Unafiki huu umeimarika kuliko ule wa miaka mingine

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Yaaani Serikali imeendelea kutegemea walevi wa Pombe na Sigara .Watu aina ya Kitwanga wameendelea kuwa muhimu sana kwa serikali vinginevyo Utekelezaji wa Bajeti utakwama.Tunahitaji Maombi.Serikali inapaswa kuweka kodi kwa lengo la ku-discourage matumizi ya Bad Goods kama ilivyo kwenye nadharia za Uchumi .Lakini sio kwa lengo la kufanya kuwa chanzo kikuu cha Mapato.Siku walevi wote wakiokoka Serikali inayumba au kuanguka kabisa kabisa.Kila Mlevi anayeokoka Serikali inakwama ,Inayumba mahali fulani.

Hatujapanua wigo wa Kodi.Kenya wamepanua wigo na kuingia hadi Sekta isiyo Rasmi.

Nimeona Uamuzi mwingine wa ajabu kabisa katika Uchumi. Unapandisha Kodi kwa wanaoutumia namba binafsi za magari kutoka Milioni 5 hadi 10 .Haya ni maamuzi ya kimchecheto. Ni bora ingebaki hizo hizo Milioni 5 maana unaweza kupata watu 100 kuliko kupata watu 10 wanaolipa milioni 10.Hii ni nadharia Rahisi sana niliyoisoma Mwaka wa Kwanza kwenye Micro-economics.

Vilevile Katika Elimu Serikali imetenga asilimia 22 ya Bajeti.Hii ni sahihi maana hata katika Uchambuzi wetu hapo kabla tulitaka bajeti ya elimu ifikie huko ila tatizo bado wameweka mikopo ya elimu ya Juu kwenye Bajeti ya maendeleo ya Elimu badala ya Recurrent expenditure.Hayo ni maamuzi ya kukwepa wajibu wa serikali katika uwiano wa Bajeti ya elimu katika vigezo viwili Matumizi na Maendeleo

Vilevile ninachoona katika bajeti hii ni hadithi zilezile za miaka 15 iliyopita

Mwaka 2000 wakati wa kuanzisha mpango wa Maendeleo ya Millenia(MDG) wachumi nchini na Wa kimataifa walioa tathmini kuwa ikiwa uchumi utakua kwa asilimia 7 kwa nchi maskini kama Tanzania kwa muda wa miaka 15 basi Umaskini utapungua kwa kiwango sio chini ya asilimia 50

Tanzania tumetangaziwa uchumi umekuwa kwa asilimia 7 mfululizo so hadi mwaka jana (Miaka 15 baada ya tathmini) umaskini wetu ulipaswa kupungua kwa zaidi ya asilimia 50.

Umaskini wetu haukupungua hata kufikia zaidi ya asilimia 10

Tunafanya hadaa kwa takwimu

Leo Serikali imetenga Trilioni Kadhaa kununua Ndege,Kufufua Reli na Pia kununua Meli.Vilevie mashine na mitambo mingi itanunuliwa nje ya nchi ukipiga hesabu ni kuwa matumizi ya serikali kwa mwaka huu hayatasisimua uchumi wa ndani (Economic Stimulation) bali uchumi wa nje.Serikali haijazingatia Uzalishaji wa ndani na ni jinsi gani pia bei za bidhaa na huduma zitaathirika hivyo kusababisha Stagflation. Maswala haya yanapaswa kufanywa kwa awamu ili isilete madhara kwa sekta nyingine.

Halafu kuna hizi Mbwembwe za kutenga Bilioni 2.6 kuanzisha mahakama ya ufisadi .Ripoti ya Warioba kuhusu Rushwa haikuonyesha kuwa na upungufu wa Mahakama.TAKUKURU yenyewe inashindwa kufanya kazi kutokana na sheria mbovu inayozuia TAKUKURU kupeleka kesi mahakamani hadi wapite Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP). Wala hakukua na haja ya kutumia Raslimali vibaya .Ifamye TAKUKURU kuwa na meno Kisheria na Kikatiba basi.

