Umuhimu wa ndoa kwako

Umuhimu wa ndoa kwako

pesa sio msingi wa ndoa
hakuna pesa au mshahara unaotosha duniani
msingi wa ndoa ni baraka
babu yangu alikuwa hana mshahara lakini
yuko kwenye ndoa mpaka leo, ndoa yao ina miaka zaidi ya 80.
Alifanikiwa kupata watoto 12 na woote akasomesha mpaka wa kike.
Hawana pesa lakini wana furaha.....na ndio maana wanaishi mpaka leo hii.
 
Eiyer, usiangalie flani amesemaje, wengi wanaongozwa na unafiki tu. Cha msingi ni kufuata kanuni ulizojiwekea.

Unaweza kujichelewesha kuoa kisa unatafuta pesa, bahati mbaya usiipate hiyo pesa na hata familia uchelewe kuwa nayo. Huwa haya meneno ya "tafuta pesa ndio uoe" yanatoka kwa singles. Labda tungepata insights za wanandoa tungeweza kuoanisha hili swala la pesa na ndoa kwa urahisi zaidi. Coz naona linaleta sintofahamu kubwa katika kizazi chetu.

Mkuu kuna watu wengi sana walioa wakiwa hawana kitu lakini walikuja kupata mali na mafanikio wakiwa kwenye ndoa

Kuna hawa wafuatao kwa mfano

Rais wetu Jakaya Kikwete
Mfanya biashara maarufu kule marekani Russel Simons
Kuna huyu ambae aliwahi kuwa tajiri wa kwanza duniani Warren Buffet
Mfanyabiashara wa mafuta Tanzania anaitwa Hilal Hamad Hilal mwenye kampuni ya Phantom Oil Tanzania
Wapo watu wengi sana ninaowafahamu hata nikiweka majina yao hapa haitakuwa na maana ila wapo

Hii dhana ya "TAFUTA KWANZA HELA" kwanza halafu uoe tunaitoa wapi?Tukikusanya watu wenye mafanikio duniani wale ambao walioa kwanza kisha mafanikio yakaja ni wengi kulinganisha na wale ambao walitafuta kwanza kisha wakaoa

Wakati Bob Marley anaoa alikuwa hata mtaa wa pili kutoka alipokuwa anaishi walikuwa hawamjui,lakini baada ya kuoa nadhani kila mmoja anajua kilichotokea

Maisha yana kanuni zake na sisi tuna kanuni zetu,cha msingi ni kuangalia kama kanuni zetu hazikinzani na kanuni za maisha na hapo tutafanikiwa

Mkuu,tunalishana uongo mwingi sana na unakuja kutugharimu kwenye maisha yetu ......!!
 
Nilichosema mimi usiipe pesa kipaumbele kwenye ndoa,dada yangu alianza maisha na chumba kimoja lakini sasa wana nyumba tatu tena zenye hadhi na gari na wanapendana mpaka raha japokuwa ndoa yao ina miaka 15,jambo la msingi ni upendo wa kweli na mkisharidhiana mnaishi vyovyote tu PESA NI IBILISI UKIIPA KIPAUMBELE INAKUVUA UTU WAKO.

Hiyo bahati ya dada yako usiote kuipata kirahisi ndugu,,,,,,!
 
Hivi usipokua na mpango wa kununua gari au kujenga nyumba kwa mfano, utatafuta hela ili uifanyie nini?Mi nadhani watu wanaitafuta hela wakiwa tayari wana mipango wa nini matumizi ya hizo fedha.

Na wangapi wanapanga na wakizipata hawaendi sawa na mipango yao!!!!!
 
Ni sawa sikatai kuna cases kama hizo....lakini sio haki kuwahukumu maskini wote kwa staili hiyo. Mimi nna ndugu zangu kibao walioanza kwa staili ya kukaa chumba kimoja sasa hivi wana hali nzuri na ndoa zao ziko vizuri tu....hao matajiri wanaogeuka nimewaona kwenye bongo muvi tu kwenye real life sijawahi kuwaona kiukweli

haya shos!!!!
 
Aisee pesa ndio kula kitu na hio amanii unayoona katika ndoa za watu na kupata taama ya kujiingizaa ni pesaa ndugu yangu! Tafuta pesa halafu tafuta kisu kikalii dunia itakujuaa tuuuuu ndugu

pesa ndo kila kitu jamani,,, watu wanabisha tu hapa
 
wanaoongoza kwa michepuko ni wanaume walio na hela au ni wanawake walioolewa na wanaume wasio na hela nyingi? Michepuko inachochewa zaidi na Tamaa au umasikini au utajiri?

Kuna mipango ya kutafuta hela, na mipango ya kutumia hela. ukiwaza upande mmoja tu wa shilingi itakusumbua. lazima uwe na yote kwa wakati mmoja.

Sijui ninaposema mipango unachagua kuamini nini. una point ya msingi ila haina corelation na ninachojaribu kukisema... Unaona, unapanga, unatake over. Hela haiji tu... lazima uwe na mipango ya kuzipata, mipango ya kuzibakisha na kuendelea kuziongeza.... ukiacha kimoja wapo utakuwa unazunguka tu hapo ulipo.

