Unaendaje nyumbani kwa mtu bila taarifa?

Unaendaje nyumbani kwa mtu bila taarifa?

Mrs Dee

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2017
Posts
209
Reaction score
324
Waswahili wenzangu hii tabia ya kwenda kwa mtu usiku bila taarifa yeyote halafu unategemea ule na mambo kama hayo, hivi unategemea watu wajiandaeje sasa?

Hivi kwa nini mnaendekeza hii tabia inayokera kupita maelezo? Kumbuka kupika chakula cha mtu mmoja ni gharama kifedha na pia inagharimu muda jamani.

Kwa mfano ugali na wali kuupika inachukua karibia dakika 40 hadi lisaa. Sisi wamama ukija kwetu hata bila taarifa inabidi upikiwe.

Kwanini unamshtukiza mtu bila taarifa jamani?
 
Kwan shida iko wap msosi wako Bado ulie lie mnyime tu (if you can't join them beat them)
 
Kama mtu hajafundishwa toka nyumbani basi hata maadili ya dini hajui?
Mambo mengi tunajifunza tukiwa bado wadogo na tunakuwa nayo
Mimi sio mhubiri ila najua kuwa nyumbani kwa mtu ni private na mtu lazima awe na heshima
Nitakuja kwako kwa dharura au kukutembelea lakini kwa taarifa pia na siwezi kuja kwako mchana wala usiku na huo ndio utaratibu
Nenda kwa mtu ukiwa umeshiba au jizuie kuwakalifu wenzio kwani hujui nao wana hali gani



Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Vyuma vyuma Mkuu VIMEKAZA halafu wengine hutia mguu karibu na lunchtime kwanini wasitoe taarifa mapema kuhusu ugeni wao ili portion ikaongezwa? Au nakosea?

Siamini kama watanzania tumefikia huku........dah
 
mi kwa imani yangu kuna watu walipokea watu nyumbani kwao wakawafanyia ukarimu kwa kuwachinjia kondoo alienona kumbe wale watu ni malaika wakamwambia mambo mazuri yakaja timia....kuna watu walitoa kibaba cha mafuta ya mwisho yaliyobakia kwa wageni mafuta yakazidishwa....acheni uchoyo mnaelekea kubaya.mwanamke ukalalamike kupika ugali mara mbili kweli haipendezi kabisa....mie napika kwa furaha zote..sharp

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom