Unafiki huu umeimarika kuliko ule wa miaka mingine

Unafiki huu umeimarika kuliko ule wa miaka mingine

Mbona unajitukana mwenyewe Jeska alifikaje Udom? Ndio akilizenu nyie
Mwenza wako anatabu kweli. Tukikwambia sisi kuwa wewe kichwani panamkojo wa Mbowe tu hutuamini. Sasa muoneshe mwenza wako kile nilichoandika na jibu lako. Akikihurumia atakupeleka kwenye matibabu ya akili.
 
Aisee kutumika kubaya sana. Ona jinsi ulivyo mtumwa maana kila saa lazima uanzishe mada hata kama hazina mashiko
Mada yake ina mashiko inaonyesha uelewa wako ni mdogo. Sio lazima uchangie hata kama mada zimekuzidi uwezo.
 
Mwenza wako anatabu kweli. Tukikwambia sisi kuwa wewe kichwani panamkojo wa Mbowe tu hutuamini. Sasa muoneshe mwenza wako kile nilichoandika na jibu lako. Akikihurumia atakupeleka kwenye matibabu ya akili.
Naona akili zako zimeshaamia kiunoni ndio maana unaparamia paramia kama gari la mwendo kasi likianza kugonga vibao barabarani
 
Huduma muhimu kama zipi? Mpango ni zahanati kila kijiji kituo cha afya kila kata. Elimu msingi ni bure. Milioni hamsini za kukopeshana hukohuko kijijini. Umeme wa rea 3 kila kijiji huduma ipi. Kijijini wanakumbukwa ngoja utekelezaji uanze kwenye hii bajeti ya kwanza
Sawa mkuu, muda utaamua
 
Mkuu, umenigusa hasa hapo pa "acheni watu wanywe viroba vyao kwakuwa watu hawana pa kupumzikia".
Makampuni ya bia yenyewe yalishalalamika kwamba tangu amri ya kuuza pombe saa kumi itolewe mauzo na mapato ya kampuni yameshuka sana. Sasa sijui hixo kodi wanaxitegemea kwenye vileo wataxipataje?
 
Makampuni ya bia yenyewe yalishalalamika kwamba tsngu amri ya kuanza kuuza pombe saa kumi imeshusha mauzo na mapato ya kampuni. Sasa sijui hixo kodi wanaxitegemea kwenye vileo wataxipataje?

Maamuzi yenye mihemko ya kisiasa mara nyingi yanaathari sana.

Huyo muuzaji wa hizo bia ana leseni ya biashara ambayo anailipia kwa mwaka.

Vile vile pango la nyumba au chumba cha biashara anatakiwa kulipia.

Inasikitisha inapoonekana biashara yake anayoifanya kihalali anapangiwa masharti wakati bajeti ya mwaka inaitegemea biashara hiyo hiyo.
 
Na madai kwamba bajeti ya maendeleo imeongezeka mpaka asilimia 40 ya budget yote halina uhalisia. Hii ni kwa ssbabu ukitoa hiyo 8 trilioni inayokwends kwenye deni la taifa, hiyo asilimia ya budget ya maendeleo itapungua!



Yaaani Serikali imeendelea kutegemea walevi wa Pombe na Sigara .Watu aina ya Kitwanga wameendelea kuwa muhimu sana kwa serikali vinginevyo Utekelezaji wa Bajeti utakwama.Tunahitaji Maombi.Serikali inapaswa kuweka kodi kwa lengo la ku-discourage matumizi ya Bad Goods kama ilivyo kwenye nadharia za Uchumi .Lakini sio kwa lengo la kufanya kuwa chanzo kikuu cha Mapato.Siku walevi wote wakiokoka Serikali inayumba au kuanguka kabisa kabisa.Kila Mlevi anayeokoka Serikali inakwama ,Inayumba mahali fulani.

Hatujapanua wigo wa Kodi.Kenya wamepanua wigo na kuingia hadi Sekta isiyo Rasmi.

Nimeona Uamuzi mwingine wa ajabu kabisa katika Uchumi. Unapandisha Kodi kwa wanaoutumia namba binafsi za magari kutoka Milioni 5 hadi 10 .Haya ni maamuzi ya kimchecheto. Ni bora ingebaki hizo hizo Milioni 5 maana unaweza kupata watu 100 kuliko kupata watu 10 wanaolipa milioni 10.Hii ni nadharia Rahisi sana niliyoisoma Mwaka wa Kwanza kwenye Micro-economics.

Vilevile Katika Elimu Serikali imetenga asilimia 22 ya Bajeti.Hii ni sahihi maana hata katika Uchambuzi wetu hapo kabla tulitaka bajeti ya elimu ifikie huko ila tatizo bado wameweka mikopo ya elimu ya Juu kwenye Bajeti ya maendeleo ya Elimu badala ya Recurrent expenditure.Hayo ni maamuzi ya kukwepa wajibu wa serikali katika uwiano wa Bajeti ya elimu katika vigezo viwili Matumizi na Maendeleo

Vilevile ninachoona katika bajeti hii ni hadithi zilezile za miaka 15 iliyopita

Mwaka 2000 wakati wa kuanzisha mpango wa Maendeleo ya Millenia(MDG) wachumi nchini na Wa kimataifa walioa tathmini kuwa ikiwa uchumi utakua kwa asilimia 7 kwa nchi maskini kama Tanzania kwa muda wa miaka 15 basi Umaskini utapungua kwa kiwango sio chini ya asilimia 50

Tanzania tumetangaziwa uchumi umekuwa kwa asilimia 7 mfululizo so hadi mwaka jana (Miaka 15 baada ya tathmini) umaskini wetu ulipaswa kupungua kwa zaidi ya asilimia 50.

