Unaendaje nyumbani kwa mtu bila taarifa?

Unaendaje nyumbani kwa mtu bila taarifa?

waswahili wenzangu hii tabia ya kwenda kwa mtu usiku bila taarifa yeyote alafu unayegemea ule,na mambo kama hayo hivi unategemea watu wajiandaeje sasa.
hivi kwa nini mnaendekeza hii tabia inayokera kupita maelezo.
kumbuka kupika chakula cha mtu mmoja ni gharama na pia inagharimu muda jamani.
kwa mfano ugali na wali kuupika inachukua karibia dakika 40 hadi lisaa
sisi wamama ukija kwetu hata bila taarifa inabidi upikiwe.
unamshtukiza mtu bila taarifa jamani
Yaani wewe Kama ni mke wangu nakuacha Mara moja
 
Kama mtu hajafundishwa toka nyumbani basi hata maadili ya dini hajui?
Mambo mengi tunajifunza tukiwa bado wadogo na tunakuwa nayo
Mimi sio mhubiri ila najua kuwa nyumbani kwa mtu ni private na mtu lazima awe na heshima
Nitakuja kwako kwq dharura au kukutembelea lakini kwa taarifa pia na siwezi kuja kwako mchana wala usiku na huo ndio utaratibu
Nenda kwa mtu ukiwa umeshiba au jizuie kuwakalifu wenzio kwani hujui nao wana hali gani

Sent from my SM-G570F using Tapatalk

Mkuu Ni maisha yako siyaingilii but Kuna kitu lazma ukitazame upya.
Mwaka 2015, nilikuwa meajiriwa wa KIA Kama mhandisi wa mifumo ya computer sikuwa nimeoa na nilikuwa nakaa na mpenzi wangu wa mda mrefu. Tulipanga nyumba nzima iliyokuwa na partition 2 hivyo partition nyingine alikuwa anaishi jamaa wa TRA .
Mimi kwetu ndo wa kwanza kuzaliwa na katika kunisomesha kwangu mpka Wazazi waliuza Rasilimali nyingi kwa sababu hawakuwa na uwezo mkubwa, nilivyomaliza chuo na kupata kazi ilikuwa ahueni kwa Wazazi ili niweze kuwasaidia wadogo zangu waliobaki. Sasa kwa sababu uwezo ulikuwepo niliwatafitia shule za bweni, na kwangu ndgu walikuwa hawakauki kuja karibia kila wiki na hata madogo wakiwa likizo nilikuwa nawatumia nauli waje..

Siku moja huyu jamaa yangu wa TRA kaniita ananiambia Kaka nataka nikupe ushauri " ukiataka kuishi vizuri na mkeo mpe uhuru, usiruhusu ndugu kuja Mara kwa Mara wanamnyima Uhuru, Hao ndgu waambie ushakuwa na maisha yako kwa hiyo Kama Kuna Jambo la kifamilia nendeni mkamalize Ila sio kufuatana fuatana kwako, mkeo hajisikii vizuri. Akaendelea " wewe SI unaona kwangu Niko mm tu na mke na maisha yetu Ni Raha kweli mm sitaki ndgu kwangu na nilishawaambia maana wananichonganisha na mke wangu, awe mama, baba, au wadogo Kama Kuna tatzo tupigiane simu tu".

Huyu jamaa nikamuitikia tu, kwa s'babu pale hata ndgu wa kike walikuwa wanakuja. Sasa huyu mpenzi wangu akaanza kubadilika na kufanya visa kwa ndgu nilipothibisha kwa asilimia 100, niliachana nae akarudi kwao.

Na sitarajii kuoa mpaka nione wadogo zangu wamesimama bila utegemezi na hata nikioa sharti kudumu kwenye lazma mwanamke apende familia yangu.

Hizi tabia sio za kisfrika huu Ni uchoyo, nowdays Kuna majiko ya gesi hata dk5 haiishi chakula kimeiva, unashindwaje kumuandalia ndgu, jamaa au rafiki?
 
Aisee kuja nikuoe walai vile
mi kwa imani yangu kuna watu walipokea watu nyumbani kwao wakawafanyia ukarimu kwa kuwachinjia kondoo alienona kumbe wale watu ni malaika wakamwambia mambo mazuri yakaja timia....kuna watu walitoa kibaba cha mafuta ya mwisho yaliyobakia kwa wageni mafuta yakazidishwa....acheni uchoyo mnaelekea kubaya.mwanamke ukalalamike kupika ugali mara mbili kweli haipendezi kabisa....mie napika kwa furaha zote..sharp

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana akikuta unataka kutoka mkabidhi jiko ajisevie
Mie kwangu mtu aje tu, aje na taarifa asije na taarifa sawa tu, kwanza hizi taarifa ni kero wakat mwingine itabidi ujipange wee kama unataka kupika solo la harusini, akija bila taarifa ndio mpango kipo kinapikwa, hakipo atakunywa soda hata maji ya bomba pia, muhimu nafsi yako inatoaje, katika uislamu kuna hadithi inasema ina ammali bin niyatin, kila amali italipwa kwa nia, kuna mwingine anampikia mgeni wake vizur akiondoka huku nyuma anaanza kumsimanga kapika tu ili mradi, kuna mwingine anapika vizuri kwa sababu anajua tumeamrisjwa kuwakarimu vizur wagen wetu, kumkarimu vizuri ni kuna thawabu na mtu mwenda kumtembelea mtu kwake kuna thawabu zote ni ibada katika uislamu! So tufanye vitu kutoka moyoni kiroho safi sio kufanya kwa kuigiza, kaja kanikuta kuna sehemu nawahi namueleza ukweli kuwa hii ni saa 5 kamili, 5 na dk 20 nahitajika sehemu, kwanini tunafosi kuigiza maisha wajameni.. Kaja kuna samaki ndani na mie ninataka kusongewa ugali tutakula ugali, kakuta nagongewa mayai basi sawa tutatafuna, hakuna kitu kabisa hata glass ya maji sawa pia..

