Vi rendra
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 3,267
- 5,599
Hello, it's me again
Ndugu zangu kuna jambo naliona sana huku duniani kuhusu mahusiano ya kimapenzi wa ke/me tunaojihisi tunawapenda sana! Mahusiano mengi sikuhizi hayana mvuto/hayafiki mbali kwakua ukweli ni kwamba tunaukimbia upweke /woga wa kuwa pekeyako bila mpenzi wa kukuamsha na "Good morning my love" Na "Pole na kazi" text nk
Tofauti kati na upendo na kukimbia upweke ni ndogo sana, pengine kuna watu hawafahamu kabisa kwa jinsi zinavyoshabihiana ( upendo & woga wa upweke)
Ukijiona : 1. Unajihisi unalazimisha mapenzi /kuwa na mtu fulani, unalazimisha akutendee yale ambayo mpenzi hutenda bila shuruti ( kukujali kwa kihisia)
2. Hata akitenda vibaya unatafuta sababu ya kuhalalisha matendo hayo, kwa mfano anaweza kutokupigia simu kutwa siku2 na hajibu meseji utasema tu kwakua hayuko online atakua busy na kazi.
3. Hata asipotaka amani, unafosi amani, ikitokea kutoelewana wewe ndio unafosi muelewane ili uwe na amani kwasababu amani yako inaletwa na yeye!
4. Unaficha hisia zako kwa ajili yake, ili uwe yule ambae unahisi anamtaka , unaficha kama umekasirika kwakua akijua hilo pengine atakuona sio muelewa, Unataka akuone msikivu utajikuta unaacha hobby zako kwa ajili yake
5. Unahisi kama yeye ndio kwa ajili yako, ukimpoteza hutapata mwingine, kwakua unaogopa upweke ambao umeletwa na dhoruba za hapa na pale za mahusiano yako yaliyopita unahisi kama huyo mtu kajitolea kuokoa jahazi kwahiyo anastahili kupewa-caring ya juu sana maana ameokoa jahazi lililokua likizama.
zipo dalili nyingi zaidi, ukiziona hizo chache basi ndugu yangu humpendi mtoto wa mama mkwe bali unakimbia upweke ulionao!! Cha kufanya ni kuelekeza nguvu kumuona therapist sio kushupalia watu wa wenyewe!
Sent using Jamii Forums mobile app