Umri umefikia, natafuta mwanamke wa kuoa ila awe na hela

naegemea kipande hiki ndugu , kusema unahitaji mke kwa sababu uko mpweke ni kama unajiongopea ndugu yangu!
unaweza kuwa ndani ya ndoa ukawa mpweke kuliko unavyotarajia na nmna yakufanya hautakuwa nayo tena.
nazungumza hivyo kwa sababu mimi nina ushahidi wa hilo ndugu.
ndoa haihitaji kikisingizio chochote ili iwepo, sijui upweke ama kuongeza familia ,kupata watoto ,ama furaha ama kupata wepesi wa maisha au kuongeza kipato nknk, ukitumia sababu hizo kuingia kwenye ndoa utakutana matokeo yalio tofauti na matarajio.

tulia kwanza, fanya upembuzi yakinifu, jipange, tena jipange haswa, hakuna namna utakayo kwepa majukumu kama mwanaume hata kama huyo mwanamke angekua na hela kiasi gani! kwanza sijui kama wanawake unawajua vizuri ndugu yangu, hela yao haliwi na mwanaume!
utanyanyasika mpaka uombe poo!!!

jipange , maana utafika kipindi mpaka ngua ya ndani utashindwa kununua brother!

japo najua badiko hili haumaanishi lakini ukweli ndoa nikama hivyo nakuzidi, lakini pia inaweza kuwa kinyume chake, kila jema.

Wewe ni therapist mzuri sana, niombee tu.
 
Upo sahihi kabisa
Kuna watu wanadharau mawazo ya watu humu lazma watambue
Mawazo na fikra za watu haziwezi kua sawa hata siku moja,ndomana hata manabii waliotumwa na mungu kuna watu walio wapinga na kuwakataa na ndio maana upinzani pia upo hakuna kusiko na upinzani na ni hatari sana kumlazimisha MTU afikiri kama unavyofikiri
 
Kumbe yule single mama alikuacha shida ilikuwa hapa
Jitahidi kufanya kazi kwa bidii ..pesa ya mwanamke ina sabufa ndani.
Ukishaweza kusimama mwenyewe utakuwa huru zaidi kuliko utegemee kusimama kwa pesa ya mwanamke.

Laiti ungelijua ungekaa kimya ila ni haki yako kuchangia
 
Kuna watu wanadharau mawazo ya watu humu lazma watambue
Mawazo na fikra za watu haziwezi kua sawa hata siku moja,ndomana hata manabii waliotumwa na mungu kuna watu walio wapinga na kuwakataa na ndio maana upinzani pia upo hakuna kusiko na upinzani na ni hatari sana kumlazimisha MTU afikiri kama unavyofikiri

Chukua bia nitalipia
 
Nimekupa ushauri huo kaka yangu
Unaweza kuuchukua au kutouchukua.
Kama unaona haufai ni sawa tu ila kutengeneza ideas za kutegemea hela ya mwanamke utakuja ulie.
Tafuta pesa zako kwanza

Pesa nilizonazo hazinitoshi


Halafu hivi vimesemo vya tafuta pesa kwanza nilishazoea njoo na msemo mwingine labda nitakuelewa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom