Umoja wa Mataifa wakatishwa tamaa na COP25

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,190
4,103
Mazungumzo ya Mabadiliko ya Tabia Nchi ya Madrid (COP25) yamemalizika kwa hali ya kuvunja moyo, baada ya wachafuzi wakubwa wa mazingira kupinga nyongeza ya jitihada za kukabiliana na ongezeko la kiwango cha joto duniani.

Waandaaji wa mkutano waliwakusanya washiriki kutoka mataifa 200 hadi zaidi ya Ijumaa, siku ambayo ilipangwa mkutano huo wa wiki mbili kumalizika.

Mwishoni kabisa mwa mkutano, wajumbe walikubaliana kwa miito ya pamoja katika jitihada kubwa ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuchukuliwa hatua kadhaa za kuyasaidia mataifa masikini kudhibiti wa athari za uharibifu wa mazingira.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema amekatishwa tamaa sana na matokeo ya mkutano huo. Alisema jumuiya ya kimataifa imekosa nafasi muhimu ya kukabiliana na athari za kimazingira, lakini hawatoacha kushiriki jitihada za kuulinda ulimwengu.

1576491156706.png
 
Back
Top Bottom