Umoja wetu ndiyo nguvu yetu

Bob Malik

Senior Member
Oct 1, 2019
121
404
Ukoo wetu hauna dini moja. Kuna Wakristo na kuna Waislamu.

Kuna wengine hawana dini kabisa. Ila some tunachangia mababu. Na tunapendana.

Siwachukii Waislamu kwa kuwa mimi ni Mkristo. Siwachukii wakatoriki kwa kuwa mimi ni Mlutheri.

Kuna wanasiasa wenye nia ovu hasa hasa kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) wameanza kupenyeza chuki za kidini miongoni mwa watanzania. Hii kitu ni mbaya sana.

Tuwapinge wale wote wanaoeneza propaganda zenye nia ya kutugawa kidini. Sisi ni wamoja.

Bandari zetu ndio urithi wetu. Tupinge mkataba wa kinyonyaji bila kujali dini zetu.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom