hahahaaaa watu wanafurahisha sana, mie kuna siku nilienda kwenye harusi na hubby sasa yeye alikuwa mwenyekiti wa kamati kila saa yuko busy na wanakamati wenzie mimi nikawa kwenye meza idle tuu aaah ikawa kila mziki ukipigwa najichanganya nacheza kikweli kweli akistuka akiona hanioni nilipokaa ananifata tunadance wote mara kaitwa tena looh!!
hee!! si ukapigwa wimbo wa twist kuna mahali unatwist hadi chini kisha unanyanyuka na twist pole pole hadi juu sas mie hizo ndo zangu niliteremka na beat na kurudi nazo kwa raha zangu nilikuwa nacheza pembeni maana naepukaga walevi kubambia halafu anajidai pombe isijezua tafrani bure. Ile kuja kuhamaki kumbe kuna jamaa mmoja muda wote alikuwa ananitazama mie ninavoserebuka nikajikuta tumekutana uso kwa uso nikampotezea kurudi kumtizama tena akanikonyeza aaah nikahama mahali pa kuchezea nikaenda upende mwingine.
Wakati wa kuondoka ukumbini maana tulikaa hadi mwisho as hubby ndo mwenyekiti wa kamati akakaa na yeye kunitizama ninavotembea heee!! nusu hubby amstukie nikajibana kwa hubby huku nimemshikilia mkono looh
Konyezo likikukuta kwa umpendae au ulie medmire linanoga ila kwa anonymous au stranger aaah mie kwangu linakera.