Nimeona watu wakipost thread zao wakitafuta wachumba, waume /wake ila wanapoweka vigezo vya umri wanaambiwa mnaowatafuta wameshaoa ila sijaona wakisema unaowatafuta wameshaolewa au wanasema ulikuwa wapi muda wote huo hujaolewa au hujaoa.
Mimi binafsi sioni kama kuoa au kutoolewa mapema hao watu wana matatizo, wengine ni majukumu tu wengine wamechelewa kwenye kujipatia elimu.
Naamini mtu anaweza kuoa au kuolewa akiwa na umri wowote kwani ndoa ni sehemu ya kusaidiana wawili katika mahitaji ya kimwili na kiroho ikiwemo kufarijiana kushauriana ili kuondoa upweke.
Ikumbukwe kuwa watoto ni zawadi kutoka kwa muumba kwani wengine husema ukichelewa kuoa utapata shida ya kuzaa hayo ni ya binadamu wazazi wetu wa zamani wamezaa mpaka miaka 47 ila sasa ukiwa na miaka 28-30 unaonekana umechelewa kuolewa.
Wana Jf hii imekaaje ndivyo nionavyo mimi sijui nyie.