Unadhani kwanini hakuna muajiriwa tajiri au aliyewahi kuingia top ten ya matajiri nchini?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Hata tuweke top 1000 matajiri tanzania, huwezi kukuta muajiriwa hata mmoja...
Badala yake utakuwa
Wamiliki wa Makampuni yaliyoajiri
Wakulima wakubwa
Wafanyabiashara
Wabunifu na watu waliotajirika kupitia vipaji
Etc

Hii inatoa changamoto ni njia ipi ya kupita linapokuja suala la maisha ya kijana kwa malengo ya Muda mrefu...

Unadhani kwa nini waajiriwa wengi sio matajiri.
Ambao tunawaita matajiri wengi wanamiliki nyumba Nzuri na magari mazuri tu.
 
Unamjua Gugai?
 
Kwa Africa mwajiriwa anaweza kuwa tajiri lakini ni ngumu kumjua kwani wengi wanaficha coz hata ukimpatia karatasi moja kuandika utajiri kaupata wapi sidhani hata mistari minne inaweza kujaa katika maelezo yake pia unaposema neno (TAJIRI} wa maana ya RICH utakuwa unakosea coz utajiri unahusisha vitu vingi ikiwamo mali mfano leo kuna wamasai wanamifugo zaidi ya 1000 tayari ni utajiri lakini wanaishi maisha ya kimaskini inatakiwa ueleze utajiri wa nini ndo maana wenzetu wanalevel mfano millionaire mpka billionaire wakimaanisha uwezo wa kifedha tu lakini ukisema rich kwa maana ya tajiri wapo wengi sana ambao ni wafanyakazi na wameajiriwa
 
Kwa Africa mwajiriwa anaweza kuwa tajiri lakini ni ngumu kumjua kwani wengi wanaficha coz hata ukimpatia karatasi moja kuandika utajiri kaupata wapi sidhani hata mistari minne inaweza kujaa katika maelezo yake pia unaposema neno (TAJIRI} wa maana ya RICH utakuwa unakosea coz utajiri unahusisha vitu vingi ikiwamo mali mfano leo kuna wamasai wanamifugo zaidi ya 1000 tayari ni utajiri lakini wanaishi maisha ya kimaskini inatakiwa ueleze utajiri wa nini ndo maana wenzetu wanalevel mfano millionaire mpka billionaire wakimaanisha uwezo wa kifedha tu
Vyote mali na fedha. Hayo maelezo usimsahau na mwanasiasa wa Afrika. Asilimia kubwa kama sio zote wana hawawezi kujustfy mali na pesa walizonazo
 
Kuna yule jamaa walimtaja anamiliki nyumba 75, pia walimkuta nyumbani kwake alikuwa na ma diaba ya pesa, alikuwa ni mkurugenzi wa....! Nimesahau. Pia, wakubwa wengi wanaogopa kuwekeza nchini wanawekeza nchi za nje
 
Mitale na midimu,

Siwezi kukushangaa , ila tatizo lako huna taarifa tu za waajiriwa ambao ni matajiri na labda unakoishi ndiyo pamedumaza akili hadi ufahamu wako umefika mwisho.

Mfano, mtu analipwa, 50M Kwa mwezi bila kuweka malipo ya mikutano na matamasha. Zidisha hiyo hela uone ndani ya mwaka uone anakuwa na kiasi gani.

Nenda UN na UN agencies , African Union, Regional Blocs, Financial Institutions, Universities especially in Research Departments kisha njooooo ubadilishe huu uzi wako.

Ila Kwa sababu, watu wenye hizo ajira na hizo hela huwa hawajitangazi lakini ukweli ni kuwa wana hela, tena ni matajiri kabisa.
 
Hata tuweke top 1000 matajiri tanzania, huwezi kukuta muajiriwa hata mmoja...
Badala yake utakuwa
Wamiliki wa Makampuni yaliyoajiri
Wakulima wakubwa
Wafanyabiashara
Wabunifu na watu waliotajirika kupitia vipaji
Etc

Hii inatoa changamoto ni njia ipi ya kupita linapokuja suala la maisha ya kijana kwa malengo ya Muda mrefu...

Unadhani kwa nini waajiriwa wengi sio matajiri.
Ambao tunawaita matajiri wengi wanamiliki nyumba Nzuri na magari mazuri tu.
Kwa sababu mshahara wa kuajiriwa hauwezi kujilimbikiza vya kutosha kuwa na utajiri wa mali kihivyo. Simple mathematics.

Kwani kila mtu kakwambia anataka utajiri?

Kwa nini uko obsessed na utajiri?

Unajua kwamba ukiwa obsessed na utajiri hata ukiupata bado utakuwa masikini?

Na kuna mtu karidhika na maisha ya kawaida tu ana utajiri mkubwa kuliko hao matajuri wa top ten?
 
Lowasa mbona alikua ni muajiriwa lakini kwenye top 20,matajiri aliingia.mpaka kukodisha ndege nakumpa nyerere lifti haha
 
Back
Top Bottom