Una uhakika gani kwamba TB Joshua ni nabii fake?

Leo nimeamini kumbe NYANI HAONI KUNDULE!!!!!!!!!!!!Eti kichaa anacheka watu na kuwaambia wamerogwa na aliyewaroga kafa,Jitambue!!!!!!!

Nawewe nawe ndio walewale' unasapoti kashfa hii kisa wamegusa interest zako. Nawewe huko uliko utakuwa unajiita mlokole!!
 
Huyu naye ni nabii?!! Hebu nitajieni nabii wa kwenye biblia aliyewahi kusababisha maafa kwa wafuasi wake, mimi hainiingii akilini eneo lililojaa "upako" kukaweza kutokea dhahma ya kuuwa watu karibia mia, I thought kuna ulinzi mkali sana wa Mungu pale!!! yaani watu waliokuja kuponywa na nabii wa Mungu wanateketezwa na jengo la nabii huyohuyo?!! Mimi sipendi kujadili suala hili kiimani, ni suala la kidunia tu, negligence, dharau na kiburi ndiyo vimesababisha yote hayo, lakini kwa nini basi mada inachengeshwa sana na kufanywa ya kiimani?!!..hilo swali sijapata majibu bado.

Kwani si serikali yao itatoa ukweli, mbona mnaconclude
 
Ninyi mnaopinga kila nabii,kila mtume basi mtuonyeshe yule wa kweli tuende basi, ama yule mnaemwona nyinyi ni wa kweli,maana ata hawa watanzania hapa mnasema ni wahuni,mbona mnakuwa kama mafarisayo !

Mathayo 23:13 “Ole wenu ninyi, waandishi na
Mafarisayo, wanafiki! kwa sababu
mnawafungia watu ufalme wa
mbinguni; kwa maana ninyi wenyewe
hamwingii, wala hamwaruhusu wale
wanaoenda huko waingie.
 
Mnakosea kwa kuwa hamjui maandiko wala nguvu za mungu. Kuwa nabii si kwamba unaona kila kitu, tunaona kwa sehemu tu tena kwa fumbo ,basi anaeza kosea kupambanua.Tukiwa mbinguni basi tutajua yote.

1 wakorintho 13:8 Kwa maana tunafahamu kwa sehemu;
na tunafanya unabii kwa sehemu;
9 lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa
sehemu itabatilika....
11 Maana wakati wa sasa tunaona kwa
kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule
tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa
nafahamu kwa sehemu; wakati ule
nitajua sana kama mimi nami
ninavyojuliwa sana.
 
Ona hapa ,nabii mkubwa Elisha. Baada ya mtoto aliyezaliwa kwa mwanamke tasa aliyemwombea kufariki ghafla baada ya kupata ugonjwa wa ghafla kama ghorofa la TB joshua, Elisha alikiri kwamba bwana alimficha.
Sasa kufa kwa hao wasouth pia bwana anaweza kumficha TB joshua.
2 Wafalme 4:
27 Naye alipofika kwa yule mtu wa
Mungu kilimani, alimshika miguu.
Gehazi akakaribia amwondoe; lakini
mtu wa Mungu akamwambia, Mwache;
maana roho yake ndani yake ina
uchungu; na Bwana amenificha, wala
hakuniambia.
28 Yule mwanamke akasema, Je!
Naliomba mwana kwa bwana wangu?
Mimi sikusema, Usinidanganye?
29 Ndipo Elisha akamwambia Gehazi,
Jikaze viuno, ukachukue fimbo yangu
mkononi mwako, ukaende zako;
ukikutana na mtu, usimsalimu; na mtu
akikusalimu, usimjibu; ukaweke fimbo
yangu juu ya uso wa mtoto.
 
Kwani si serikali yao itatoa ukweli, mbona mnaconclude

hivi haukumsikia tb josh na wafuasi wake walivoconclude?!! au wewe ni mgeni na habari hii?!
mind you, system ya nigeria ni corrupt sana, afadhali hata sisi wahusika wa matukio kama hayo huwa wanakamatwa wanaachiwa baadaye, sasa wenzetu huyu mtu anadunda mtaani tu wakati kasababisha vifo vya watu karibia mia sasa!!!
 
