Halafu Mkwawa ndugu yangu hao wanaosema wanasaidia,kiufupi wanahali mbaya sana kimaisha.Wananchi wengi marekani hawana kazi wala mahali pa kuishi na kutegemea kupewa chakula na serikali.Kwahiyo hapa mimi naona ni danganya toto tu hiyo ikiwa ndani ya nchi yao inaanguka kiuchumi halafu wao tena wanasaidia nchi nyengine hii haingii akilini.Mimi naishi nje zaidi ya miaka 15 sasa najionea mwenyewe kwa macho yangu jinsi hali ilivo na inasikitisha.Na kingine Mkwawa kuhusu hii misaada yao,wakitoa hata huku kwetu yaani tunatukanwa nahawa wananchi ile mbaya.Kama nilivokueleza wakiwa wanatoa hiyo misaada hutangaza ktk media zao halafu uone hizo coment za wananchi wanavotutukana na kutunyanyasa.Kiufupi tu tuwaache hao Palestine wajiongoze wenyewe na wapewe nafasi na wao washirikiane na mataifa watakaowataka.Yeyote atakaetaka kuwasaidia wacha wasaidie wasiotaka na waache.