Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,619
Gazeti moja la kila juma linalochapishwa katika lugha ya Kiswahili, leo ukurasa wa mbele limeripoti CHADEMA kumuhitaji Dkt. Wilbroad Slaa tena kwa msisitizo eti "kwa wakati huu kuliko uliopita" kikitaja sababu kuwa ni uwezo wake wa kuelewa mambo na kutetea misimamo yake.
Naendelea kuamini kuwa kwenye siasa chanya inawezakuwa hasi na hasi inawezakuwa chanya. Huenda siku moja CHADEMA kikawahitaji Lowassa na Sumaye.
Julai 2, 2023, niliandika makala humu yenye kichwa "Dkt. Wilbroad Slaa ni dhahabu iliyokosa mteja?" Leo yanatimia.
Ushauri wangu kwa Dkt. Slaa kama ataridhia mwaliko huu, ni kuwa aende kukisaidia CHADEMA kutengeneza agenda ya kueleweka ya miaka hata 20 mbele ili kukiokoa na saratani ya "zero-agenda" ambayo inakifanya kuviziavizia matukio ya kitaifa na kuyadaka na kuyalazimisha kuwa agenda yake.
Matukio hayo yanapozimwa na matukio mapya ya kutengenezwa CHADEMA kinajikuta kinapoteza mwelekeo kwa sababu hakijatengeneza hayo matukio na matukio hayawezi kuwa agenda.
Hamu ya CHADEMA kumuhitaji Dkt. Slaa KWA DHARURA inathibitisha uelewa wangu wa siku zote kuwa urais siyo rangi ya nywele wala rika wala makunyanzi urais ni ubongo wa mtu, ndiyo maana Wamarekani walimchagua Obama kijana na leo wakamchagua Biden babu kabisaaa...
Kenya tu hapo, babu Mwai Kibaki ameacha legacy ambayo Uhuru Kenyatta kijana hajaacha. Kumbe urais ni ubongo wa mtu siyo mwonekano wa mtu. Mwl. Nyerere aliendelea kuisahihisha dunia na JMT hata katika umri mkubwa baada ya kung'atuka. Ni vivyo hivyo kwa rais Nelson Mandela wa Afrika Kusini.
Hadi hapa tulipo leo CHADEMA hakina agenda na CHADEMA hakina Presidential material. Kina kazi ngumu ya kusaka hivyo viwili ndani ya muda mfupi uliobaki wa kujiandaa. Asomaye na afahamu!
- Dkt. Slaa ni dhahabu iliyokosa mteja?
Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app