Umepanga kufanya nini leo siku ya Pasaka?

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
Kwanza niwatakie heri ya Pasaka kwa Wakristo wote duniani kote.

Naomba niwaambie kitu katika siku hii ya leo muhimu duniani katika maisha yetu.

Tunapoisherehekea Pasaka, tunasherehekea kufufuka kwa Bwana Yesu Kristo.

Tunaambiwa kwamba bila ya Bwana Yesu kufufuka basi Ukristo usingekuwepo.

Hebu jiulize, kama Ukristo usingekuwepo wewe ndugu yangu Mkristo ungekuwa wapi?

Hivyo basi, tufanye matendo yanayompendeza Mungu katika siku ya leo.

Tumia muda wako kumshukuru Mungu, kufanya ibada, kutembelea ndugu, majirani na marafiki bila ya kuwasahau wagonjwa na wenye mahitaji maalum.

Usisahau kutoa sadaka, usiangalie kama wewe ni tajiri au masikini, toa sadaka kulingana na uwezo wako. Kumbuka sadaka ni kitu chochote kile.

Inawezekana kwako ukaona kitu kidogo, lakini yule unayempa kwake ni kitu kikubwa sana.

HERI YA PASAKA KWENU NYOTE
 
Back
Top Bottom