Umri gani wa kupishana kati ya watoto?

wenzetu wapemba mtoto akifikisha miezi nane wanampeleka mtoto kwa bibi iliwatafute mtoto mwingine
 
wenzetu wapemba mtoto akifikisha miezi nane wanampeleka mtoto kwa bibi iliwatafute mtoto mwingine
Dah,umenikumbusha jinsi wapemba walivyo na watoto wengi,ukichanganya na ndoa ya wake wengi,balaa.
 
miaka miwili siyo mbaya. ila napenda kuna mdada humu alisema akiwa na mtoto wa miezi mitano akawa mjamzito na sasa analea watoto wake na wamekua kwa hiyo inategemea
 
ni umri/muda gani wa watoto wanaozaliwa wanastahili kupishana
Kwa ujumla child spacing inategmea AFYA ya mama, njia ya kujifungua (kawaida au kwa operesheni), hali ya ELIMU na UCHUMI wa watengenezaji wa hao watoto, kwa watu maskini ujumbe ni kuwa spacing iwe si chini ya miaka miwili, lakini kama mama ana afya njema, anajifungua kwa njia ya kawaida na uchumi wako unaruhusu basi ruksa kuchagua spacing ambao ni convenient kwenu hata kama ni chini ya mwaka mmoja.
 
umri wa miaka 3-4 ni mzuri sana kwa maendeleo yote ya mama, mtoto na uchumi wa familia. Tusivute wala kukawia sana!
 
mimi nimeolewa nikiwa 26, next wk nagonga 35, nimeshajingua watoto 4, na funguo nimeweka hata ikija tsunami haifungui! sasa nakimbizana kuwatafutia riziki nikiwa na nguvu kibao! msiogope kuzaa!

It as if mnamwingilia Mungu..........okey mie nitapishananisha miaka 10 ili akikua anisaidie kulea mwenzie..............lakini ni lazima kuwa na watoto zaidi ya 1?
 
mimi nimeolewa nikiwa 26, next wk nagonga 35, nimeshajingua watoto 4, na funguo nimeweka hata ikija tsunami haifungui! sasa nakimbizana kuwatafutia riziki nikiwa na nguvu kibao! msiogope kuzaa!
Umejitahidi sana,bravo.
 
Kweli umejitahidi. Siku hizi watu wengi wanaishia watoto wawili na wenyewe wanatutoa watu jasho.
mimi nimeolewa nikiwa 26, next wk nagonga 35, nimeshajingua watoto 4, na funguo nimeweka hata ikija tsunami haifungui! sasa nakimbizana kuwatafutia riziki nikiwa na nguvu kibao! msiogope kuzaa!
 
mama anapokuwa mjamzito mpaka kujifungua kuna mabadiliko mengi sana hutokea mwilini mwake(physiological changes). Hivo anahitaji muda wa kutosha ili aweze kurecover hayo mabadiliko yaliyotokea na kurudisha virutubisho mbalimbali vilivyopungua mwilini. Hii itasaidia hata ujauzito unaofuata ucwe na shida zozote kama upunguf wa damu nk. Kiafya ili kupata mtoto mwingine inashauriwa isipungue miaka miwili.
 
Back
Top Bottom