No TB joshua alisema ana shaka na île ndege,akijaribu kuisisitiza serikali isidharau katika upelelezi wake,ila akasema hataconclude anaachia security. Sasa waumini sio wasemaji wala wapinzani. Rais Jonathan alienda akaona akatoa pôle kwa joshua na wafiwa ,alafu akaahidi uchunguzi wa haki
 
Kama nabii wa kweli alitakiwa kuona hilo tukio kabla halijatokea na hivyo watu waliokuwemo katika jengo wangehamishwa kabla ya jengo kuanguka na kupata madhara. Kwa hili lililotokea unabii wake ni "highly questionable" bila kujali utetezi dhidi yake wa watu kama wewe! Kwani Kibwetere alikuwa na watu wangapi na mwisho wake aliwapeleka wapi hao watu? Wajinga ndiyo waliwao.

Wewe wakati unawaza kuokoa ,mungu anaeza kuwa aliwaza hivi!

Zaburi 116: 15 Ina thamani machoni pa Bwana
Mauti ya watakatifu wake.
 
Iliyotokea ni ajali kama ajali zingine japo uzembe umechangia. Hakuna cha kafara wala ndumba

Pia TB Joshua ni mganga njaa kama waganga njaa wengine kama kina kakobe, rwakatare, lusekelo na wengine wote. Hana jipya zaidi ya kucheza na akili za watu hasa wenye matatizo (truth be told)

Bado sijapata jibu, inakuwaje mtu anamuamini mNigeria, hawa jamaa ni waongo, wajanja wajanja , waliotumwa pesa Kwa njia iwayo yeyote
 
Nyote,
Ni nani aliye na ukweli moyoni mwake juu ya haya yaliyotokea? Nina katika dunia hii anayeweza kusimama na kuthibitisha yanayoenea duniani kwamba waliokufa wametolewa kafara?

Ni Ujinga wa Kitanzania.
Imani za kishirikina zimetufanya kuwa wajinga sana wa TZ, nchi yetu maskini, elimu ndogo, magonjwa yanatundama 100%, lugha matatizo, uelewa tuko chini kabisa ya dunia, lakini unakuta kajitu kamekomaa kanasema TB Joshua ametoa kafara washirika wake, una uthibitisho? Peleka kwenye dola.

Unabii wake,
Hata kama ni nabii fake, kuna husiana nini na ajali? Yeye ni binadamu na anaishi duniani madhara kama haya huwa yanatokea je, yeye hayakumpasa kutokea? Hebu fikiria hapa tanzania ghorofa liliposhuka na kuua watu nini kilifanyika? mabomu ya mbagala mtu analipwa fidia 1900/ hala jitu na akili kama kamasi tu limekomaa TB Joshua, TB Joshua, TB Joshua pumbafuuu kabisa bila hata adabu. bora hata TB Joshua anasaidia watu na misaada sehemu mbalimbali, na mifisaidi yenu iliyoficha mabilioni nje? Eti inapeana zawadi bilioni 1? nchi ya watu maskini wanaotumiwa kama condom huku wakiwa wabishi wa kutupwa fungeni kinywa.

Unapata wapi ujasiri?
Unauhakika gani kwamba TB Joshua ni nabii fake? kama hauamini anayoyafanya ukinyamza utaonekana mjinga? Mtu mwenyewe unalalia kitanda cha chuma, ukiona laki utafikiri umepewa tibaijuka halafu ndo umevimba misuli kulalama Tb Joshua, watu maelfu hao wanaoingiaga kwenye kanisa la TB Joshua umewazidi akili? Elimu yako yenyewe ya divisheni faivu? IQ ndogo ndiyo zinaua taifa hili.

USIMHUKUMU MTU BILA USHAHIDI HATA KAMA AMEKOSEA NAYE NI BINADAMU, UNA USHAHIDI WA MAKOSA ANAYOFANYA PELEKA MAHAKAMANI.

Mtumishi wa Mungu
London

Aloo umekomaa kweli,utadhani TB Joshua sio nabii fake, he is.Yeyote anayetoa unabii usiotimia ni nabii fake.Ameshatoa nabii ambazo hazikutimia.Hiyu ni characteristic moja tu ya nabii wa uongo,Zipo nyingi ambazo anazo.Sikio la kufa halisikii dawa.
 
