WomanOfSubstance
Platinum Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 975
Huwa najiuliza, hivi binadamu tuna raha gani ya maisha? Je wewe mwenzangu huwa unajiuliza maswali gani ya kifilosofia juu ya maisha?
Job 7:7 ¶ O remember that my life is wind: mine eye shall no more see good. {shall...: Heb. shall not return}. Job 10:12 Thou hast granted me life and favour, and thy visitation hath preserved my spirit. Compare and contrast the two bible verses you might get your answer
Pia ushawahi kujiuliza usawa wa binadamu uko kwenye jambo lipi? Maana binadamu tumetofautiana sana - tumetofautiana rangi, mwonekano, akili, busara, hekima, sauti, hulka, haiba, mahitaji, matakwa, mapenzi, tajiriba, n.k. n.k.
Je, ni kipi ambacho kinatufanya sote tuwe sawa?
dah...wos leo umenirudisha kwenye darasa langu la philosophy 101, advanced philosophy, truth and knowledge, epistemology, mind, language, and logic, existentialism and phenomenology, etc.
Damn i was good in that class....lol
Sisi ambao wenye kuamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu tunaamini kuwa tumeumbwa kwa maumbo, tabia, tofauti za rangi, mwonekano, akili, busara, hekima, sauti, hulka, haiba, hurka, jamii na tofauti zingine ili tupate kujuana (Kufahamiana). Vile vile Utajili na umasikini pamoja na ufukara ni mtihani Anaowapa Mola waja wake, katika mitihani ya kila aina iliyomo katika maisha ya binaadamu, mitihani mizuri na mibaya yote ni mitihani. Mfano, binaadamu anapopewa mali basi ajue kuwa ni mtihani huo kuwa vipi ataitumia mali yake, akijaaliwa kupewa elimu atajaribiwa pia kuwa vipi ataitumia elimu yake, akipewa akili na siha, vyote atajaribiwa navyo kuwa vipi atatumia neema hizo.Pia ushawahi kujiuliza usawa wa binadamu uko kwenye jambo lipi? Maana binadamu tumetofautiana sana - tumetofautiana rangi, mwonekano, akili, busara, hekima, sauti, hulka, haiba, mahitaji, matakwa, mapenzi, tajiriba, n.k. n.k.
Je, ni kipi ambacho kinatufanya sote tuwe sawa?
Ukifikiria kwa undani kabisa hayo uliyoandika, unaweza kujiuliza hivi kwanini mtu aamue kuwa mwizi na kufisadi jamii kubwa wakati maisha yenyewe ni mafupi sana? Hivi kuhodhi mabilioni ya pesa kwa wizi, ghiriba na udanganyifu ni sahihi wakati kuna watu wanataabika? Kwakweli kila mtu akifikiria kuwa maisha ni muda mchache nadhani dhana hiyo inatosha kabisa kuacha ujambazi na kuishi katika misingi inayokabalika.
G nadhani ukifanya kazi 16 hours u wouldnt call tht raha...plus raha ya hapa duniani huwezi kuipata kama hujapata tabu kwanza..there's no such thing as a free lunchkwani wew WOS raha kwako ni nini ?
maana mie naona raha zimejaa kila kona ya dunia hii, raha ndogo ndogo na kubwa kubwa....................
Maisha ya mwanadamu hayazidi miaka 70 wachache kuenda hadi 100 kwa wale waliojaaliwa kuishi umri mkubwa, achilia mbali life expectancy ambayo kwa Watanzania kufuatia UKIMWI kuwa tishio na magonjwa mengine kama shinikizo la damu, cancer etc,hayazidi miaka 50.
Chukulia kuwa toka kuzaliwa hadi uweze kusimama kwa miguu yako mwenyewe kimaisha, ukijumlisha na miaka ya kusoma hadi chuo ni miaka 25. Halafu ongezea miaka mingine kama 15 ya kujijenga kimaisha ( kuanzisha familia yako na kujiweka sawa kiuchumi) kwa walio wengi ukiondoa wachache wenye kukuta wazazi wamewawekea kila kitu au labda waliorithi, au kubahatisha kupata mali upesi kwa njia halali au labda zisizohalali! Hapo tayari ni miaka 40. Ongezea hapo miaka mingine 20 ya consolidation na kustaafu = 60.
Baada ya hapo ni mtu kupumzika na ama kula jasho lake au kuanza msoto mkali wa kutafuta riziki baada ya kustaafu, ilhali mwili na hata akili vimeanza kuchoka kwa miaka 10 = 70 ambapo ndio umri mrefu wa wastani wa binadamu kuishi.
Huwa najiuliza, hivi binadamu tuna raha gani ya maisha? Je wewe mwenzangu huwa unajiuliza maswali gani ya kifilosofia juu ya maisha?