Umaskini wetu haukupungua hata kufikia zaidi ya asilimia 10

Tunafanya hadaa kwa takwimu

Leo Serikali imetenga Trilioni Kadhaa kununua Ndege,Kufufua Reli na Pia kununua Meli.Vilevie mashine na mitambo mingi itanunuliwa nje ya nchi ukipiga hesabu ni kuwa matumizi ya serikali kwa mwaka huu hayatasisimua uchumi wa ndani (Economic Stimulation) bali uchumi wa nje.Serikali haijazingatia Uzalishaji wa ndani na ni jinsi gani pia bei za bidhaa na huduma zitaathirika hivyo kusababisha Stagflation. Maswala haya yanapaswa kufanywa kwa awamu ili isilete madhara kwa sekta nyingine.

Halafu kuna hizi Mbwembwe za kutenga Bilioni 2.6 kuanzisha mahakama ya ufisadi .Ripoti ya Warioba kuhusu Rushwa haikuonyesha kuwa na upungufu wa Mahakama.TAKUKURU yenyewe inashindwa kufanya kazi kutokana na sheria mbovu inayozuia TAKUKURU kupeleka kesi mahakamani hadi wapite Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP). Wala hakukua na haja ya kutumia Raslimali vibaya .Ifamye TAKUKURU kuwa na meno Kisheria na Kikatiba basi.

Mtazamo wa Haraka haraka kwenye bajeti ya jumla naona mambo yale yale ya hadaa kama miaka iliyopita na hii ya safari hii ndio inaumbua watu kabisa na watu wamefikia ukomo wa ubunifu.. Bajeti yote ni trilioni 29. Serikali inategemea kukusanya mapato ya ndani yatokanayo na kodi kama trilioni 19. Trillioni 8 zimetengwa kwa ajili ya kilipa deni la Taifa.

Halafu mishahara kwa mwezi mmoja serikali inatumia kama Sh. 500 bilioni kuendana na taarifa ya Benki Kuu ya mwezi Machi.

Kwa hiyo bil 500 X miezi 12 inakuwa kama trilioni 6.

Tuseme Trilioni 6.3 kwa sababu kutakuwa na ajira mpya n.k.

Kwa hiyo deni na mishahara itakua kama 15 Trilioni. Ukiweka matumizi mengineyo ndani ya serikali kama Trilioni 2.

Jumla matumizi ya kawaida ni kama Trilioni 17 hivi. Hii ina maana kwamba sehemu kubwa ya makusanyo ya kodi yataishia kwenye matumizi ya kawaida na kuhudumia deni la taifa. Mapato ya nje yatakuwa Trilioni 3. Mikopo ya kibiashara toka vyanzo vya ndani trilioni 7. Hizi ndio zinategemewa kuingia kwenye maendeleo!

Pesa ya wahisani na mikopo.

Pia Waziri anapotangaza kwenye hotuba pia viinua mgongo vya wabunge vitakatwa kodi ilipaswa kuwa Tangazo nje ya Hotuba tu maana ni suala la miaka ijayo watakapostaafu.Hakukua na ulazima wa kuliingiza katika matamshi ya bajeti kama vile ni immediate Source of revenue.

Unafiki huu umeimarika kuliko ule wa miaka mingine

Nitajadili Kadiri nitakavyoisoma kwa Undani na kufanya Rejea

Tukatae Unafiki.Hii ni Bajeti inayozidi kuwaumiza wananchi

Unawapunguzia Kodi ya 3,800 au 1,100 wafanyakazi halafu unawapandishia kodi ya bidhaa na hata huduma za Simu wanapotumia wazazi au ndugu zao vijijini fedha au Ada

Aluta Continua,Victory Ascerta.....

Ben Saanane
 
Mkuu lizaboni nakuheshimu sana, mimi pia sio shabiki wa vijana wa upinzani aina ya kina saanane lakini wanaposema ukweli lazima tuukubali kwa maendeleo ya taifa.Nchi ni yetu sote, tunaoumia ni sisi wote hasa ndugu zako walio kule kwenu kijijini wanaokosa huduma muhimu.

Mkuu tuendelea tu kuwaambia hawa ndugu zetu, kiukweli hawa wenzetu utafikiri sio watanzania maana wao ni kutetea chochote kile nahisi wanalipwa kwa kazi hii.
Hili la bajeti liko wazi halihitaji degree, serikali inakosa ubunifu kila siku na kuendelea kutegemea wanywa bia na wavuta sigara huku resources zetu zikiendelea kukamuliwa kila kukicha.
 
Back
Top Bottom