Dah kidume cha mwaka mmoja kimesha jua kuzama chumvini vilivyo . Sio ma huse girls tuu, pia wanao weka ma house boys , Vijana wengi wakiume wamepoteza bikra zao kwa ma haus geli , najiuliza kw asasa je vijana wanao balehe na ndani kuna demu katoka kijijini je watanusurikaje na Ukimwi?
KUna kisa kingine cha ukimwi nilisikia kwenye radio hicho kina iskitisha na kutisha sana , nikajiuliza utaepukaje kitu kama hiki? kilikua kama hivi
Mama mmoja ambaye ameolewa na kujaaliwa kupata watoto wata ,wakiwa kwenye maisha mazuri ya ndoa na majirani, kipato chao kizuri kiasi cha kuonekana wao tofauti mtaani kwao.
Watoto wao walikua na range ya miaka 12 ,9,6,3 na 1, walio na afya njema , mara chache huw awan sumbuliwa na maralia ikawa ina bidi kupelekwa hospitali na kuandikiwa sindano za masaa.
Siku hazikupita nyingi yule mtoto mdogo wa mwisho ambaye alikua na mwaka mmoja ,akaanza kuugua magonjwa yanao husiana na ukosefu wa kinga, wakajaribu kila njia vipimo vyote lakini mtoto akazidi kuugua na kufariki.
Baada ya kuzika tu wamekaa muda mfupi mtoto wa nne kuzaliwa ambaye ana miaka mitatu , naye akaaanza kuumbulia na ugonjwa kama ule ule ulio muua mdogo wake, wakaangaika vipimo lakini wapi mtoto akafariki,
Haikupita tena muda baada ya kuzika mtoto wa tatu , ambaye ana mika 9 naye akanza kuugua vile vile na kuwashangaza wazazi , ndipo yule mama akashauriwa kwenda kwa mganga labda karogwa, kupiigiwa ramli kaambiwa karogwa , tiba za asili na yote wameendelea hakuna nafuu mtoto bado mgonjwa.
Ndipo wakashauriwa wampime mtoto HIV, kitu ambacho kiliwashangaza pale majibu yallipo kuja, wakakuta ni kwamba mtoto kaathirka.
Ugomvi mkubw aukatokea na kuleta mgogoro mkubwa kwani kila mmoja akimtuhumu lmwenzake kwamba ndio kaletta ukimwi nyumbani mbaka watoto wameambukizwa, ikashauriwa fammilia nzima ipimwe, Yani baba , mama, nawatoto walio salia. Majibu yalipo rudi wote wakakutwa ni hawaja athirika ni wazima wenye afya , swali likaja je hawa watoto wamepataje Ukimwi?.
Muda ukafika yule mtoto akafariki na kuleta majonzi makubwa , na kuacha maswali mengi inakuaje watoto walio chini ya umri wa maiaka 10 wawe na ukimwi bila ya kuzaliwa nao nini haswa?
Siku zikapita ,bila tatizo lolote la Afya ,mbaka siku moja, huyu mama alipo rudi kazini jioni na kuambiwa unaombwa uende kwa jirani yako ambaye ni nesi ambaye ni mgonjwaa taabani, naye akaitikia wito kwenda kwa yule jirani ambaye ni rafiki yake na wanasaidia na mambo mengi ya kijamii.
Kufika hapo kama kawaida ni alikua mgonjwa sana na alimkuta Mchungaji wa kilokole hapo.
Nesi alipo muona ,huyu mama anakuja , akaanza kulia sana na kumwambia kwamba yeye ana kufa ila kuna dhambi mbaya anataka atubu mbele yake kwani kamtendea jambo baya sana , yule mama akawa ana shangaa jambo gani hilo litakua , ndipo yule nesi akaanza kwa kusema kusema "naomba msamaha mkubw akwako na kwa Mungu, kwani yeye ndio sababu ya watoto wa huyu mama kufa kwa Ukimwi" akaulziwa kivipi mbaka yeye awe sababu, akasema" Siku ambazo wale watoto wakiumwa maralia ana kaundikiwa dozi ya sindano, yeye ali muomba huyu mama kua awachomee nyumbani kwake sababu ya kupunguza safari za kwenda hospitali usiku ,sasa wakati kabla hajawachoma alijijua kathirika ndipo alipo amua kujichoma yeye sindano , halafu kuwachoma watoto akijua kua ana wambukiza virusi"
Yule mama kusikia hivyo , alizimia, alijikuta yuko hospitali .
Sikujua iliishaje, mana nilikau kwenye gari nakwena kwnye meeting so sikuweza kukaa kuimaliiza ila ili nisikitisha sana.