Umewahi kutana na mwanamke wa hivi?

Umewahi kutana na mwanamke wa hivi?

CarloJesus

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2019
Posts
431
Reaction score
838
Wasalaam
Nikiwa na miaka 10,Kuna binti alikua anakuja nyumbani kucheza na ndugu wa kike

Mara nyingi kalionesha viashiria vya kunipenda Sana Kama kuniletea tuvyakula au matunda kutoka kwao,lakini katika michezo iliyojumuisha jinsi zote kalipenda kuwa timu Mimi

Kuna muda kalinirukia na kunikumbatia,utoto wangu nilichukia na kukafokea...muda kaliniangalia kakawa Kama kanalia,haitoshi kaliwatuma sista zangu wanambie

Sasa Kuna muda nami nkaanza kukaelewa,basi nkasema niandike barua,kwa sababu tulikua shule moja,madarasa tofauti,nilikaazima daftari lake,then kurudisha nkaweka na barua,loh...natoka darasani nikakuta kanalia kamezungukwa na watu wengi kweli huku kameshika ile barua yangu,wanajadili waende kwa mwalimu au waende nyumbani kwetu,mzee mkali kweli..?

Nashukuru msala uliisha salama...tukawa maadui kweli ,sijui kako wapi siku hizi



Mwingine chuo,nimesoma kipindi hicho chuo Fulani maarufu Sana mjini(DSM)...katikati kabisa ya jiji,sifa za chuo hicho zilinifanya kuchukia tahadhari,ikiwa Ni pamoja na kukaa mbali na madem lakini starehe pia


Nilifanya mkakati wa kujibrand Kama mshamba na nilifanikiwa,wakati wenzangu wanapiga pamba Safi,mi nilipiga mashati yangu ya kitenge na wakati mwingine sare za kwaya(Napenda kwaya nilikua naimba kwaya)...nkasema ntakaa mbele na urafiki na wahuni sitaki


Kweli nilikutana na mazingira niliyotegemea

Kuna Dada mmoja alikua mzuri sana ku attract/ku draw attention ya watu wengi

Huyu Dada Kuna siku nimekaa alone na solve,nkashangaa Yuko mbele angu ananiangalia muangalio sio wa kawaida... session ya mchana naingia natafuta siti,nkashangaa ananielekeza sehem ya kukaa,keshawahi siti mbili,hapa na hapa kaanza kuniomba nimsaidie vimaswali viwili vitatu,now act siko vizuri,kumbe ananichora,demu alikua kafanya EGM Yuko vizuri maths...

Hapa na hapa kaniomba no. Ya simu...sms za usiku mwema na mbwembwe zikawa nyingi,wanasema hakuna mkate mgumu mbele ya chai...akawa akinikuta na Dem mwingine ana mind Hadi anabadilika rangi...muda wote huo mi nilikua namvutia pumzi

Boom langu lilikua halijatoka,akawa ananipa kampani kweli kwa issue za stationery na msosi lakini hata mambo madogo madogo

Shida ikaja siku nilipoamua kujua mstakabari wetu kimahusiano...asee,haikuwa poa ,tuligawana mbao...lakini mwisho wa siku kila mtu alibaki Kama anaumia huku akijifanya jeuri

Ninyi wanawake hiki huwa Ni Nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UDSM iko katikati ya mji? Nafikiri ameeleweka tu pale aliposema chuo maarufu katikati ya mji.
UDSM darasani kuna nyani na ngedere [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukikaa vibaya Cafeteria unanyang'anywa lunch na ngedere.

Turudi kwenye mada. Mleta mda labda ulimchelewesha sana huyo binti mpaka akapata pumziko jingine ila akawa hana sababu hivyo alikua anakulia timing tu siku umpe sababu.
 
Mi Kuna Kabinti Kalikua Kakishare Kila Kitu Na Mimi Nakuonesha Dalili Zote Zakunitaka Bt Nilipokaeleza Hayo Mambo Kalinitukana Sana...
Dah! Nilijisikia Ovyo Mno Bt Mpaka Leo Sijawah Eksipiriensi Hili Jambo...
Wadada Mtusaidie Hua Mnamaanisha Nini Mnapodhihirisha Dalili Zote Zakumhtaj Mtu Then Mkiambiwa Mnachange??
 
Chuo maarufu ni UDSM vingine ivi sema chuo tu tutakuelewa
Mkuu Nimesema katikati ya jiji...UDSM iko katikati ya jiji?

Chuo maarufu DSM Ni UDSM[emoji44],kwa ajili ya Nini(subject to...)...mfano ukisema chuo maarufu Cha usafirishaji utaitaja UDSM,Au chuo maarufu Cha ufundi utaitaja UDSM,Mkuu toka nje ya box

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha mbali hapo kwenye kale kabarua kukaweka ndani ya daftari. Yaani wote ndio tuliijua njia hiyo ya kuifikisha barua yetu. Tatizo kubwa, hao wenzetu tu. Hawakuwa na akili sawa sawa. Miye, aliipeleka uanjani kwenye tea break. Shule nzima yenye watoto zaidi ya 400. Masichana yote yakakusanyika kuisoma ile barua yangu. Kwani maneno yalikuwa mengi basi. Machache tu! ##Nakupenda. Halafu muandiko wa darasa la pili.
Sitasahau aibu iliyonipata. Kila mtu alikuwa adui yangu pale shuleni. Leo sijui kamefia wapi wala sikutamani hata kukaa darasani naye tena.
 
Mi Kuna Kabinti Kalikua Kakishare Kila Kitu Na Mimi Nakuonesha Dalili Zote Zakunitaka Bt Nilipokaeleza Hayo Mambo Kalinitukana Sana...
Dah! Nilijisikia Ovyo Mno Bt Mpaka Leo Sijawah Eksipiriensi Hili Jambo...
Wadada Mtusaidie Hua Mnamaanisha Nini Mnapodhihirisha Dalili Zote Zakumhtaj Mtu Then Mkiambiwa Mnachange??
Na wewe ungemwonyesha kwa vitendo! Sometimes hawa viumbe hawataki maneno mob...!
 
Back
Top Bottom