Umeshawahi kukutana na balaa la nyoka?

Basi hii mada ya nyoka leo naogopa hadi kukaa kwenye sinki la choo, maana nilishawahi kuona video nyoka anatokezea chooni. Leo kazi ipo
Tangu nione hiyo video mtu aling'atwa na nyoka kwenye tako basi kila kuingia chooni naogopa vibaya, tena ilikuwa Uingereza kama sikosei
 
Tangu nione hiyo video mtu aling'atwa na nyoka kwenye tako basi kila kuingia chooni naogopa vibaya, tena ilikuwa Uingereza kama sikosei
Mimi kuna kipindi nilisahau ila leo woga umezidi upya...yaani nikitaka kukaa nainuka mwenyewe, ndoo zisipotumika leo sijui[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kuna nyingine nyoka anatokezea kwenye sinki la choo halafu anarudi ndani.
 
Mimi kuna kipindi nilisahau ila leo woga umezidi upya...yaani nikitaka kukaa nainuka mwenyewe, ndoo zisipotumika leo sijui[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kuna nyingine nyoka anatokezea kwenye sinki la choo halafu anarudi ndani.
Mi uoga upo kila siku, na mbaya zaidi kuna chamber ilikanyagwa na gari yani kila nikienda toi mawazo km yote, itabidi nimwagie oil huwa namwagia hot water sometimes,, ni kwikwi huyu mdudu sijui kwanini aliumbwa
 
We muoga sana
Naogopa sana na sijawahi ona kwa macho. Mwaka huu mtoto wangu ilikuwaa usiku tupo nje yeye alisimama kwenye majani ghafla akaja analia amegongwa na nyoka mimi sikumwona ila yeye anasema kamuona wa black ( mweusi). Nilikuwa na jirani yangu akamwangalia akasema huyo sio nyoka atakuwa mdudu tuu wa kawaida mimi sijui kitu.

Tumekaa ndani kama dk 5 hivi mguu ukaanza kuvimba, bahati kuna bodaboda niliagiza msosi akawa analeta akashangaa leo mbona anko mpole sio kawaida yake nikamwambia kuna mdudu kamng'ata anavimba mguu kuja kumwangalia nusu aninase vibao aisee.

Akamfunga mguu kumbeba mbio mpaka kwa huyo mzee anamjua ndio kumpa dawa ya kunywa na nyingine akampaka na kusugulia mguu wote. Akaendelea na dawa hizo siku hadi ilipoisha Yule boda boda alinambia kama nisingekuja kwa dk 10 mbele ulikuwa unamkosa mtoto huyu. Yaani sikulala karibia wiki kwa woga.
 
[emoji125][emoji125][emoji1787]
 
Habari za nyoka zisikie tu kwa wengine, ni hatari sana huyu kiumbe japo ana huruma ambayo wengi hawaijui.

Nakumbuka kipindi hicho tuko kijijini shamba wakati wa mavuno ya mahindi, basi baada ya jua kali nikasema nikapumzike kidogo chini ya Muembe.

Nilishtuka baada ya kumuona binamu yangu akiwa bize anamuua nyoka mkubwa.

Ajabu anasema yule nyoka alikua pembeni yangu kidogo tu nikiwa nimelala fofofo na hakutaka kuniamsha kwa kuhofia huenda ningeruka upande wa nyoka.

Yule nyoka alikua mkubwa sana na nilipata woga kiasi sijawahi tena kurudi shambani pale.

Nilimshukuru sana ndugu yangu na kumuona mtu jasiri na mpaka leo tukikumbuka lile tukio tunacheka na utani wa hapa na pale.

Lakini jinsi siku zinavyoenda nikawa najiuliza, kwa nini nyoka yule hakunidhuru na nafasi ya kufanya hivyo alikua nayo? Kwa nini binamu yangu asingetafuta namna ya kumfukuzia mbali bila kumuua Kiumbe yule ambaye alikua na uwezo lakini hakuamua kunidhuru?

Nyoka ni hatari na mpaka leo picha ya tukio lile inanitesa zaidi ya miaka 16 sasa.
 
Chatu alitaka kunimeza.Lakini kwa vile hii hadithi nimeisimulia mara kadhaa Facebook na wapi,sitaki kuwaboa watu.
Lakini huyu chatu nilikuwa sijui kama ni chatu. Nilidhani ni oversized cobra.
We unasema cobra alikuhurumia. Hayo ndiyo mawazo yangu pia. Nilifanikiwa kumtoroka yule chatu,au alinihurumia?
Siku hiyo chatu alipomitokea ni siku ambayo Kagame alikuja Dar kumuona Kikwete,siku hiyo hiyo.
 
Ulifanya uzembe mkubwa sana yaani kupuuzia, huyo ni Kobra moja kwa moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…