Umeme wa Tanesco: Rais Magufuli anajua kinachoendelea?

ntamaholo

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
12,956
Reaction score
7,006
Wana bodi salam.

Ukiwa mjini na unafanya kazi kwenye majengo makubwa ya mashirika au hotel kubwa kubwa, unaweza toka ofisini usijue kinachoendelea mtaani. Sababu ni kuwa wana automatic power generator. Naamini hata ikulu iko hivyohivyo.

Wiki mbili mfululizo watumiaji wa umeme wa tanesco wako kwenye mgao holela, viwanda havifanyi kazi, shuguli zimesimama, uchumi hauendi kokote.

Kifupi, tangu kuondolewa kwa Prof na kukabodhiwa kijiti aliyekuwa naibu wake, umeme imekuwa shida. Kimsingi kalemani wizara imemshinda mapema sana na hakuna juhudi za kurekebisha hilo, maana hata tangazo la mgao mie binafsi sijalisikia.

Mh Rais, ikulu kuna umeme lakini kwa wazalishaji hakuna umeme, shuguli zimekwama. Bidhaa zimeharibika, mitaji imekata.

Kama ni kuisoma, tarakimu zimesomeka kwa wengi.

Litatue au tusikie kauli yako.
 
Jamani kwa kifupi mgao upo, ikumbukwe kwamba sasa hivi maji kule mtera, kidatu, na kihansi ni kidogo sana. Hii inasababishwa na tanesco kushindwa kutumia maji muda wote sababu hakuna mbadala wa mashine za mafuta km IPTL, wakati wa kiangazi inabidi kuzalisha zaidi kwa mafuta au gasi ajili ya kujisongeza mpk masika. Kwa sasa mitambo ya ziada km IPTL na Symbion yote imezuiliwa kuzalisha umeme, tatizo hili kisha ni mpk mitambo ya kinyerezi II itakapoanza uzalishaji. Hili ndiyo tatizo walionalo Tanesco, hakuna mitambo ya kuzalisha umeme wa ziada, km kutatokea tatizo kwenye plant moja basi mabo yanakuwa km Mtwara na Lindi.

Sent from my SM-A300FU using JamiiForums mobile app
 
Aisee hii shida ya umeme imekuwa kero kubwa sana. Watu kazi haziendi
 
Jamani kwa kifupi mgao upo, ikumbukwe kwamba sasa hivi maji kule mtera, kidatu, na kihansi ni kidogo sana. Hii inasababishwa na tanesco kushindwa kutumia maji muda wote sababu hakuna mbadala wa mashine za mafuta km IPTL, wakati wa kiangazi inabidi kuzalisha zaidi kwa mafuta au gasi ajili ya kujisongeza mpk masika. Kwa sasa mitambo ya ziada km IPTL na Symbion yote imezuiliwa kuzalisha umeme, tatizo hili kisha ni mpk mitambo ya kinyerezi II itakapoanza uzalishaji. Hili ndiyo tatizo walionalo Tanesco, hakuna mitambo ya kuzalisha umeme wa ziada, km kutatokea tatizo kwenye plant moja basi mabo yanakuwa km Mtwara na Lindi.

Sent from my SM-A300FU using JamiiForums mobile app
Sababu ya kuzuia hiyo mitambo isizalishe umeme ni nini?
 
Kalami kutolewa pale msahau, jifunzeni tu kutumia karabai na kupikia gas, mchina na mkaa
 
Kwa nini Rais asijue?Hatupendi ukweli hivyo changamoto kama hizi ni za kawaida
 
Naskia viwnda n vingi sana ndo vinakula umeme hasa... vinasababisha gridi kuwa unstable
 
Mimi najiuliza kwa nini serikali hairuhusu private sector kuwekeza kwenye umeme na kuleta ushindani kwa tanesco? Shirika moja kuhodhi! sector ya umeme nchi nzima inaleta uzembe na kujisahau, private sector waruhusiwe kuwekeza na kuuza umeme kwa wateja kupitia clean energy tu (umeme wa jua na upepo) .

Nchi ina ardhi kubwa na hali ya hewa rafiki kujenga wind na solar farms lakini wao wanapambana na maji, diesel. Wakati wa kubadilika sasa kama kweli kuna nia ya dhati ya kuwa nchi ya viwanda.
 
Jamani kwa kifupi mgao upo, ikumbukwe kwamba sasa hivi maji kule mtera, kidatu, na kihansi ni kidogo sana. Hii inasababishwa na tanesco kushindwa kutumia maji muda wote sababu hakuna mbadala wa mashine za mafuta km IPTL, wakati wa kiangazi inabidi kuzalisha zaidi kwa mafuta au gasi ajili ya kujisongeza mpk masika. Kwa sasa mitambo ya ziada km IPTL na Symbion yote imezuiliwa kuzalisha umeme, tatizo hili kisha ni mpk mitambo ya kinyerezi II itakapoanza uzalishaji. Hili ndiyo tatizo walionalo Tanesco, hakuna mitambo ya kuzalisha umeme wa ziada, km kutatokea tatizo kwenye plant moja basi mabo yanakuwa km Mtwara na Lindi.

Sent from my SM-A300FU using JamiiForums mobile app

We unaongelea maji? Gas imeenda/inaenda wapi?
 
Back
Top Bottom