Umuhimu wa kufatilia na kurekebisha baadhi ya vifungu kuhusiana na sekta ya mifugo

Borosilicate

Member
Feb 27, 2023
21
17
Tanzania ni miongoni mwa nchi tano bora zinazoongoza kwa kuwa na mifugo mingi barani Afrika.

Hivo kuchangia mojamoja katika ukuzaji wa uchumi kupitia mazao mbalimbali yatokanayo na mifugo kama vile: maziwa, nyama na ngozi.

Hivo basi ili mradi uzalishaji upate kushamiri ni muhimu vitu vya msingi kuzingatiwa kuhusiana na mifugo hususani afya ya mifugo.

Lengo la kuandika Uzi huu ni kwamba idara kiujumla inayohusika na afya ya mifugo (Veterinary) inafanya kazi Kwa kusuasua kutokana na Sheria ya Matibabu kutokufanya kazi inavotakiwa.

Kwa sababu kikawaida mfano kwa idara ya afya ya binadamu (medical) inafanya vizuri kwa sababu inafata mpangilio na Sheria yake inafanya kazi inavotakiwa. Yaani mfano mtu anavyoumwa au kuonesha dalili za ugonjwa fulani, hawezi moja kwa moja kupewa tu dawa pasipo kufata utaratibu unaotakiwa.

Ambapo ni lazima kuonana na daktari ambaye atakuhoji kwa ajili ya kuchukua historia kisha, utaandikiwa vipimo kwa ajili ya uchunguzi wa maabara kutokana na dalili za ugonjwa husika na historia, na moja kwa moja vipimo vya maabara ndio huwa mara nyingi vinasaidia kutoa majibu kuhusiana na ugonjwa husika,n a kama ikigundulika majibu ni chanya (positive) basi mgonjwa ndipo hupatiwa dawa.

Sasa tukirudi upande wa afya ya mifugo (veterinary), utaratibu kama wa medical huwa haufatwi kabisa, yaani tukisema tufanye uwiano ni asilimia labda 10% tu ya wamiliki wa mifugo ndio huwa wanafata utaratibu. Kwa hiyo kwa asilimia 90% zilizobaki hazifati utaratibu kwahiyo ni sawa tu kusema utaratibu kwamba haufatwi kwa upande wa veterinary.

Ukifatilia kiundani si kwamba wataalamu wa afya ya mifugo (veterinary) kwamba hakuna ila ni kwamba wapo wengi tu, ndio maana si ajabu hata mtaani mtu akisikia kuhusu mtaalamu wa maabara ya mifugo anashangaa.

Kwa sababu utaratibu haufatwi kwahiyo inakuwa ni ngumu kwa mtu wa maabara ya mifugo kufanya kazi, kwasababu mnyama akiumwa kinachofanyika zinaangaliwa dalili tu (pathognomonic signs) kisha mnyama anapatiwa dawa pasipo kufanyiwa vipimo vya maabara.

Ndio maana ni ngumu hata watu wenye fedha kuwekeza katika ujenzi wa vyuo, hospitali na kliniki za wanyama ni kutokana utaratibu kutokufatwa.

Ombi langu ni kwamba hili jambo litazamwe kwa jicho la pili, kwa ajili ya mustakabali mpana wa maendeleo ya nchi, kwasababu utaratibu ukifatwa kutakuwa na faida nyingi sana kama vile:

1. Vijana wa Kitanzania kupata ajira.

2. Uzalishaji wa mazao ya mifugo kuongezeka.

3. Kugundua mapema na kuzuia magonjwa yatokanayo na mnyama kwenda kwa binadamu (zoonotic disease) mfano Kimeta (Anthrax), Kifua Kikuu (T.B) na Kichaa cha Mbwa (Rabies).

4. Kukuza uchumi wa Taifa kupitia uuzaji wa mazao yatokanayo na mifugo nje ya nchi.

Ni hayo tu, karibuni kuchangia hoja.
 
Ikiwa kwa watu tu serikali imeshindwa kuja na mpango mahsusi na imilivu wa huduma za kitabibu kwa wananchi wake kupitia bima kwa wote (NHIF);

1. Unadhani kwenye mifugo inaweza kuwa rahisi kiasi hicho?

2. Na kama inawezekana, je unaweza kudadavua namna utekelezaji utakavyofanyika huku ukiainisha gharama ambazo zitakuwa imilivu kwa wafugaji?

3. Kwa maoni yako, unadhani kukosekana kwa huduma za wataalam wa mifugo ndiyo tatizo kubwa kuliko mengine yanayoikabili sekta ya ufugaji?
 
ikiwa kwa watu tu serikali imeshindwa kuja na mpango mahsusi na imilivu wa huduma za kitabibu kwa wananchi wake kupitia bima kwa wote (nhif);

1. unadhani kwenye mifugo inaweza kuwa rahisi kiasi hicho?

2. na kama inawezekana, je unaweza kudadavua namna utekelezaji utakavyofanyika huku ukiainisha gharama ambazo zitakuwa imilivu kwa wafugaji?

3. kwa maoni yako, unadhani kukosekana kwa huduma za wataalam wa mifugo ndiyo tatizo kubwa kuliko mengine yanayoikabili sekta ya ufugaji?
Kuhusu Kwa binadamu iko wazi kwamba Sheria ipo na utaratibu unafanya kazi, lakini Kwa mifugo utaratibu kuhusu swala la kitabibu haufatwi kabisa naongea hivi nikimaanisha Kwa mfano hivi ungejisikiaje
ukiwa unaumwa ugonjwa serious mfano malaria halafu haupimwi wala nini halafu unapewa labda Dawa za typhoid kisa wamecheki dalili wakaona una dalili labda za typhoid lakini kiuhalisia tukifata vipimo ni unaumwa malaria.

Umezumgumzia matatizo kwenye sekta ya mifugo, kuhusu matatizo ni kweli yapo mengi lakini swala la afya ya mifugo ndo swala la msingi zaidi kwa sababu mifugo kama itatokea itakuwa haina afya bora, itashindwa kuishi Kwa hiyo existance yao haitokuwepo.
 
Back
Top Bottom