Una kipawa gani?

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Posts
23,372
Reaction score
55,049
Kila mtu ana kitu kile ambacho mwenzake hana na kila mmoja anatumia kipawa chake kwa usahihi kabisa kuliko mwenzake.

Kipawa na uwezo wa kufanya kitu chochote kile ambacho kinaweza kuwa kigumu kwa baadhi ya watu/mtu (Kipaji)

Naamini kila mmoja anajua kipawa chake hadi sasa kama huna kipawa basi pole sana na Mungu akuoneshe kipawa chako na jinsi ya kukitumia.

Kwangu mimi nina kipawa cha USHAWISHI nasema hili kwa uhakika sana ninaweza kushawishi pande mbili kuwa sawa au pale ambapo hakuna amani kukawa na amani, naweza kubadilisha mtu mawazo yake na akaenda vile navyotaka kwa muda mfupi sana.

Kwangu mimi Najivunia sana kuwa na kipawa hiki wote ambao wamekuwa na mimi wamejikuta wanapita njia yangu, marafiki, wapenzi, ndugu na jamaa.

Kwako wewe una kipi unachoweza kushukuru Mungu kuwa amekupa kitu cha kipekee kuliko yeyote?

Karibu.
 
Natambua fikra za MTU kwa kumwangalia tu. Haihitaji anieleze. Nikimuona tu physically basi. Sikusomea na wala si kwa dawa.
Naajiuliza sana no uwezo gani Mola alinipa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…