Serikali: Vitasa janja (smart Lock) kiboko ya wapangaji wanaokwepa kodi ya pango

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,433
49,102
Serikali imeanzisha utaratibu wa kufunga Vitasa janja yaani smart lock kwenye nyumba zake za makazi ya kupangisha Ili kuwadhibiti Wanaokwepa Kodi ya Pango.

Swali, kwani hakuna program au software ya kucheza na hii mbinu ili kupata upenyo?

===

magorofa-pic.jpg

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema ujenzi wa majengo ya maghorofa nchini unaotekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ni moja ya mkakati wa serikali katika utekelezaji wa sera ya matumizi bora ya ardhi na kujenga nyumba za kutosha kwa watumishi wake.

Hayo ameyasema leo, Machi 29, 2023 Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa majengo mapya mawili ya ghorofa kwa ajili ya kuishi watumishi wa wa umma, moja likiwa limejengwa eneo la Magomeni Kota litakalo chukua kaya 16 na lingine Msasani litakalobeba familia 12 yote yakiwa na jumla ya thamani ya Sh10.3 bilioni.

Katika maelezo yake waziri huyo amesema serikali inatambua umuhimu wa makazi bora kwa wananchi wake ambapo yamefikia 3 milioni kwa nchi nzima huku akieleza yanaongezeka kila mwaka na kufikia mahitaji ya nyumba 200,000.

“Nawapongeza TBA kwa kuzingatia matumizi bora ya ardhi kwa kujenga nyumba bora na miradi hii inatekelezwa kwa kuzingatia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 inayoelekeza maeneo ya kuendelezwa,”amesema.

Profesa Mbarawa amesema ilani hiyo inaelekeza kujenga nyumba yenye uwezo wa kuchukua Kaya nyingi jambo lilofanywa kwenye mradi huo wa Magomeni Kota, kwa kujenga jengo la kuchukua familia 16.

“Shughuli yetu kama serikali ni kusimamia kuhakikisha nyumba zinapangishwa kwa bei na fuu na kwa watu binafsi wenye nia njema ya kuungana na taasisi hii milango iko wazi hivyo mnakaribishwa,”amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TBA, Daud Kandoro amesema ghorofa lilojengwa Magomeni Kota ambalo ujenzi wake ulianza mwaka 2021 linaghorofa saba na litachukua kaya 16 na kujengwa hadi kukamilika kwake wametumia Sh5.6 bilioni.

“Wakati lile tulilojenga Masaki linaghorofa tano litakuwa na uwezo wa kuchukua kaya 12 na linathamani ya Sh4.6 bilioni na kukamilika kwakwe kutaleta manufaa makubwa ikiwemo kuiongezea taasisi yetu wigo mpana wa mapato hivyo kuweza kujiendesha,”amesema.

Kandoro amesema katika kuhakikisha wanaepukana na adha ya kukusanya kodi nyumba hizo zitakuwa zinatumua vitasa janja (Smartrock,) kuwadhibiti wanaokwepa kulipa kodi kwa wakati na kuhakikisha taasisi hiyo inapata fedha ya kuendeleza miradi mingine ya watumishi.

Mwananchi
 
Wanakandamiza maskini tu ila mafisadi ndio kwanza wanayasaidia kutuibia.
 
Wanakandamiza maskini tu ila mafisadi ndio kwanza wanayasaidia kutuibia.
Wewe naye chuki kwa Rais aliyepo imezidi mpaka umejikuta umeuza akili na utu kidogo uliokuwa umebakiza! Huyo maskini anayepangisha kwenye maghorofa ya NHC yuko wapi unioneshe? Tunajua ulikuwa unafaidika na utawala uliopita ila just move on hata km umetumbuliwa tulia tu utakumbukwa mbeleni.
 
Back
Top Bottom