Umri wa dunia ni upi hasa?

Naamini mmepotea hoja iliyotolewa hapa kwa upuuz wenu na mabishano yasio na matinki.

Turudi kwenye hoja DUNIA INA UMRI GANI.

Kama sehemu kubwa ya dunia inaamini mungu yupo, na ndiye aliyeiumba dunia, huwezi ku address suala la umri wa dunia bila ya ku address jinsi dunia ilivyoanza.

Na huwezi ku address dunia ilivyoanza bila ya kuzungumzia suala la mungu.

Kuna watu wanafuatisha biblia/ quran kama neno la mungu, na watataka kutupa majibu kwa mujibu wa biblia/ quran.

Mtu akifanikiwa kuonyesha kwamba hizi habari za mungu wa biblia/ quaran ni uzushi tu, tunaondoa theory moja na kuendelea kuangalia zingine.

Majadiliano ya mungu kwenye uzi wa umri wa dunia yanahusika vizuri sana.

Labda unaweza kuona hayahusiki kama unaangalia mambo kijuujuu tu.
 

Hujajibubswali.

Kabla ya mungu kuumba viumbe.

Pale alipokuwa anaumba ulimwengu.

Kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekaniki?

Alukuwa hawezi au hakutaka tu?

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote na upendo wote aruhusu uovu uwezekane katika ulimwengu wake?
 
you debate with a conclusion in mind....

One that you have failed to disprove.

This godhead cannot exist, because the very idea is inherently self contradictory.

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote na upendo wote aruhusu mabaya yawezekane kwenye ulimwengu wake?
 
Hivi naombA niulize kitabu cha mwanzo aliandika nani?
Means alikuwa Amekaa na mungu af alikuwa anamuona mungu kwa hiyo mungu huyo yupo physical?

Biblia imeandikwa na watu tu.

Hakuna yeyote anayeweza kuthibitisha kwamba mungu yupo. Nimewapa nafasi mara kibao hapa wathibitishe hilo, sijaona uthibitisho.

Mungu gani anashindwa mtihani wa logic wa darasa la saba?
 

Kama wewe unaamini Mungu hayupo na omani yako haikuruhusu kuamini hvyo una haja gani ya kuleta mabishano yasipna na umuhimu tena ya kupotosha umma.
Kuna vungi sana vya Mungu ambavyo binadamu hata ufanye vipi kuvijua hata ungeamua kutumia maisha yako yote kwenye utafiti utaambulia zerro.
 

Nani kaleta mabishano?

Unajuaje kwamba mimi nimeleta mabishano na sijaletewa mabishano kwa mualiko maalum?

Kati yangu ninayeuliza maswali ya kutaka uthibitisho wa kuwapo kwa mungu, maswali ambayo sijajibiwa, na hao wanaosema mungu yupo, lakini hawawezi kujibu maswali ya kumhusu huyo mungu, nani anapotosha umma hapa?

Hivyo vingi vya mungu ni vipi? Na umejuaje kwamba ni vya mungu?

Unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo? Au unaendekeza hadithi za mapokeo tu zisizo na uthibitisho?
 
Unaliza maswali ambayo hata ww mwenyewe unaamini hayana majibu na hata ww pia ajibu huna, unachokifanya hapa ni kurefusha maada. No point
 
Habari nzima ya kuwapo kwa mungu muweza yote na mwenye upendo mkuu imezaliwa kutoka kwa baba aitwaye uzembe na mama aitwaye woga.

Uzembe unataka majibu mepesi kwa maswali magumu. Hivyo kila swali likiwa gumu na halieleweki, kwa mfano, dunia imeanzaje? Uhai umeanzaje? Baada ya kifo kuna nini? Wazembe wameopenda kujibu kwa habari za mungu, bila uchunguzi. Kwa imani tu.

Woga umesiliba habari ya mungu kwa kutisha watu kwamba ukihoji uwepo wa mungu unafanya kufuru na utachomwa moto milele na milele.

Binadamu wa leo kwenda na imani king'ombe ng'ombe tu bila kuuliza maswali ya wazi kabisa inasikitisha sana.
 
Unaliza maswali ambayo hata ww mwenyewe unaamini hayana majibu na hata ww pia ajibu huna, unachokifanya hapa ni kurefusha maada. No point

Hayana majibu au majibu yake huyajui?

Hivi ni vitu viwili tofauti.
 
Hata ww mwenyewe huyajui wala huna

Hilo siyo swali langu.

Swali uliloulizwa hujajibu, ulilojibu hujaulizwa.

Nimekuuliza, hayana majibu au majibu yake huyajui?
 
kwa hiyo kuna mungu wengi tu, kila imani na mungu wake?

Ndio maana yake, na huu ulimwengu hauishii kwenye hii dunia yetu na jua lake, ukitoka kwenye hii solar system yetu a trilion miles, kuna majua (suns) nyingine zina solar system zake, na kuna planet kuna viumbe hai, viumbe hivyo ktk hizo planet wengine wametuzidi maarifa, na planet nyingine tumewazidi maarifa, ndio kwanza wanaulizana jua limesimama au linazunguka,na hata rangi zao ni tofauti, wapo viumbe wa blue, yellow nk, na majua yanatofautiana kwa ukali na nguvu za mionzi, my point miungu ipo kibao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…