Inaelekea wewe ni polisi Trafiki.Huwaga wanakimbia Sana Hawa wafanyakazi wa serikalini walipigwa tochi manyoni mbele wakapata ajali na kufariki woote,RIP hawakusimamaView attachment 907478View attachment 907479View attachment 907481View attachment 907483View attachment 907484
Usiwe na hasira na Traffic police. Nini uelewa wa dereva? Kuwa na namba za ST isiwe ni umaarufu wa kukiuka sheria. Hiyo inayoonyeshwa ni somo kwa wote! Ukikimbia mkono wa sheria ukakutana na ajali na kifo, nini umwamba wako? Tunakutana nao barabarani na wanalazimisha uwapishe, eti tu kwa sababu kawasha taa kuonyesha ana haraka, mara unawakuta morogoro wnakula supu! wakiondoka upuuzi ule ule!Inaelekea wewe ni polisi Trafiki.
Utetezi wako hautoshelezi.
Huna simu ili iwekwe road block mbele?
Mikono ya kazi yako ina damu!
chakwanza mimi sio polisi,na chapili hizi picha zilitolewa mitandaoni na polisi baada ya hii ajali kusudi madereva wazembe wajifunze kitu,na cha tatu jukumu la kusimamia sheria hasa za barabarani si la polisi pekee bali nilakila mtu hata hao waliopata ajali walitakiwa wajijali wao kwanza kwa kufuata alama za barabarani na kuwa na mwendo ambao hauta hatarisha maisha yao,damu zao zipo juu ya vichwa vyao wenyewe hasa dereva ambaye alikuwa anakimbia bila kufuata alama za barabarani,usitegemee traffiki wakusaidie na namna ya kuendesha gari kama huwezi kufuata sheria za barabarani kwa manufaa yako na yawengine usiendeshe gariInaelekea wewe ni polisi Trafiki.
Utetezi wako hautoshelezi.
Huna simu ili iwekwe road block mbele?
Mikono ya kazi yako ina damu!
Shida ni kuwa Madereva wengi wazoefu wameondolewa na vyeti feki ndio maana waliopo ambao ni vijana wanamaliza watu na kukimbia hovyo wakidhani ni ushujaa.Mara baada ya maafisa waandamizi kuhamia Dodoma kumekuwa na mtindo mpya wa uendeshaji magari barabarani. Kila gari ya serikali itokayo Dodoma kwenda nje ya mkoa huwasha taa na kukimbia kwa mwendo kasi zaidi ya alama za barabarani.
Huu ni umwamba wa kijinga kwa kisingizio cha haraka au dhalula. Haiwezekani kila gari ya serikali iwe na dhalula na uhitaji wa mwendo kasi kiasi hicho. Matokeo yake ni hizi ajali ambazo zingeweza kuepukika.
Isingekuwa tatizo kama ajali ni zenu tu lakini ukweli ni hata waendeshaji wengine munawaingiza ktk ajali za kizembe kama hizi.
Hakuna sababu ya kutofuata sheria na alama za barabarani kwa kisingizio cha haraka au dhalula. Fuateni sheria na kuacha kuchekelea mwendo kasi. Polisi munashindwa kuwatia adabu watu hawa kwa uzembe wenu pia!
Spidi na vituko hivi vimeanza kipindi hiki baada ya kuhamia Dodoma, maana kuvunja sheria za barabara kwa kisingizio cha uafisa wako, kilikwama kipindi kile mke wa waziri mwenye maringo alipotiwa kibano. Nawaangalia watumishi hawa wa serikali kama kikundi cha watu wanaojiamini wao wako juu kwa ufahamu. Nahisi ni ile syndrome ya kuhama Dar wanaamini bado Dodoma ni mkoani, kumbe wote wamehamia Dodoma. Ujuaji mwingi bila sababu!Hawa jamaa wanakimbia mwendo Wa hovyo sana na watakufa mpaka wakome Leo nilikuwa naenda iringa walikuwa wanatupita kama tumesimama
Lakini madereva hawa, wanakuwa na mabosi wao pembeni. Inakuwaje hata bosi hajitambui kiasi hicho?Shida ni kuwa Madereva wengi wazoefu wameondolewa na vyeti feki ndio maana waliopo ambao ni vijana wanamaliza watu na kukimbia hovyo wakidhani ni ushujaa.
Ha ha ha ha ha haKwa mtaji huu madereva vijana wengi watapotea na abiria wao wakicheza na malori yenye mwendo na yaliyosheheni mzigo.
Naungana na mtoa hoja mmoja hapo juu.Shida ni kuwa Madereva wengi wazoefu wameondolewa na vyeti feki ndio maana waliopo ambao ni vijana wanamaliza watu na kukimbia hovyo wakidhani ni ushujaa.
Najiuliza; Hapo kuna dereva wa darasa la saba aliyeajiliwa kabla ya katazo au kuna form 4 fulani aliyebahatika kuajiliwa. Pembeni kuna afisa msomi wa kiwango cha University mwenye uelewa kiwango cha kuiendeleza nchi. Eti hawa kuna kipindi wana mawazo ya aina moja kwamba tukimbize gari. Polisi wakitusimamisha wee nenda tu! Overtake! Halafu wakifika salama dereva huyu anapongezwa kwa kuaminika. Lazima dereva ajisikie sifa kwa kupongezwa na msomi wa wizarani. Sasa wasipofika kama hii iliyotokea, eti tunasema madereva wabaya. Hapana! Dereva anamkoga bosi, naye anakogeka na kutoa pongezi!Wapumzike kwa amani ila hata abiria wanachangia kutokea ajali tusilaumu madereva pekee. Wakati dereva anakimbiza gari walimkemea? Mimi upumbavu wa kuonyesha umwamba kukimbiza gari siuvumiliagi. Kwanza gari ikiwa speed napata panic attack. Tuanze kukataa mwendo kasi sisi kabla ya kupeleka lawama kwa madereva