SoC02 Umuhimu wa kuajiri mtaalamu wa saikolojia (psychologist) mashuleni

Stories of Change - 2022 Competition

Mhorani

Member
Jan 11, 2022
7
6
Ufaulu wa mwanafunzi unategemea vitu vingi ikiwemo nyenzo za kusomea mfano vitabu, marudio ya mitihani nk
Walimu bora, mazingira mazuri ya kujisomea nk

Lakini kumekuwa na tatizo kubwa la wanafunzi wengi kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao au hata kijamii nikimaanisha kufeli mitihani nakushidwa kuishi vizuri na jamii inayo wazunguka.

Ukijaribu kumuuliza kila mtu kama amewahi kushuhudia mwanafunzi aliye kuwa anafanya vizuri sana darasani lakini akaja kuanguka katika mitihani yake ya mwisho haita mchukua muda mrefu sana kufikiria kukupa jibu la ndio pengine akakupa na histroria kidogo ya jinsi gani ambavyo watu walishangazwa na matokeo hayo.

Kwanini kuna umuhimu wa kuwa na mtaalamu wa saikolojia mashuleni, afya ya akili inabeba dhamana kubwa sana ya maendeleo ya mwanufunzi iwe kwa kufanya vizuri katika masomo na kumuandaa kuwa mwananchi bora yapo mazingira kadhaa wa kadhaa ambayo kwa namna nyingi yanaweza kumuathiri mwanafunzi kwa uchache ni kama ya fuatayo

Matatizo ya kifamilia,
Ukuaji,
ushawishi wa kundi lika.

Matatizo ya kifamilia
Katika familia mwanafunzi anaweza kuwa anapitia matizo mengi ambayo si rahisi kumshirikisha rafiki au mwanafalilia mfano unyanyasaji wa kingono, vipigo, wazazi kutengana nk


Ukuaji au balehe
Ukuaji una chukuliwa kwa njia tofauti kwa maana kila mtu anaupokea tofauti msukumo wa ukuaji unaweza kumpelekea mtu akapata matatizo ya akili mfano kujichukia pengine kwasababu ya kusemwa (Bullied)

Ushawishi wa kundi lika
Katika ukuaji wa huwezi kumtenga mtoto na kundi lika na pengine si rahisi kumtoa kwenye kundi lika baya mfano kumshawishi kutumia vilevi kuna umri ushawishi wa kundi lika unaonekana ndio maisha yanavo takiwa kuwa

Sababu hizi pamoja na nyingine nyingi zinaonyesha ni muhimu kiasi gani kuwa na mtaalamu wa saikolojia shuleni, kutokana nguvu ndogo inayo hakikisha afya ya akili ya mwafunzi inakuwa sawa. Shule zina taratibu za kuwapa majukumu walimu ya malezi (walimu wa malezi). Ambao kwakiasi kikubwa ndio wanategemewa kufanya majukumu ya saikologia ambapo pia wanatakiwa kuingia darasani kufundisha. Kutokana na umuhimu na ukubwa wa changamoto wanashindwa kukidhi uhitaji wanazidiwa na majukumu. Pia mwalimu wa malezi anasimama zaidi kama mwalimu wa kawaida mfano kutoa adhabu nk hupunguza ukaribu wa mwanafunzi na mwalimu wa kuweza kufunga changamoto zake.

Eneo jingine linalo tegemewa kuhakisha ukuaji wa mwanafunzi ni familia ambapo siku hizi wazazi wengi wapo busy hivyo inakuwa ngumu kuhakisha wanafatilia maendeo ya watoto wao. Pamoja na kwamba matatizo mengi yana anzia kwenye familia mfano unyanyasaji wa kingono hivyo ni ngumu kutatua.

Ufaulu wa mwanafunzi katika masomo na kijamii kunetemea sana afya ya akili tunapoteza mafanikio ya wanafunzi wengi sana kwa kutokuwa na wataalumu wa saikolojia mashuleni pamoja na kwamba serikali inaitoa kozi vyuoni ( bachelor of education in psychology ) lakini haina ajira za wataalamu hawa, tatizo la wimbi kubwa la kufeli wanafunzi lingeweza kutatuliwa angalua kila shule ingekuwa na wataalumu japo wawili katika kila shule. Ingekuwa ni chanzo cha kumfundisha mwanafunzi kujitambua, kumuoka mwanafunzi na unyanyasaji nk hii isinge ongeza tu ufaulu mashuleni lakini ingesaidia sana kuandaa vijana bora katika jamii.
 
Back
Top Bottom