OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 419
- 670
Waziri wa Fedha na Mipango amependekeza kugawa TIN kwa watu wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, na taarifa hizi ziende sawa na NIDA ili kulipa kodi kwa usahihi.
Baadhi ya watu wamehusianisha namna hii ya ukusanyaji kodi na Kodi ya kichwa, kitu ambacho naona ni kupotosha ukweli kuhusu kodi ya kichwa.
Kwanza lazima tujua kuwa na namba ya mlipa kodi haimaanishi unalipa kodi, kwa mfano kila mwenye leseni ya udereva ana namba ya mlipa kodi, ila sio kwamba wanalipa kodi.
KODI YA KICHWA
Kodi hii ilikuwa inalipwa na kila mtu mwenye kichwa na unapewa kibali, hivyo ukikosa kibali unashtakiwa kwa kutolipa kodi. Ni kodi ambayo ilikuwa na udhaifu mkubwa kwa kuwa watu wa kijijini na porini walikuwa ni ngumu kufikiwa ili kulipa kodi hiyo.
Kodi inayopendekezwa ktk bajeti ya mwaka 2022/23 ni kila mtu anapofanya muamala, sio kuwa atalipa kutokana na umri wake, bali ni kuongeza wigo wa kufanya malipo yanayofanyika yakatwe kodi.
Hakuna mtu ambaye atafuatwa kudaiwa kodi kwa sababu ana namba ya mlipa kodi. Kumbuko kwenye kodi ya kichwa unafuatwa kuhakikisha kama una kibali.
Kwa sababu hiyo, wale wanaodhani kuwa kodi hii ni sawa na kodi ya kichwa wanapotosha.
Signed OLS