UN Ina wasiwasi na maandamano ya kenya

UN Ina wasiwasi na maandamano ya kenya

jamaikatz

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2023
Posts
395
Reaction score
1,398
Umoja wa Mataifa umesema kuwa una wasiwasi sana na vurugu zilizotokea wakati wa maandamano nchini Kenya ambapo takriban watu 16 walifariki huku wengine wakiwa na majeraha huku wakitoa wito wa utulivu na kujizuia

Maandamano ya Jumatano yalianza kwa amani lakini yakaishia kuwa machafuko huku maafisa wa polisi wakitawanya waandamanaji kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi.

"Tuna wasiwasi sana na ripoti za vifo vya waandamanaji kadhaa na majeruhi yaliyojumuisha waandamanaji na maafisa wa polisi wakati wa maandamano nchini Kenya siku ya Jumatano"

"Tuna wasiwasi na ripoti kwamba baadhi ya waandamanaji walikuwa na majeraha ya risasi"

"Chini ya sheria ya kimataifa ya haki za kibinadamu, utumiaji wa nguvu kupita kiasi wa maofisa wa kutekeleza sheria, kama vile silaha, zinapaswa kutumiwa tu inapokuwa lazima kufanya hivyo" amesema msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Elizabeth Throssell

Maandamano hayo yalikuwa kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu maandamano ya kupinga mswada wa fedha 2024 ambapo vijana wa Gen Z walivamia Bunge.
 
Wapuuzi sana hao UN,yaani Waandamanaji wakidhuru polisi na kuiba mali za watu ni poa,lakini polisi wakipindisha hata mtu mmoja tu kesi zinaanza,hao waandamanaji ni wahalifu na dawa ya muhalifu ni kuwatuliza by force.Akitokea kufa mmoja basi atakuwa amekufa kishujaa.
 
Back
Top Bottom