Unafiki wa mama ntilie

Vesper-valens

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
5,287
7,388
Habari wakuu,

Leo nimeona nijaribu ku share baadhi ya tabia za mama ntilie ambazo wakiwa wenyewe huzifanya ila akiwepo mteja hawafanyi,

Wakati wa asubuhi akiwa anakaanga vitavuno, (Maandazi, vitumbua, half cake na chapati) wakati anaviweka kwenye zile meza zao za Aluminium tayari kwa ajili kuuza, huwa wanaweka kwa mikono, ila akija mteja kumuuzia anatumia kijiko au kuvaa nylon mkononi wakati anampatia mteja

Kwenye kuosha vyombo hususani vijiko, wakati anaosha kama humuangalii atatumbukiza kwenye maji na kukuletea ,ila ukiwa unamwangalia anatumia sabuni anasafisha vizuri

Wenye kujua tabia zingine ambazo huwa wanazifanya wakiwa peke yao au mazingira ambayo mteja haoni waziweke hapa.

Note:
Uzi huu hauna lengo la kuwakashifu na kuwasema vibaya hawa wajasiriamali, ila ni katika kukumbushana na kuzingatia afya za walaji

Asanteni
 
Kuna mama ntilie wasafi na wachafu pia, ila zaidi wasaidizi wao wa kazi huwa ndo wanakua wachafu mara nyingi, hata mhusika akiwa anajali usafi;

Hygiene kibongo bongo ipo five star tu, sehemu nyingi za kula hata zilizo expensive juu ya hao mama ntilie usafi ni tia maji tia maji.

Hii ni kwa sababu Hygiene ni tabia ya mtu na ni mara chache kukuta wafanyakazi wote wa mgahawa fulani wana hiyo tabia.

Usipokula uchafu kwenye mboga utakula kwenye ugali, ukikosa kwa ugali utaupata kwenye vyombo, ukikosa huko utakutananao kwenye juice.
 
Back
Top Bottom