Hii ipo kwa wazungu sana au kwa wabongo wachache sana walioshauriwa vibaya,

Hao unaosema masikini wana jeuri saana kwa taarifa yako. Labda ukute ameoa mtoto wa tajiri au mdada mwenye hela kumshinda yeye kama hatokuwa makini na kucheza karata yake vizuri inamlazimu kuwa hivyo...

''Money talks but has nothing to say'' again ''Money is a good servant but a very bad master''. Whatch out how you treat money, can be either your servant or your master... choose wisely and be the MASTER.

Mie sema yooote lkn bila hela ni bureee....... na kma ni mume nataka awe nazo kabisa..... sio aje na mipango kma ya serilakali ya tz isiyotimia siku zote..
 
Wewe unavyojua matunzo ni kitu gani?

Kuna watu hawana pesa na kke anatunzwa na hana maradhi,sijui kama unalijua hilo

Kwa akili yako ya ajabu naona unaweza kudhani kutunzwa ni kuwa na iPhone 5,kwenda saloon,kuwa na Gari,kuwa na nyumba kali na mengine ya kufanana na hayo,hayo sio matunzo bali ni matatizo tu

Binadamu ana mahitaji yake ya msingi,akishapata uwezo wa kuyatim iza hayo mengine ni utashi tu,binadamu anahitaji kula bila kujali anakula chakula gani na cha gharama gani, kulala bila kujali analala kwenye kitanda cha gharama gani,kuvaa bila kujali anavaa nguo ya gharama gani na mengine ya kufanana na hayo

Najua unaweza kuniona kama mwendawazimu fulani hivi lakini najua ni kwasababu hujui kitu kuhusiana na ukweli wa maisha,ngoja ukiendelea kuwepo kwenye dunia hii utakuja kukumbuka haya

You know nothing about God,so acha kabisa kuen delea kujionesha vile ambavyo hujui kitu

Mungu unamjua wewe?
Yaani kwa akili yako kama ya panzi unadhani Mungu anategemea kitu ambacho binadamu amekitengeneza ili afanye mambo yake,wewe ni wa kuhurumiwa kabisa

Hebu acha kuchekesha watu we binti,hujaolewa halafu unadai ndoa ni pesa,sijui kama uko sahihi wewe

Acha kuishi kwenye ndoto,tafuta watu ambao wamekua na wamekaa muda mrefu kwenye ndoa halafuy waulize kwa adabu halafu uone watakuambia nini cha kujifunza kama unataka kuishi maisha halisi

Labda cha kukumbuka kuhusu hili ni vile ambavyo nilivyocheka nilivyosoma haya maelezo yako!

Naona umekuja na hasira lkn huo ndio mtazamo wangu kunibadilisha huwezi...
 
Upeo wako WA mwisho kufikiri ni PESA tuu, pesa zisizo na idadi kamili!! bado hadi sasa hujajua definite amount of money worth for you!!!
Think of ideas first then materials will follow you!!!
Unatoka kwnye necessary demands unakimbilia kwnye luxurious ones!!!!
Hekima & busara hata mfalme Suleiman aliiomba kwa Mungu licha ya Ukwasi wake woooote!!!

tinna CUTE!!!!

Uwezo wng wa kufikiri ndio huo na huwezi kubadilisha hata........
 
Last edited by a moderator:
Sorry for the money itself so we dont give a damm
marriage is more than finding money but there is a lot of incomplete marriage and reasons to that ploblems its not about money®®®®®®
 
Niliachana na kipenz changu kwa sababu ya ukata,yy alaikuwa anataka ndoa au tuishi pa1 but mm nilikuwa cjajipanga kitendo kilichopelekea amtafute mwenye kuweza kutimiza malengo yake
Kwa msisitizo hela ni muhimu,Ndio maana inafika miaka 2 ndoani watu wamechokana kisa mipango haiendi,kulumbana tu,kulalamika etc
 
1: status; hata uwe na wake mia bila hela utaishia kuitwa mjinga usie na akili
2: Mipango; bila hela hakuna mipango itakayopangika zaidi utakesha ukiota mipango,,,, na ukioa kilaza ndo kabisaaaaaaaaaa!!!!!!!!! utahisi una mikosi ya kila rangi.
3: Watoto; yes watoto ni furaha na faraja baraka kutoka kwa mungu..... but bila hela utawaona ni mzigo na kuchukia mama yao eti haijui nyota ya kijani anaijua ya bluu tu!!!!!!!!!!!!!
Ushauri; tafuta hela,, pata hela,,, waza kuoa over!!!!!"
shikamoo upo?
 
Mimi naomba niishie hapa dada ila kama unataka mume mwema mshirikishe sana Mungu lakini kama pesa ndio kipaumbele sahau mume mwema.

Mungu namshirikisha ktk kila nifanyalo,,, mume mwema mwenye pesa atanipatia muda ukifika
 
Back
Top Bottom