katika kuwatumia watu.
Awali aliwatumia wabunge wa upinzani na makada wa ccm wasiompenda JK akiwa spika, baadae alivyobanwa na kuhofia kuuawa sambamba na Dr.Mwakyembe.

Alipita makanisani ili aonewe huruma lakini katika BMK aliwadhalilisha maaskofu. Kimsingi watanzania tulikuwa na imani kubwa na Samwel Sitta tukiamini MZALENDO kumbe yupo kwa maslahi yake. SItta ni aina ya mtu anayeweza kupambana mkaamini mwezenu na kesho akipata fursa anatetea na kuimarisha upande aliopinga awali.

NI USHETANI
 
Hao sita na kyembe ni ndumilakuwili. Lowassa kwanza CCM Baadae. Hila zote kufichuka. EL akihamia popote tuko nae. EL juu
 
Ulivyoanza nimeona kama unajaribu kutueleza kuwa ujasiri wa sita haujaanza leo. Kuipinga serikali wakati wa mwalimuilitahitaji mtu uwe jasiri. Hongera zake.
 
Hao sita na kyembe ni ndumilakuwili. Lowassa kwanza CCM Baadae. Hila zote kufichuka. EL akihamia popote tuko nae. EL juu

Inataka moyo kujitoa akili kama hivi na kumuunga mkono mtu ambaye kathibitika kuwa sio presidential material
 
Kama Samwel Sitta akimkasirisha Mwalimu Nyerere kwanini alikuja kumteua kuwa waziri 1977?
 
Back
Top Bottom