Umewahi kuchapa wanao ?

Kuchapa ni short cut...
umerudi kazini umechooka na uko full na stress..
unaambiwa mtoto hataki kula ugali...
sasa kwa nini upoteze muda wa kumuelimisha...na kumbembeleza?
unamcharaza hadi anakula....na ukubwani anakushukuru..lol
na kesho akisikia mlio wa bajaji nje anajua baba/mama anakuja matonge yanateremka.....
 
sio adhabu !kwa hiyo tuwe makini na adhabu
 
Kongosho umenena vyema sana sana.
mimi ninachapa kulingana na kosa na hili sihitaj ushauri na hata mgen akiingia kwangu atagundua kwamba hapa ni mahali tofauti.

huwa nashindwa sana kuelewa hivi NGO's zinazosema stop canning ilihali wanasahau kwamba ni adhabu ambayo inaumaiza lkn inakumbusha na kuogopesha kurudia kosa. sikatai ikizidi humfanya mtu kuwa sugu lkn tukasahau kwamba hata adhabu nyingine huleta usugu miongoni mwa watu. mfano ukimwambia mtu aruke kichura kama adhabu ama aite mvua akizoe atafanya mchezo tu wala haitakuwa na impact kwake.

swala si viboko ila swala ni mtoto anakosa gani hadi aadhibiwe?
 
Last edited by a moderator:



hell yeah,,
well said..
 
Yaani nikianza kumchapa mtoto , ile anaanza kulia kwa uchungu , hua nasisimka na roho ya huruma inanijia, najikuta namwacha , ila mimi ni mwepesi sana kumnasa mtoto makofi.
 


utotoni ulichapwa? utotoni tu? lol
 
Yaani nikianza kumchapa mtoto , ile anaanza kulia kwa uchungu , hua nasisimka na roho ya huruma inanijia, najikuta namwacha , ila mimi ni mwepesi sana kumnasa mtoto makofi.

Wengine tuna bahati ya kupata watoto walio well behaved.

I have never raised my hand to hit my child.

I believe in dialogue but I'm also cognizant of the fact that it doesn't work for everyone.
 
sio tu kuchapa bali kucharaza kisawasawa..... Fimbo naitumia kama njia ya mwisho baada ya kuzungumza nae mara kadha kusipotoa matunda.... Hata biblia inaruhusu bakora
 
Wengine tuna bahati ya kupata watoto walio well behaved.

I have never raised my hand to hit my child.

I believe in dialogue but I'm also cognizant of the fact that it doesn't work for everyone.

Duh Kumbe NN ni baba Hongera
 
Kusema kweli sijawahi kuchapa mtoto
Ok kwa wale mnaosisitiza tuwachape angalau iwe fundisho
Unamwambia mtoto lala chini ndo unaanza stick
na je Ni fimbo ngapi zinamfaa mtoto?
Ama unaweza chapa mikononi ,miguuni nk nk
Nakumbuka nikiwa Primary kuna ticha alikuwa anatuchapa, fimbo yake ni ile ilikuwa na matawi mengi yeye anaita nyuki..
Ukiitwa na ticha tu unajua nyuki mfululizo leo ..unajipanga maana alikuwa hachagui pa kuchapa
 
This is true!

Mimi ninawachapa hata sasa, mtoto wangu mdogo ana miaka mitatu tu, kuna kitu alikuwa anafanya sikuwa nikikipenda, nikwa naongea nae kwa upendo aache but kesho yake anarudia hivyohivyo, siku hiyo nikampa viboko vichache na miaka yake mitatu, hakika nakuambia hajawahi kurudia hadi ninapoandika hapa

 

Well said! They always know hapa nimekosea na mzazi alikuwa na kila sababu ya kunichapa! Wa kwangu huwa hachelewi kuja kuomba uswahiba akijua amemkasirisha dingi!
He is a good kid though
 


There is no rules when it comes to disciplining a kid! Just spank em while they still know what they have done is wrong!
 
Nadhani karibu asilimia 90 ya wanajf tulichapwa viboko utotoni kwa makosa tuliyofanya,ebu jichunguze,kama ulichapwa na kama imekuathiri kisaikolojia au la na linganisha na watoto wa leo ambao hawachapwi.au linganisha mtoto wa kiafrika na kizungu kimaadili,na watoto wa kizungu hawachapwi.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mtoto wangu ni mtundu mno,na ana mwaka na nusu,utundu ukazidi mpaka akawa anapiga watoto wenzie wakija nyumbani,basi sasa hivi akifanya tu mambo yako namchapa vikono vyake anaacha,adhabu hii ni nzurinilimradi isizidi sana,iwe na kipimo.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
wa kwangu ni watundu mno hivyo kila ninapokaa nikiwa nyumbani lazima pembeni niwe na fimbo maana niligundua makofi au kumfinya huwa anachukulia tunacheza lakini akiniona nimechukua fimbo adabu debe...
 
Naomba nisisitize kumchapa mtoto ni kinyume na haki za binadamu. Nitarudi baadae kufafanua kwa evidence.
 
Naomba nisisitize kumchapa mtoto ni kinyume na haki za binadamu. Nitarudi baadae kufafanua kwa evidence.

mtoto ana haki yakupewa adhabu pale anapokosea. Ila isiwe deadly one kama kumchoma moto, kumuumiza,kumnyima chakula nk. Nakumbuka mama yangu kama ukiwa na kosa na ni muda wa kula anawaacha mle vizuri,baada ya kula mnaanza kukumbushana makosa. Alikuwa tayari kukubembeleza kula ili usilale njaa maana kuna muda fimbo zikizidi unamchomoka na kulala kwenye banda la mbuzi, loh!!.. Nikikumbuka enzi zile huwa nacheka mwenyewe.
 
It depend on the situation unaweza mchapa mwanao au kumpa adhab kutegemeana na kosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…