Unaendaje nyumbani kwa mtu bila taarifa?

Unaendaje nyumbani kwa mtu bila taarifa?

mi kwa imani yangu kuna watu walipokea watu nyumbani kwao wakawafanyia ukarimu kwa kuwachinjia kondoo alienona kumbe wale watu ni malaika wakamwambia mambo mazuri yakaja timia....kuna watu walitoa kibaba cha mafuta ya mwisho yaliyobakia kwa wageni mafuta yakazidishwa....acheni uchoyo mnaelekea kubaya.mwanamke ukalalamike kupika ugali mara mbili kweli haipendezi kabisa....mie napika kwa furaha zote..sharp

Sent using Jamii Forums mobile app
We utakua unatumia rice cooker au jiko la gesi ndio maana unaona poa tu, Kimbembe kwa wanaotumia kuni au jiko la mkaa.
Ila mbona hata kwenye mafundisho ya dini yako hilo jambo limekemewa?

Maendeleo hayana chama
 
Mie kwangu mtu aje tu, aje na taarifa asije na taarifa sawa tu, kwanza hizi taarifa ni kero wakat mwingine itabidi ujipange wee kama unataka kupika solo la harusini, akija bila taarifa ndio mpango kipo kinapikwa, hakipo atakunywa soda hata maji ya bomba pia, muhimu nafsi yako inatoaje, katika uislamu kuna hadithi inasema ina ammali bin niyatin, kila amali italipwa kwa nia, kuna mwingine anampikia mgeni wake vizur akiondoka huku nyuma anaanza kumsimanga kapika tu ili mradi, kuna mwingine anapika vizuri kwa sababu anajua tumeamrisjwa kuwakarimu vizur wagen wetu, kumkarimu vizuri ni kuna thawabu na mtu mwenda kumtembelea mtu kwake kuna thawabu zote ni ibada katika uislamu! So tufanye vitu kutoka moyoni kiroho safi sio kufanya kwa kuigiza, kaja kanikuta kuna sehemu nawahi namueleza ukweli kuwa hii ni saa 5 kamili, 5 na dk 20 nahitajika sehemu, kwanini tunafosi kuigiza maisha wajameni.. Kaja kuna samaki ndani na mie ninataka kusongewa ugali tutakula ugali, kakuta nagongewa mayai basi sawa tutatafuna, hakuna kitu kabisa hata glass ya maji sawa pia..

Sent using my nokia ya tochi
 
We utakua unatumia rice cooker au jiko la gesi ndio maana unaona poa tu, Kimbembe kwa wanaotumia kuni au jiko la mkaa.
Ila mbona hata kwenye mafundisho ya dini yako hilo jambo limekemewa?

Maendeleo hayana chama
halijakemewa unaambiwa tuwe wakarimu kwa wageni isipokua inakatazwa kwenda kupeleka miguu yako mara kwa mara kwa jirani yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
waswahili wenzangu hii tabia ya kwenda kwa mtu usiku bila taarifa yeyote alafu unayegemea ule,na mambo kama hayo hivi unategemea watu wajiandaeje sasa.
hivi kwa nini mnaendekeza hii tabia inayokera kupita maelezo.
kumbuka kupika chakula cha mtu mmoja ni gharama na pia inagharimu muda jamani.
kwa mfano ugali na wali kuupika inachukua karibia dakika 40 hadi lisaa
sisi wamama ukija kwetu hata bila taarifa inabidi upikiwe.
unamshtukiza mtu bila taarifa jamani

Huu ni ujinga kwa kweli na unakuta mtu anasimu na namba yako ya simu anayo ila atakuja kwako bila hata taarifa, tena kwa makusudi tu.
 
Dah nikekumbuka, kuna familia moja ukienda bila taarifa kuna mtu ana nuna kweli, mmmh kwanini uje bila taarifa, na hata kama ni ndugu chakula anaweza asipewe. Kazi kweli
 
Kimjini mjini mtu akija kwako saa tatu usiku tena bila taarifa huyo keshakula huko alikotoka.
 
Maisha yanabadilika simu zimeharibu undungu,enzi zile ukipata suprize ya mgeni unaona ni kama bahati Mungu kakumbuka kutembelewa.siku hz imekuwa tofauti
 
Mrs Dee? Akina Dani tupite kushoto hapa..
Ghafla nmemkumbuka yule ex wangu alikuwa anafupisha jina langu kwa kuitwa Dee.
 
Dah nikekumbuka, kuna familia moja ukienda bila taarifa kuna mtu ana nuna kweli, mmmh kwanini uje bila taarifa, na hata kama ni ndugu chakula anaweza asipewe. Kazi kweli
Kimsingi ukitoa taarifa umaana wa ugeni haupo tena
 
Kam kuinesha upendo ni kumpa chakula basi mpe chai tu ya mkono mmoja kam kiporo hakuna.
 
Huo uchoyo wa kiwango cha juu.... Wazazi wetu walikuwa hawana hayo... Na mtu alikuwa anapokelewa kwa mikono miwili.... Siku hizi... Ooo toa taarifaaa.... Mxcuuuuu!
waswahili wenzangu hii tabia ya kwenda kwa mtu usiku bila taarifa yeyote alafu unayegemea ule,na mambo kama hayo hivi unategemea watu wajiandaeje sasa.
hivi kwa nini mnaendekeza hii tabia inayokera kupita maelezo.
kumbuka kupika chakula cha mtu mmoja ni gharama na pia inagharimu muda jamani.
kwa mfano ugali na wali kuupika inachukua karibia dakika 40 hadi lisaa
sisi wamama ukija kwetu hata bila taarifa inabidi upikiwe.
unamshtukiza mtu bila taarifa jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunapoiga uzungu tukasahau uafrika mimi mtu kuja kwangu kunitembelea ni heshima na kunijali
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Back
Top Bottom