Umwamba barabarani wa maafisa wa Serikali mlioko Dodoma, unatumaliza kwa ajali

Ndomana na mispidi yao hyo huwa wanapata ajali hadi wengine kupoteza maisha

Ova
 
Inaelekea wewe ni polisi Trafiki.
Utetezi wako hautoshelezi.
Huna simu ili iwekwe road block mbele?
Mikono ya kazi yako ina damu!
Unamuoneà tu polisi wa watu, alichotaka kufanya ndicho kiñgewasaid8lia hao madereva lkn wakashupaza shiñgo akaachana nao. Je huko walikokimbilia??
 
Spidi na vituko hivi vimeanza kipindi hiki baada ya kuhamia Dodoma, maana kuvunja sheria za barabara kwa kisingizio cha uafisa wako, kilikwama kipindi kile mke wa waziri mwenye maringo alipotiwa kibano. Nawaangalia watumishi hawa wa serikali kama kikundi cha watu wanaojiamini wao wako juu kwa ufahamu. Nahisi ni ile syndrome ya kuhama Dar wanaamini bado Dodoma ni mkoani, kumbe wote wamehamia Dodoma. Ujuaji mwingi bila sababu!

Ukiangalia watumishi hao wa wizara ya kilimo walikuwa wengi ktk gari moja na ni watu wazima, wote above 30. ilikuwaje asipatikane hata mmoja mwenye uelewa wa kutoa onyo kwa wenzake na kusikilizwa. Ni kama walikuwa wanamchochea dereva wao asisimame. Wana haraka! Wana kazi muhimu, nk. wako wapi sasa! Nahisi pia ktk hii tumbua tumbua, kuna watu wamepewa madaraka premature. Ukiona mtu anapewa ukurugenzi na anajivuna kwa hilo kama yule aliyewahi kumtolea bastola traffic police pale Morogoro, hiyo ni ishara ya ubora duni wa akili. Ukiwa Mkurugenzi, Mbunge, Waziri, public figure, boss fulani, inatakiwa uwe smart! Ujue risk za kila jambo, hata maneno unayotumia yawe standardized. Leo hii ni bureeeee!
You have narrated the whole bittersweet truth
 
Mara baada ya maafisa waandamizi kuhamia Dodoma kumekuwa na mtindo mpya wa uendeshaji magari barabarani. Kila gari ya serikali itokayo Dodoma kwenda nje ya mkoa huwasha taa na kukimbia kwa mwendo kasi zaidi ya alama za barabarani.

Huu ni umwamba wa kijinga kwa kisingizio cha haraka au dhalula. Haiwezekani kila gari ya serikali iwe na dhalula na uhitaji wa mwendo kasi kiasi hicho. Matokeo yake ni hizi ajali ambazo zingeweza kuepukika.

Isingekuwa tatizo kama ajali ni zenu tu lakini ukweli ni hata waendeshaji wengine munawaingiza ktk ajali za kizembe kama hizi.

Hakuna sababu ya kutofuata sheria na alama za barabarani kwa kisingizio cha haraka au dhalula. Fuateni sheria na kuacha kuchekelea mwendo kasi. Polisi munashindwa kuwatia adabu watu hawa kwa uzembe wenu pia!

STK, STL, DFP Ni matatizo sana hawa jamaa wako rough utafikiri wana matumbo ya kuharisha
 
Nimesikia tena maafisa wa TANROAD Kagera wamekumbwa na ajali! Hao nao ni umwamba tu! Ukikutana nao wana feelings kwamba barabara ni mali yao. Lazima elimu itusaidie badala ya kutuongezea matatizo. Tunasingizia madereva wapya lakini naamini ni mentality mbaya ya kutaka kuonekana superior.
 
Nimesikia tena maafisa wa TANROAD Kagera wamekumbwa na ajali! Hao nao ni umwamba tu! Ukikutana nao wana feelings kwamba barabara ni mali yao. Lazima elimu itusaidie badala ya kutuongezea matatizo. Tunasingizia madereva wapya lakini naamini ni mentality mbaya ya kutaka kuonekana superior.
Ilo kweli
 
Ndo madhara ya kulazimisha watu wahamie dodoma bila maandalizi....wewe unategemea nini mtu anaishi Dar lkni kituo cha kazi ni dodoma kwahiyo hamna namna akichelewa atatumbuliwa bure, familia yake na mkopo nani atavimudu akikosa ajira kwa ujinga wa kufuata sheria za barabarani....hamna jinsi mkuu.
Siyo sababu
 
Usiwe na hasira na Traffic police. Nini uelewa wa dereva? Kuwa na namba za ST isiwe ni umaarufu wa kukiuka sheria. Hiyo inayoonyeshwa ni somo kwa wote! Ukikimbia mkono wa sheria ukakutana na ajali na kifo, nini umwamba wako? Tunakutana nao barabarani na wanalazimisha uwapishe, eti tu kwa sababu kawasha taa kuonyesha ana haraka, mara unawakuta morogoro wnakula supu! wakiondoka upuuzi ule ule!

Binadamu anayependa umaarufu eti hakamatwi, tunapita tu, wanatuogopa, sisi muhimu, sisi waheshimiwa, n.k. haiwasaidii zaidi ya hatari kwao na kwa wengine. Maisha ya umaarufu ni mafupi sana! Barabara ya Dodoma - Dar imekuwa ni ya kuwasha taa tuuuu na overtake za kishenzi tu.
Na watakufa hadi akili ziwakae sawa.
 
Najiuliza; Hapo kuna dereva wa darasa la saba aliyeajiliwa kabla ya katazo au kuna form 4 fulani aliyebahatika kuajiliwa. Pembeni kuna afisa msomi wa kiwango cha University mwenye uelewa kiwango cha kuiendeleza nchi. Eti hawa kuna kipindi wana mawazo ya aina moja kwamba tukimbize gari. Polisi wakitusimamisha wee nenda tu! Overtake! Halafu wakifika salama dereva huyu anapongezwa kwa kuaminika. Lazima dereva ajisikie sifa kwa kupongezwa na msomi wa wizarani. Sasa wasipofika kama hii iliyotokea, eti tunasema madereva wabaya. Hapana! Dereva anamkoga bosi, naye anakogeka na kutoa pongezi!
Si sababu
 
Wapumzike kwa amani ila hata abiria wanachangia kutokea ajali tusilaumu madereva pekee. Wakati dereva anakimbiza gari walimkemea? Mimi upumbavu wa kuonyesha umwamba kukimbiza gari siuvumiliagi. Kwanza gari ikiwa speed napata panic attack. Tuanze kukataa mwendo kasi sisi kabla ya kupeleka lawama kwa madereva
Amen
 
Back
Top Bottom