Hata Yesu alipokuwa msalabani aliambiwa na ajiokoe mwenyewe. Wanadamu wataongea mengi ni kupuuza tu. mwisho wa Siku ni kumwombea mtumishi wa Mungu

Sure,, ila YESU hakuuza maji chupa dollar 60 hilo nalo vipi
 
Kama nabii wa kweli alitakiwa kuona hilo tukio kabla halijatokea na hivyo watu waliokuwemo katika jengo wangehamishwa kabla ya jengo kuanguka na kupata madhara. Kwa hili lililotokea unabii wake ni "highly questionable" bila kujali utetezi dhidi yake wa watu kama wewe! Kwani Kibwetere alikuwa na watu wangapi na mwisho wake aliwapeleka wapi hao watu? Wajinga ndiyo waliwao.

Mnapotea kwa sababu hamjui maandiko... (by Jesus). Naomba nikueleweshe kidogo jinsi ofisi ya unabii inavyotenda kazi. Nabii ni binadamu ambaye anaoneshwa na Mungu mambo yatakayotokea mbeleni. Kumbuka kuwa anaoneshwa na Mungu, haoni mwenyewe, ni mpaka aoneshwe na Mungu.

Therefore Mungu asipomwonesha hawezi kujua kitu chochote. Na pia lugha anayoitumia Mungu kumwonesha ni prophetic language, anaweza asiweze kuitafsiri vizuri na ndio maana kuna wakati huwa anasema naona kama kitu fulani kinaweza kuwa na maana hii...n.k

Nakumbuka kuna nyakati kadhaa amekuwa akisema ameona kuna ndege angani inaanguka mahali mahali, yawezekana alikuwa anaoneshwa kuhusu jambo la kiroho litakalotokea kwake na kusababisha madhara ila kwa kuwa pia ni mwanadamu hakuweza kuwa 100% sure kuwa linamhusu yeye.

Lugha za Mungu huwa ni symbolic. Unakumbuka Yohana kwenye Ufunuo alikuwa anaoneshwa maono lakini ilikuwa inamuwia vigumu kidogo kujua exactly ni kitu gani. Kuna wakati akawa anasema, kisha nikaona kitu mfano wa mwanadamu, au mfano wa bahari au kama nzige, n.k Kwa hiyo tafsiri ya lugha hizo za kimbinguni sometimes zinaweza kumfanya hata prophet kama T.B Joshua kumiss the exact meaning. Na Mungu anaendelea kumtrain through these challenges kama vile ambavyo mtoto anaweza kuanza kutembea halafu akadondoka na akavunjika mguu, kwa Mungu its part of a learning process.
 
Ninyi mnaopinga kila nabii,kila mtume basi mtuonyeshe yule wa kweli tuende basi, ama yule mnaemwona nyinyi ni wa kweli,maana ata hawa watanzania hapa mnasema ni wahuni,mbona mnakuwa kama mafarisayo !

Mathayo 23:13 "Ole wenu ninyi, waandishi na
Mafarisayo, wanafiki! kwa sababu
mnawafungia watu ufalme wa
mbinguni; kwa maana ninyi wenyewe
hamwingii, wala hamwaruhusu wale
wanaoenda huko waingie.

manabii wa kweli wapo kwenye kitabu chako kitakatifu kama umeshindwa kuwaamini hao basi ungana na matapeli uliwe kichwa fasta. hao wanaoibuka miaka hii wote fake kila mmoja anamponda mwenzake
 
manabii wa kweli wapo kwenye kitabu chako kitakatifu kama umeshindwa kuwaamini hao basi ungana na matapeli uliwe kichwa fasta. hao wanaoibuka miaka hii wote fake kila mmoja anamponda mwenzake

Mmmh! Kwa hiyo na wachungaji nao wako kwenye kitabu changu,wanichunge leo?
 
naona umekuja kuharisha hapa f.ala wewe eti unajiita mtumishi wa mungu unaongea kashfa kiasi hiki ni mtumishi wa aina gani wewe. na kama uko ldn ondoka rudi afrika wanakopatikana wajinga kama wewe. siyo siri umenichefua sana
 
Back
Top Bottom