Unadhani ni mchumba kumbe si mwenzio! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unadhani ni mchumba kumbe si mwenzio!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mtafungwa, Mar 4, 2012.

 1. m

  mtafungwa Member

  #1
  Mar 4, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwanza nashukuru kupata fursa hii ya kulitembelea jukwaa hili kwa mara ya kwanza. Nawasalimuni ninyi nyote.

  Mie naanza na stori fupi kabla ya kuuliza swali kwenu. Hapo zamani nilipokuwa kijana (kwa sasa nishafikia umri wa miaka karibu 50), kama kawaida ya wengi, nilianza kupata hamu ya kuanzisha maisha yangu ya ndoa. Kwa hiyo nilianza kumtafuta mwenzi (wa kike, mie ni wa kiume). Nilipoona nashindwa kumpata, nilimuuliza bibi (nyanya) nini nifanye ili nipate huyo niliyemtaka. Akaniambia "uwe mwangalifu mjukuu wangu, halafu pia usiende kwa pupa. Chukua muda wako na umtafute polepole wala usijali kupita kwa muda maana kusemakweli muda huwa haupiti". Akaendelea "unajua kuna watu ambao huonekana kama watu vile lakini kumbe si watu, ni mwonekano tu". Akaendela tena "Kuna watu huzaliwa kwa masharti ya wataalam wa jadi na huzaliwa kwa uwezo wa wataalam hao pamoja na mizimu na miungu yao, si katika hali ya kawaida" Akasema "watu hao wapo duniani hawajaumbwa na Mungu ila wapo...sasa uwe mwangalifu usije ukatuletea kiumbe ukidhani ni mchmba kumbe sio mwenzio"

  Nilimwomba anifafanulie maelezo hayo naye hakutaka kufanya hivyo. Akasema "wewe kama mwafrika kweli kweli unatakiwa kuyajua haya na kama hujui waulize wenzio hata huko unakofanya kazi". Sikuulizia zaidi kwani katika ulimwengu wangu niloupata ktk shule za bweni na vyuo sikuona maana yoyote katika maelekezo yale. Lakini nikiwa mtu mzima yale maelezo yanaanza kuonekana yana mantiki fulani. Sasa mnipe msaada kwa kunijibia swali langu hilo hapa chini.

  Je ni kweli kwamba kuna wataalam wa jadi wanaoweza kumfanya mtu azaliwe kwa kutumia mizimu au miungu? Je ni kweli kwamba watu waliozaliwa kwa mtindo huo wapo? Mwanasayansi najua huwezi kuyajua mambo haya!

  Asanteni!
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  asante pia,
  ila ndefu, ngoja nipate kahawa ya jioni afu nirudi kusoma.
   
 3. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Shetani ananza kukuchanganya katika biashara zake, ili uzidi kukufuru.
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  watu kuzaliwa kwa masharti ya waganga wa jadi haimaanishi wameumbwa na waganga
   
 5. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Kama huyo mtu hakutokana na tendo la ndoa, hakuna sababu ya kutoamini maneno ya bibi yako!
   
Loading...