Mtazamo wa Haraka haraka kwenye bajeti ya jumla naona mambo yale yale ya hadaa kama miaka iliyopita na hii ya safari hii ndio inaumbua watu kabisa na watu wamefikia ukomo wa ubunifu.. Bajeti yote ni trilioni 29. Serikali inategemea kukusanya mapato ya ndani yatokanayo na kodi kama trilioni 19. Trillioni 8 zimetengwa kwa ajili ya kilipa deni la Taifa.

Halafu mishahara kwa mwezi mmoja serikali inatumia kama Sh. 500 bilioni kuendana na taarifa ya Benki Kuu ya mwezi Machi.

Kwa hiyo bil 500 X miezi 12 inakuwa kama trilioni 6.

Tuseme Trilioni 6.3 kwa sababu kutakuwa na ajira mpya n.k.

Kwa hiyo deni na mishahara itakua kama 15 Trilioni. Ukiweka matumizi mengineyo ndani ya serikali kama Trilioni 2.

Jumla matumizi ya kawaida ni kama Trilioni 17 hivi. Hii ina maana kwamba sehemu kubwa ya makusanyo ya kodi yataishia kwenye matumizi ya kawaida na kuhudumia deni la taifa. Mapato ya nje yatakuwa Trilioni 3. Mikopo ya kibiashara toka vyanzo vya ndani trilioni 7. Hizi ndio zinategemewa kuingia kwenye maendeleo!

Pesa ya wahisani na mikopo.

Pia Waziri anapotangaza kwenye hotuba pia viinua mgongo vya wabunge vitakatwa kodi ilipaswa kuwa Tangazo nje ya Hotuba tu maana ni suala la miaka ijayo watakapostaafu.Hakukua na ulazima wa kuliingiza katika matamshi ya bajeti kama vile ni immediate Source of revenue.

Unafiki huu umeimarika kuliko ule wa miaka mingine

Nitajadili Kadiri nitakavyoisoma kwa Undani na kufanya Rejea

Tukatae Unafiki.Hii ni Bajeti inayozidi kuwaumiza wananchi

Unawapunguzia Kodi ya 3,800 au 1,100 wafanyakazi halafu unawapandishia kodi ya bidhaa na hata huduma za Simu wanapotumia wazazi au ndugu zao vijijini fedha au Ada

Aluta Continua,Victory Ascerta.....

Ben Saanane
 
Subirini utawala wa Mzee wa Mamvi ndo mje mshauri hayo. CCM haina dhiki ya washauri mpaka akina Ben Saanane ndo wajifanye washauri
 
Aisee kutumika kubaya sana. Ona jinsi ulivyo mtumwa maana kila saa lazima uanzishe mada hata kama hazina mashiko

Tatizo ninaloliona tanzania nikulalamika na kupinga bila kuonyesha mdala wa na anlysis yake. Yaani sisi tumejikita kukaa na kusubili idea za watu ili tuzikatae.

Ben ni mwanachama mwenzangu chadema lakini niseme ilitakiwa unapopinga basi onyesha alternative ambayo ni practicable ambalo wote kama taifa hatufanyi.

Tanzania ni mabingwa kwa kubisha bila kutoa practical alternative solution
 
Aisee kutumika kubaya sana. Ona jinsi ulivyo mtumwa maana kila saa lazima uanzishe mada hata kama hazina mashiko
Mkuu lizaboni nakuheshimu sana, mimi pia sio shabiki wa vijana wa upinzani aina ya kina saanane lakini wanaposema ukweli lazima tuukubali kwa maendeleo ya taifa.Nchi ni yetu sote, tunaoumia ni sisi wote hasa ndugu zako walio kule kwenu kijijini wanaokosa huduma muhimu.
 
huyu jamaa sijui yuko sawa kweli, hata mimi sishabikii upande wa pili ila wakiwa na mambo ya msingi kwa taifa tutapiga makofi sana. nchi inataka maendeleo lizaboni anapenda ushabiki, kama kuna makosa hata kama ni baba yako yaseme tu
 
Yaaani Serikali imeendelea kutegemea walevi wa Pombe na Sigara .Watu aina ya Kitwanga wameendelea kuwa muhimu sana kwa serikali vinginevyo Utekelezaji wa Bajeti utakwama.

