Umeshawahi kulipigania penzi lisivunjike lakini mwisho wa siku ukakubali kushidwa

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Nakumbuka miaka 6 nyuma kuna binti niliwahi kumpenda sana sasa katika mahusiano tulifikia kile kipindi kile mahusiano yapo too toxic kila nikijitahidi kuliokoa penzi kuliokoa tusiachane lakini wapi.

Mwisho wa siku nilikubali matokeo niliumia sana lakini mwisho wa siku ilibidi nikubali kumwacha wakati yeye alishaniacha siku nyingi sana.
 
Penzi likichuja, best way ni kukubali matokeo mapema iwezekanavyo, ili uumie halafu iishe, upone uendelee na maisha (move on). Ukiwa king'ang'anizi kwa mtu ambaye kimsingi ameshakuacha, utajikuta una maumivu yasiyoisha.

Hayo ni mateso ya kujitakia kwani ulimwengu una machaguo kibao...unachotakiwa ni kufumbua macho tu.
 
Ahsante mkuu! Kwanza nimegundua kama mapenzi yameisha ni kukubali tu matokeo ila ukilazimisha mtu abaki kwako utaishi kwa stress .Maana hujui karudi kweli ama yupo tu kwa muda.

Love hurts, ukiwa mwepesi ku let go and move on husaidia sana kwenye nyakati hizo. Unaweza kutumia kila mbinu kumshawishi lakini ukaishia kuumia tu na usiombe hayafanye hayo yote akiwa tayari kwenye penzi jipya.
 
Love hurts, ukiwa mwepesi ku let go and move on husaidia sana kwenye nyakati hizo. Unaweza kutumia kila mbinu kumshawishi lakini ukaishia kuumia tu na usiombe hayafanye hayo yote akiwa tayari kwenye penzi jipya.
Kiukweli nimejifunza sahivi hamna kubembeleza mtu ukiniacha naachika kweli. Ila tatizo kamoyo nako kanakua kagumu kuelewa 😒
 
Back
Top Bottom