Sent using my nokia ya tochi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwangu nina utaratibu ambao ni lazma ufuatwe, ametokea mpita njia au mtoto akalalamika njaa, na chakula kipo hata kama niliwekewa mimi apewe ale, ila ikitokea mgeni amekuja kwangu bila ya taarifa rasmi kwamba siku flani nitakuja huyo aishie nje
 
Umenikumbusha jamaa mmoja,alizamia ulaya muda mrefu sana ila amerudi bongo kama miaka 8 iliyopita,akijaga home kusalimia wazee anakujaga na bia zake za kopo kama 4 hivi wkt mnapiga story ye anakunywa bia zake taratiiibu akimaliza hapo anaenda kwny gari yake anachukua mfuko anaweka makopo ya bia alizotumia then nduki anasepa na makopo yake,hahah.

Hio tabia washampiga marufuku kuifanya hapo home lkn ishashindikana ndio maisha waliyochagua hayo.

Lifestyle yake naikubali sana.
 
Mkuu Ni maisha yako siyaingilii but Kuna kitu lazma ukitazame upya.
Mwaka 2015, nilikuwa meajiriwa wa KIA Kama mhandisi wa mifumo ya computer sikuwa nimeoa na nilikuwa nakaa na mpenzi wangu wa mda mrefu. Tulipanga nyumba nzima iliyokuwa na partition 2 hivyo partition nyingine alikuwa anaishi jamaa wa TRA .
Mimi kwetu ndo wa kwanza kuzaliwa na katika kunisomesha kwangu mpka Wazazi waliuza Rasilimali nyingi kwa sababu hawakuwa na uwezo mkubwa, nilivyomaliza chuo na kupata kazi ilikuwa ahueni kwa Wazazi ili niweze kuwasaidia wadogo zangu waliobaki. Sasa kwa sababu uwezo ulikuwepo niliwatafitia shule za bweni, na kwangu ndgu walikuwa hawakauki kuja karibia kila wiki na hata madogo wakiwa likizo nilikuwa nawatumia nauli waje..

Siku moja huyu jamaa yangu wa TRA kaniita ananiambia Kaka nataka nikupe ushauri " ukiataka kuishi vizuri na mkeo mpe uhuru, usiruhusu ndugu kuja Mara kwa Mara wanamnyima Uhuru, Hao ndgu waambie ushakuwa na maisha yako kwa hiyo Kama Kuna Jambo la kifamilia nendeni mkamalize Ila sio kufuatana fuatana kwako, mkeo hajisikii vizuri. Akaendelea " wewe SI unaona kwangu Niko mm tu na mke na maisha yetu Ni Raha kweli mm sitaki ndgu kwangu na nilishawaambia maana wananichonganisha na mke wangu, awe mama, baba, au wadogo Kama Kuna tatzo tupigiane simu tu".

Huyu jamaa nikamuitikia tu, kwa s'babu pale hata ndgu wa kike walikuwa wanakuja. Sasa huyu mpenzi wangu akaanza kubadilika na kufanya visa kwa ndgu nilipothibisha kwa asilimia 100, niliachana nae akarudi kwao.

Na sitarajii kuoa mpaka nione wadogo zangu wamesimama bila utegemezi na hata nikioa sharti kudumu kwenye lazma mwanamke apende familia yangu.

Hizi tabia sio za kisfrika huu Ni uchoyo, nowdays Kuna majiko ya gesi hata dk5 haiishi chakula kimeiva, unashindwaje kumuandalia ndgu, jamaa au rafiki?
Nakubaliana na wewe ingawa umeelekea kushoto sana
Ndugu ni tofauti kabisa na washikaji au marafiki
Hao ndugu na wageni ni mila zetu na utaratibu wetu kwani kuna likizo na kuna watu wanapita hata transit wqnasalimia siku mbili na kupita.
Hilo ni jambo jema kulifanya kwani hata mimi wanangu huenda likizo kwetu
Lakini mimi nilikuwa nalenga zaidi hao wa hapo hapo mji mmoja wanaokuja kukubughudhi na sio lingine
Salaam za usiku? Unakuja kufanya nini na jua limeishazama au mchana huenda watu wanapumzika kidogo.
Ila pole kwa yaliyokupata

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Wageni ni baraka. Wageni ni sadaka. Look, mtu hadi kaja kwako anaamini kuwa wewe ndo unaweza msaidia chakula, labda Mungu kamwelekeza aje hapo. Ukimhudumia ni baraka unapata, kingine hata siku moja, narudia hata siku moja usije mnyima mtu chakula au maji ilhali una uwezo navyo.
Maana mi nikipataga njaa naugua kabisaaa, sa namfikiria mtu ambaye ana njaa na uwezo wa kupata msosi hana!
Mi nilishajikataza kabisaaa kuwa mchoyo wa chakula, naamini nikitoa na mi nitapata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom