Umuhimu wa kuwa flexible katika kusaka pesa

miamiatz

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
288
500
Katika kusaka pesa huwa tunashauriwa sana kusimamia tunachokiamini na kukomaa nacho. Hili halina ubishi.

Ila kuna experience inayoashiria kuwa mazingira yanavyozidi kubadilika umuhimu wa kuwa flexible nao unaongezeka.

Haijalishi unataka kufanya biashara ya vitu ama ya ujuzi wako muhimu sana kuwa flexible.

Ongezeko la uhitaji wa kuwa flexible ndio unaopelekea watu kufanya kazi tofauti na masomo waliyosomea.

Hii inaashiria pia utafutaji wako wa maarifa lazima nao uwe flexible. Kuna wakati utalazimika kutumia maarifa tofauti tofauti kufikia lengo flani.

Mathalan: Kuna kipindi niliwahi shikilia msimamo wa kufungua mini supermarkets kadhaa maeneo tofauti tofauti.

Bahati mbaya kila nilipotafuta fremu yenye ukubwa wa kutosha eneo ambalo lina wateja wengi tarajiwa wa bidhaa za mini supermarket nilikosa. Madalali wakawa wananipeleka maeneo ambayo itachukua miaka mpaka kuchangamka.

Ilinilazimu kuwa flexible na kuhamia kwenye trading business. Katika trading business kanuni ni simple buy -- sell or buy -- store -- sell once price has gone up.

Umuhimu wa flexibility umenifanya kuona haja ya kuwa na jukwaa la crowdsourcing hapa Tanzania. Mana kuna watu wengi wanahitaji huduma zilizo na ubora na kuna watu wengi wanajua kutoa huduma kwa kiwango cha juu ila linkage inakosekana.

Hii ndio sababu ya kuweka post iliyotangulia yenye maudhui ya kuwataka wale wenye muda wa ziada kujiunga na miamia web based project management portal ambapo kazi yetu kubwa itakuwa kubridge the gap.

Bahati nzuri huko kutakuwa na wataalam wa kila kada na sio full time job kwaiyo hata kama mtu hana nafasi ya kufanya kazi mwezi mzima ataweka indication tu kuwa yupo occupied na projects za wakati huo zitakuwa hazimhusu.

Lengo lingine la kuwa na wataalamu mbalimbali ktk jukwaa moja ni kulifanya jukwaa liwe na nguvu zaidi.

So be flexible guys mambo yanaenda speed sana ukiwa rigid mambo yatakupita. Ukipishana na fursa sehemu mwenzio anaiokota. Mungu hatokulazimisha uikubali fursa aliyokuletea. So grab it before it's grabbed.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Avatar

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
10,789
2,000
Mbona umeongea mambo mengi alafu hayana coordination....?

Unataka kusema nini?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom