Unadhani tupo pekee yetu ulimwenguni kote? Je, viumbe wengine wapo wapi?

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Maswali ni mengi sana yaliyokosa majibu yakueleweka kuhusu dhana ya kuwepo na viumbe wengine katika maeneo mengine ulimwenguni kwetu, kwa kuchukulia kuna idadi kubwa ya mifumo ya nyota na sayari zake ambazo zengine zipo katika maeneo rafiki kabisa.

Maana halisi ya neno " Alien " ni Mgeni wa kutokea eneo lengine kabisa nje na dunia yetu au tuseme mgeni au kiumbe kisichokuwa na yoyote ya hapa duniani kwetu , Alien ni neno la kigeni lenye maan tajwa hapo juu.

Unidentified Flying Object kwa wafuatiliaji wa mambo haya yaa anga za mbali neno hili halitakuwa geni sana , Maana halisi ya neno hili ni kitu chochote cha ajabu kinachopaa katika anga yaani kitu kisichoweza kuelezeka kabisa kwa urahisi.

Wengi wamekuwa wakihusishanisha kitu hichi na neno Alien yaani kifaa hichi kitakuwa kina mahusiano ya moja kwa 1 na hawa viumbe Alien.

Suala la kufahamu kuwa tupo peke yetu au kuna uwepo wa viumbe wengine ni badi ndoto kubwa kwakuwa bado jambo hilo halijaweza kuthibitishwa na mtu yeyote yule bali wanadamu wamekuwa wakipata hisia pengine katika mfumo fulani wa nyota sayari fulani ndani yake inaweza ikawa imebeba viumbe hai , hii ni kutokana na kupata data mbalimbali kupitia vyombo vyetu tulivyowahi kuvituma , data hizo zinaweza zikawa based katika gesi mbalimbali zinazopatikana kwenye magimba hayo.

Hata katika mfumo wetu wa solar system kuna baadhi ya magimba yameonekana na kuwa gesi ambayo kikawaida haswa inawezs kubeba maisha ndani yake kama data zilizotumwa kutoka katika mwezi wa sayari ya saturn unaofahamika kama Encladus moon of Saturn, wanasayansi wanahisi pengine kuna viumbe ndani ya maji yanayopatikana katika mwezi huo.

Mawazo ya wengi yanakwenda mbali sana pale wanaposikia kuhusu uwepo wa viumbe wengine mbali zaidi na dunia yetu wengi wao wanadhani kiumbe ni lazima awe mwanadamu kama sisi, jambo hilo haliko sawa kabisa tunaposema kiumbe basi kile chenye sifa za viumbe hai kama tulivyosoma mashuleni.

Hadi sasa hakuna taarifa yeyote yenye kutuhakikishia uwepo wa viumbe wengin katika maeneo mengine kabisa ya ulimwengu wetu bali tumejawa na hisia kwakuwa, uwepo wa mifumo mengine ya nyota na sayari zake haiwezi kuwepo bila ya kazi maalumu ni lazima itakuwa na kazi zake kama ulivyo mfumo huu wa jua.

Dimension ni kikwazo kikubwa sana kwa sisi wanadamu pengine ndio daraja tulilonalo baina ya viumbe sisi na viumbe wengine.

Dimension ni maono, uono wa jambo ambapo kuna viumbe wengine wana maono makubwa kupita sisi, jambo la kuja hapa duniani pengine wanafanya hayo labda daraja la dimension ndio linaloleta utengano wa sisi kuwaona hao viumbe.

Dimension zipo nyingi sana zinazoweza kufika mpaka 16 zote zinasimamia maono ya kitu tu, huku mwanadamu wa kawaida akiwa na uwezo wa kuoma dimension 4 tu pekee yake.

Bado hatuwezi kukataa wala kukubali kuwa kuna uwepo wa viumbe wengine ila kuna viashiria vinavyotufanya tukubali uwepo wa viumbe hao.

🇬 🇪 🇷 🇦 🇱 🇩 
FB_IMG_1665308265706.jpg
 
Mkuu nakupa big up sana kwa mada zako huwa zina vitu vingi vya kuelemisha na kuhabarisha

Keep it up buddy
 
Back
Top Bottom