Umuhimu ya kuwa na mke

Umuhimu ya kuwa na mke

Bazazi

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2008
Posts
2,806
Reaction score
3,502

Bazazi kwa muda sasa, amekuwa akishambuliwa na kushutumiwa sana na baadhi ya wanajamvii kutokana na yeye kila wakati kutoa mawazo mbadala (hasa upande wa kushoto kwani wengi hulalia upande wa kulia). Hali hiyo imewafanya baadhi ya hao washutumu kumuita Bazazi ni bazazi badala ya Bazazi ni Bazazi! Kutokana na mashutumu hayo, leo amekuja kivingine kabisa ingawa sio kwa kutegemea akili yake tu, bali kwa kunukuu maandishi ya karne ya pili kabla ya Kristo (162KK) kutoka katika kitabu cha Yoshua Bin Sira 36:21-27 (Jerusalem Bible).

21.
Mwanamke atamkubali mwanaume yeyote,
Ila Binti mmoja ni mzuri kuliko mwingine.
22. Uzuri wa mwanamke huuburusha uso,
Wala mwanaume hatamani neno lolote kuliko huo;
23. Aidha akiwa nao ulimi wa unyenyekevu,
Mume wake si mfano wa wanadamu.
24. Apataye mke hujipatia mali iliyo bora,
Msaidia wa kufaa, na nguzo ya kumtegemeza.
25. Pasipo ukuta shamba la mizabibu litafanyika ukiwa;
Naye asiye na mke atapata kuwa mtoro asiye na kikao.
26. Ni nani atakaye waamini kundi la wanyang’anyi warukao huko na huko.
27.
Kadhalika mtu asiye na kioto,
Mwenye kulala ovyo wakati wa usiku popote alipo.


Tutaendelea kujuzana ambayo nitaona yanafaa kuwapasha ndani ya kitabu tajwa.


Ndimi Bazazi!
 
Una kiherehere!!...... hukulazimishwa kusoma wala ku comment! Pambafu zako wana izaya!
Acha kuiga misemo yangu..... nimekwambia ukweli na hili sio jukwaa la dini
 
ni kweli Bazazi mtu asokuwa na mke ni kama mnyang'anyi mtu ambaye hulala huku na kule pasi kuwa na makazi maalum. imeandikwa hivi moyo wa mwanaume utaambatana na mkewe so asokuwa na mke moyo wake huzurura tu pasi sababu.
 
Last edited by a moderator:
Umeona ee Madame B! Kuzozana na shooga kazi kwei kwei. Nimeachana na mtu anayepumuliwa mgongoni.

Bazazi ni Bazazi!

Ila Acheni malumbano.
:ban: itakuwa haki yenu wapendwa.
 
Last edited by a moderator:
napita tu wakuu....naenda kule kwenye jukwaa lile la wakuu bw aaaaa.....
 
Back
Top Bottom