Wasalaam
Nikiwa na miaka 10,Kuna binti alikua anakuja nyumbani kucheza na ndugu wa kike
Mara nyingi kalionesha viashiria vya kunipenda Sana Kama kuniletea tuvyakula au matunda kutoka kwao,lakini katika michezo iliyojumuisha jinsi zote kalipenda kuwa timu Mimi
Kuna muda kalinirukia na kunikumbatia,utoto wangu nilichukia na kukafokea...muda kaliniangalia kakawa Kama kanalia,haitoshi kaliwatuma sista zangu wanambie
Sasa Kuna muda nami nkaanza kukaelewa,basi nkasema niandike barua,kwa sababu tulikua shule moja,madarasa tofauti,nilikaazima daftari lake,then kurudisha nkaweka na barua,loh...natoka darasani nikakuta kanalia kamezungukwa na watu wengi kweli huku kameshika ile barua yangu,wanajadili waende kwa mwalimu au waende nyumbani kwetu,mzee mkali kweli..?
Nashukuru msala uliisha salama...tukawa maadui kweli ,sijui kako wapi siku hizi
Mwingine chuo,nimesoma kipindi hicho chuo Fulani maarufu Sana mjini(DSM)...katikati kabisa ya jiji,sifa za chuo hicho zilinifanya kuchukia tahadhari,ikiwa Ni pamoja na kukaa mbali na madem lakini starehe pia
Nilifanya mkakati wa kujibrand Kama mshamba na nilifanikiwa,wakati wenzangu wanapiga pamba Safi,mi nilipiga mashati yangu ya kitenge na wakati mwingine sare za kwaya(Napenda kwaya nilikua naimba kwaya)...nkasema ntakaa mbele na urafiki na wahuni sitaki
Kweli nilikutana na mazingira niliyotegemea
Kuna Dada mmoja alikua mzuri sana ku attract/ku draw attention ya watu wengi
Huyu Dada Kuna siku nimekaa alone na solve,nkashangaa Yuko mbele angu ananiangalia muangalio sio wa kawaida... session ya mchana naingia natafuta siti,nkashangaa ananielekeza sehem ya kukaa,keshawahi siti mbili,hapa na hapa kaanza kuniomba nimsaidie vimaswali viwili vitatu,now act siko vizuri,kumbe ananichora,demu alikua kafanya EGM Yuko vizuri maths...
Hapa na hapa kaniomba no. Ya simu...sms za usiku mwema na mbwembwe zikawa nyingi,wanasema hakuna mkate mgumu mbele ya chai...akawa akinikuta na Dem mwingine ana mind Hadi anabadilika rangi...muda wote huo mi nilikua namvutia pumzi
Boom langu lilikua halijatoka,akawa ananipa kampani kweli kwa issue za stationery na msosi lakini hata mambo madogo madogo
Shida ikaja siku nilipoamua kujua mstakabari wetu kimahusiano...asee,haikuwa poa ,tuligawana mbao...lakini mwisho wa siku kila mtu alibaki Kama anaumia huku akijifanya jeuri
Ninyi wanawake hiki huwa Ni Nini?
Sent using
Jamii Forums mobile app