Kuna wakati huwa naziona siasa ni kitu cha kipuuzi kabisa kisichoakisi ukweli wala uhalisia wa kile kimachohubiriwa majukwaani na kupigiwa makofi mengiHalaf hao wanaokwambia ujiajir wao wameng'ang'ania vyeoo wanastaaf ila bado wanataka waajiriwe kwenye vtengo tuuuu
Hao jamaa ni matapeli na sijui kwanini serikali inawafumbia macho labda ni kwakuwa inawasadia kupunguza pressure ya ishu za ajiraNipo Kituo cha daladala hapa kuna tangazo la ajira na mshahara laki tatu sabini elfu kwa mwezi. Labda hii nayo inaweza kuwa fursa kwa we nye uhitaji wasting wakisubiria ajira ya ndoto yao!
Ungefanya la maana sana ukatutajia ni nani huyo kwani wengine sisi ni wazito kujua ni nani!![emoji86] [emoji86]Haya yote yamesababishwa na mtu mmoja
Kwaio huoni kuwa janga la ajira litazidi kuongezeka kwa hy reli? Fikiria kuna magari makubwa mangapi yanayopeleka mizigo huko na watu wanaoziendesha kupata kipato cha kuendeleza familia zao? Naona watakuja mitaani.Mkuu Drc kaskazini ni Rahisi kupitia Rwanda,na kusini ni Rahisi kupitia ,Zambia,kati ni kupitia kigoma
Utaona wazi kabisa hii ya Rwanda itarahisisha kubeba mizigo ya Goma na kivu ya kaskazini
Mtu akiyechaguliwa kwa kishindo chaguo la mungu. Akaanza kutalii badala kufanya kaziHaya yote yamesababishwa na mtu mmoja
Tunapopita mitaani asubuhi kwenda kazini na tunaporudi jioni wale vijana walioko vijiweni yale macho yao yanayotuangalia ukiwa makini kuyaangalia yanaongea mengi sana na kwa sehemu kubwa yamejaa maumivuUmeniwazisha sana mkuu, mshana jr ! Mungu wewe mkuu sana, itazame kila nafsi ya mmoja wetu!
Tuna shida kidogo kwenye vipaumbele vyetu kama kile cha kujenga reli kwenda Rwanda yenye watu milioni kumi badala ya kujenga reli kwenda DRC Congo yenye watu zaidi ya milioni mia moja
Ni wazi kuwa kila kimoja kina umuhimu wake lakini kwasasa nchi haina tatizo kubwa la usafiri wa anga! Pengine zile pesa za Bombardier zingetosha kujenga viwanda vidogo vidogo zaidi ya 20 na kuleta ajira zisizopungua 500...nina hakika ajira zitakazotokana na bombardier mbili haziwezi kuzidi miamoja nchi nzima
Vile vile ile project ya kuua upinzani nchini kupitia bwana yule na wengineo pesa yake ingetosha kujenga walau kiwanda kimoja cha matunda mkoani Tanga na kuzalisha ajira zisizopungua 100 kuanzia kukusanya kuuza kuprocess matangazo kutawanya na kuuza
Kwa njia hii tungewapunguzia vijana wengi stress za maisha bila ajira
View attachment 411685
Ni asubuhi ya siku nyingine tena, harakati zimeshaanza na nyingi Zikiwa ni kuwahi kazini au mishemishe pamoja na uchovu wa jana lakini huna budi kuamka na kujiandaa ili uwahi kazini
Ni katika kipindi hiki kwenye hizi harakati za kuwahi kibaruani kuna mtu yuko kitandani muda huu si kwa kupenda la hasha! Anaumia hana kazi naye angetamani muda huu awe anapasi nguo za kazini au yuko barabarani kuwahi
View attachment 411686
Anaumia sana akikumbuka alivyosoma kwa tabu na sasa ni mwaka wa tatu huu hana ajira huku washkaji zake wakipeta(mawazo mabaya huanzia hapa)kwanini na si mimi?kwanini wao wapate na mimi nikose? Kwani tunatofautiana nini? INAUMIZA SANA
Huwezi kuendelea kulala siku nzima utaumwa unaamua kutoka uende kijiweni au ukajaribu bahati yako popote lakini du mfukoni huna hata mia!inauma sana.
Siku yako inapita hivyo hivyo kimungu Mungu na jioni inapokaribia unaanza kuwaona watu wakirudi toka makazini, kwenye magari yao na wengine kwenye usafiri wa jumuiya wengine wamechoka wengine wanapiga story inaumiza mno unatamani na wewe ungekuwa mmoja wao
Unavuta picha jinsi ulivyochomekea na tai yako jinsi ulivyohudumia wateja wako kazini changamoto ulizokutana nazo..unajikuta kabisa ukitumika na kuhudumia kwa furaha unapotelea kabisa mawazoni mpaka unatabasamu, na ghafla unashtuka kumbe uko kijiweni honi ya mshikaji uliyesoma naye inakushtua yuko kwenye altezza anatoka job INAUMIZA SANA
View attachment 411684
tatizo la ajira ni la dunia nzima lakini hii isiwe kisingizio cha serikali...kila mwaka vijana wetu wanamaliza elimu zao wakitegemea kupata ajira...na idadi inaongezeka kila mwaka.. ! Hili linapaswa kuangaliwa kwa umakini zaidi hali ni mbaya sana mitaani