Kumbuka:

Marufuku uuzwaji wa vileo kabla ya saa kumi jioni.
Marufuku uuzwaji viroba.
Marufuku uuzwaji vileo kuanzia saa sita usiku.
 
Mkuu lizaboni nakuheshimu sana, mimi pia sio shabiki wa vijana wa upinzani aina ya kina saanane lakini wanaposema ukweli lazima tuukubali kwa maendeleo ya taifa.Nchi ni yetu sote, tunaoumia ni sisi wote hasa ndugu zako walio kule kwenu kijijini wanaokosa huduma muhimu.
Mkuu, ukiona mpinzani anakupogia kelele juu ya jambo fulani basi usiache kulitekeleza
 
Nimeona Uamuzi mwingine wa ajabu kabisa katika Uchumi. Unapandisha Kodi kwa wanaoutumia namba binafsi za magari kutoka Milioni 5 hadi 10 .Haya ni maamuzi ya kimchecheto. Ni bora ingebaki hizo hizo Milioni 5 maana unaweza kupata watu 100 kuliko kupata watu 10 wanaolipa milioni 10.Hii ni nadharia Rahisi sana niliyoisoma Mwaka wa Kwanza kwenye Micro-economics.
Hii kitu Tanzania inaonekana kama ni ya wenye nazo .......... ukienda Bondeni South au Namibia kila mtu anaweza kuweka ..... especially wale wanaopenda kujionyesha. Gharama zake ni kama laki 4 tu za Tanzania kwa mwaka!! Ukiweka very low kuna makampuni yanaweza kutumia hizo personalized number plates kwa wingi ili magari yao yatambulike kirahisi na vile vile yajitangaze kibiashara!! Mfano Bakhresa anaweza kuwa na Number plate za AZAM kwenye magari yake, ITV pia n.k.!! Mtu mwenye magari Matatu nyumbani anaweza kuweka DIAMOND1, DIAMOND 2 na DIAMOND 3. Kwa million 10 sidhani hata Tajiri au anayependa kujitangaza anaweza kutupa 30 million kwenye number plates kwa mwaka!!

Leo Serikali imetenga Trilioni Kadhaa kununua Ndege,Kufufua Reli na Pia kununua Meli.Vilevie mashine na mitambo mingi itanunuliwa nje ya nchi ukipiga hesabu ni kuwa matumizi ya serikali kwa mwaka huu hayatasisimua uchumi wa ndani (Economic Stimulation) bali uchumi wa nje.Serikali haijazingatia Uzalishaji wa ndani na ni jinsi gani pia bei za bidhaa na huduma zitaathirika hivyo kusababisha Stagflation. Maswala haya yanapaswa kufanywa kwa awamu ili isilete madhara kwa sekta nyingine.

Badala ya kununua ndege bora hizo pesa angezipeleka kufufua viwanda. Wangeanza na viwanda kama vya Korosho ambavyo havihitaji pesa nyingi. Pia pesa ingetumika kutoa subsidy kwa wakulima wa kati na wakubwa au kupunguza bei za pembejeo za kilimo kama vile mbolea na madawa. Wakulima wadogo wadogo wangefaidika kwa kushushiwa kodi ya mbolea na madawa!!

Kwa kweli hii bajeti haimsaidii sana maskini hasa Mkulima huko kijijini ........ Kuinua maisha ya Mwanakijiji, nilitegemea angelenga pia kwenye kupunguza kodi ya uzalishaji vifaa vya ujenzi. Kama kodi vifaa vya ujenzi haitashuka basi Watanzania wataendlea kuishi kwenye nyumba za majini na Matope kwa miaka!! Sijui hata huo umeme wanaoupeleka huko vijijini utafungwa kwenye nyumba za aina hii!!??

Inawezekana ikawa ni bajeti nzuri tatizo wame underline au emphasize kwenye vitu ambavyo siyo vya msingi sana ......... Binafsi sijaiona zaidi ya kupata vipande vipande humu jukwaani.
 
Mkuu, ukiona mpinzani anakupogia kelele juu ya jambo fulani basi usiache kulitekeleza
Kweli upinzani imewashika pabaya ccm mpaka wameon mikutani isifanyike wakati katiba inaruhusu na ndio kazi ya siasa kweli mekosa mwelekeo
 
Back
Top Bottom