Tuliwahi kutumia gharama nyingi ili kulinda mahusiano lakini mwisho wa siku chali

Mr sule

JF-Expert Member
Oct 14, 2021
607
1,097
Katika harakati za huku na kule miakaa kadhaa iliopita.

Nilikuta na binti aliekuwa anasoma chuo flani Tanzania kwenye Whatsapp.

Baada ya kuwa nje ya Tanzania, nilianza kuwatafuta ndugu ambao sijawasiliana nao siku nyingi.

Katika harakati hizo nilikuwa kila namba ninaona iko whatsaapp na sijawasiliana nayo basi nilikuwa naacha salaam.

Baada ya week moja huyu Binti alijibu salama, nikamuuliza kama yeye ni muhusika ninaemtafuta, akasema sio yeye na hapo nikapotezea.

Lakini binti alioneka kuwa interest kutaka kunijua zaidi na kuniuliza maswala kadhaa.

Hiyo salama iliendelea na mwisho wa siku tukajikuta kwenye mahusiano

Kama unavyojua nguvu ya mapenzi, nilizama kwenye penzi licha yalikuwa mahusiano ya mbali, na nilianza kumsupport kwa kila kitu wakati iko chuo, yaani kuanza vocha mpaka ada nilihusika mimi.(alitokea kwenye familia isiokuwa na uwezo)

Alipomaliza chuo, nilifikiri kumpa biashara na wakati huo nilikuwa na Duka la urembo hata before sijawah nje ya nchi na nilipanga kumkabizi hilo duka.
Kabla sijamwambia nia yangu ya kumpa hilo duka alionekana kuanza mambo mengi.

Nijituma kutoa matunzo ili nimuepushe na tamaa cos mahusiano yalikuwa ya distance. so njia bora niliona ni kumpa support kadri ya uwezo wangu.

Lakini mambo mengi yalizidi, akanivuruga akili alafu ukizingatia kabisa mpaka ndugu niliwashirikisha. ilibaki nirudi Tanzania na tufanye utaratibu wa kuishi pamoja.

Nilijaribu kumwelezea jinsi ninavyonijisikia kwa tabia alio nayo sasa lakini hata text alikuwa ajibu tena. nilipiga simu sana nikabembeleza sana lakini kila siku ni ugomvi tu.

Niliona inatosha na nikasema najiongelesha kimoyo moyo Mungu alikuwa na makusudi yake na niwe tayari kupokea matokea yote.

Ilinipa wakat mgumu sana maana niliwekeza sana kwake na siwah kufkiria jambo hili kutokea.

Maamuzi yangu yalikuwa sahihi lakini nilikutana na mtu ambae si sahihi alafu mimi huwa si mtu wa kujutia maamzu yangu na sipend tabia hiyo. huwa sina haraka ya kuchukua maamuzi na ninapofanya maamuzi yakienda tofauti na nilivyotarajia bas huwa sipend kujilaumu ila naweza kuumia kitu kuwa tofauti na nilivyotarajia.

Baada ya kumsahau na kuwa kwenye jimbo lingine. leo anarudi na story mbaya. hana hata kazi mjini, support niliompa alijaribu kufanya biashara na ndugu zake lakini biashara hakufanya vizuri mwisho wa siku ikafa kabisa.

Mpenzi wake ambae kwasasa ni Ex wake alimuibia vitu vyote vya ndani alipokuwa ameenda kufatilia biashara mkoa B.(vitu hvyo mimi ndo nilikuwa nanunua cos nikirud niwe naishi kwake badala ya kukaa hotel)

Kwaiyo anahisi mimi kuna kitu nimefanya ndomana mambo yake hayaendi.
Ila nilimsamehe siku nyingi na sina hata chembe ya kinyongo, nampenda Yesu na kumfuata.

Mimi ni mwepesi wa kusamehe na kusahau. juhudi zangu nyingi saiv nkumtumikia Mungu wangu. nisaidie ndugu jamaa na marafiki na yeyote anahitaji msaada wangu.

Anayonifanyia Mungu ni makubwa sana na mimi ninarudisha mema kwa kuishi na watu wake vizuri.

Lakini Dear Ex anataka tena turudiane. nilimjibu katika mambi ambayo hayatawezekana katika maisha yake basi aweke na hili kwenye List.

Lei nimshea story zangu mbili za Mapenzu na nimejiskia tu kufabya hvyo na si kwamba nahitaji ushauri.
Asante
IMG_9147.jpg
 
Hongera kwa ku-move on.
Haya maisha sisi kama wanaume naweza kusema tunapitia changamoto nyingi sana za mahusiano ambazo kwa namna moja ama nyingine usipokuwa makini zinabadilisha kabisa mustakabali wa maisha yako kwa ujumla.

Story yako inataka kufanana na yangu, jinsi mlivyoanza ndivyo hivyo na sisi tulianza, baadae majuto yakawa mjukuu.

Nimejifunza haya maisha usije ukaweka nguvu zako na akili zako zote kwa jinsia pinzani, iwe ke au me, maisha yanabadilika na mambo pia yanabadilika.

Umdhanie ndiye utafika nae nchi ya ahadi yeye anataka kuishia njiani.
 
Kweli mkuu, ogopa sana mtu kukuyumbisha
 
Mkuu kufahamiana tu mtandaoni ndo ukazama na kuwekeza gharama zote hizo.....kama vipi endelea naye maana hao viumbe akili zao zinafanana sana.

Ndugu, Mungu anatukutanisha katika njia tofauti, alafu watu kufamiana mtandao si kwamba ndo hakuna upendo. Dunia saivi inaenda na nyakati na online ni njiia rahis kukutana na watu.
Wapenzi wakikutana mtandaoni si swala la kushangaa mkuu
 
Niliwahi kukutana na sister fulan mkubwa kidgo kunizidi umri, nilikua nampenda yule sister ila alikua ananiakataa.

Nikakaza sana mpaka akakubali sasa issue ikawa kwenye matunzo yeye akanichukulia kama mume aise yaani anataka nimgaramie kuanzia asubui mpaka jioni alafu kila jmos nimpe hela ya saluni.

Kwakua nilikua nampenda na lengo lilikua niwe namla tu Kama mchepuko nikawa natimiza yote hayo kila siku nampa ten ya kula na kila jmos nampa 25k.

Sijui aliniroga mpaka sielewagi, tulikaa kama miez 3 namuhudumia hivo ila kuna siku mizimu ya kwetu ikapata nguvu nikasema hivi nafanya upumbavu gani huu!! Nikapiga chini siku hiyo hiyo.

Nilipiga hesabu hela zangu alizokula nikagundua nilitumia zaid ya milion 1 mpaka muda huo nikasema huyu mchawi sio kawaida nikapiga chini.
 
We have the same story...

Sema ulinizidi kuhonga master.
 
Back
Top Bottom