Umepanga kuzaa watoto wangapi?

Acha uoga mkuu hata wenye wawili watatu wanangaika ata kuliko wewe, hakuna mahusiano kati ya kipato na watoto, mimi nina saba wote wako private schools na hawakosi hata siku moja kwenda shuleni eti kisa ada wakati majirani wana moja wa wili wana kuja kufuata msaada wawarudishe shuleni, mimi lazima ni fikishe watoto kumi Mungu akiafiki tawazanani hilo sio suala ila sizai na singo maza kwasbb siko tayari kuhudumia damu isio ya kwangu na sitaki kubagua mtoto wa mtu.
 
Hali ya Maisha na Usasa imechangia kwa sehemu kubwa Watu kupunguza idadi ya watoto wa kuzaa hata wale wa kulea (Wandugu na Jamaa).

Miaka ya zamani Mwanamke mmoja aliweza kuzaa watoto 8 hadi 12.

Maana shughuli za Kilimo na Ufugaji zilichangia pakubwa.

Hawa Wanawake wakileo ambaye anahitaji kuolewa na Mwanaume mwenye kipato na yeye mwenyewe hadi awe amemaliza Masters yake mtaishia kuzaa mtoto 1 ama 2.

Binafsi Mungu akinijalia afya njema, naweza kufikisha 6 ama 8.

Hapa naendelea kuweka mazingira ya wao kuishi na kusoma hadi Chuo Kikuu bila fedha za Bodi ya Mkopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…