Una jambo gani la matumaini la kuwaambia watu waliokata tamaa kabisa?

Nilitamani kusikia hatma ya yule manzi aliekuita nyumbu alliishia wapi??
 
Ndio ukweli,kwenye maisha tunapitia magumu mengi.baada ya form 4,nikaenda college,Wazazi walilipa nusu ada ya muhura wa kwanza,mwaka wa kwanza,ada yote mpaka namaliza,nili hustle mwenyewe,ukiniuliza nilimaliza vipi chuo,kwa kweli ni miujiza TU,nimemaliza chuo,nilipokuwa nakaa,anko wangu ananishuku nimemwibia,vituko kibao,hiyo ni 2006!hata simu Sina!
Ikatoka kazi gazetini,wenzangu wakaiona,nikatumiwa,nikapata kazi,maisha yakabadirika,
Cha msingi usikate tamaa,hatq kama mbele Ni Giza tupu,Mungu Huwa na namna anavyotwist mambo ili deal ikuangukie wewe.
 
Kila mtu akate alicho nacho. Kama ana tamaa aikate hiyo, kama ana mafanikio naye ayakate hayo. Mtu kakata tamaa unataka kumfanyaje? Akukate wewe?
Ahsante huu mchango wako unaendana na jina lako! Daaah nimejikuta nacheka tu
 
Kila lenye Mwanzo halikosi kuwa na mwisho ,

Achekae mwisho hucheka sana.

Hili nalo litapita tu.
 
Wasihofu, mwisho wote tutakufa tu. Yote tunayofanya hapa duniani ni ubatili mtupu. Wako wapi walioishi mwaka 1507?
 
Imeandikwa: “

Mtumaini Bwana Mungu kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe, katika njia zako zote umkiri Yeye , Yeye atanyoosha mapito yako”

Pia Imeandikwa:

“Tumaini la Bwana halitahayarishi”

Tafakali kwa kina .
 
Nyakati ngumu hazidumu, usife moyo yatapita.
 
Usijal maisha ni mapambano hakuna kukata tamaaa
Mtegemee mungu , pale unapodondoka inuka endelea na safari,changamoto zinatokea kwny maisha ili kutufunza na kutuimarisha ,, wakati wa Mungu ni sahihi
 
Umenena vyema
 
Kwenye haya maisha, ili utie huruma make sure wapo watu wa kukuonea hiyo huruma, tofauti na hapo option ni moja tu "Kukaza"

Usimlaumu mtu yeyote kwa hali yoyote ngumu utakayokuwa unapitia. Never feel too comfortable.
 
Kuna wakati tunakata tamaa haswa tunapojaribu kujipambania nakufeli mara nyingi na kila ukitafuta wakukupa mkono hakuna upo mwenyewe katika vita usiojua utaishinda vipi na lini
Broh maisha yako ni yako. Hata hao unaotamani wakushike mkono, nao wanahitaji kushikwa mkono hivyo hawawezi kukuangalia wewe muda wote.

Ukishaona huna mtu wa kukupa back up, inabidi ikusaidie kujua future yako inadepend kwako 100%. Wengi wamechelewa kufika kwa kusubiria support toka kwa wengine. Make sure hukati tamaa broh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…